settings icon
share icon
Swali

Makerubi ni akina nani? Makerubi ni malaika?

Jibu


Makerubi / masherabi ni viumbe malaika wanaoshiriki katika ibada na sifa ya Mungu. Makerubi ndio wa kwanza kutajwa katika Biblia katika Mwanzo 3:24, "Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani y Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia yam ti wa uzima." Kabla ya uasi wake, shetani alikuwa kerubi (Ezekieli 28:12-15). Hema na hekalu pamoja na makala zao zilizomo zilikuwa na uakilishi wa makerubi (Kutoka 25:17-22; 26:1, 31; 36:8; 1 Wafalme 6:23-35; 7:29-36; 8:6-7; 1 Mambo ya Nyakati 28:18; 2 Mambo ya Nyakati 3:7-14; 2 Mambo ya Nyakati 3:10-13; 5:7-8, Waebrania 9:5).

Sura ya 1 na 10 ya kitabu cha Ezekieli huelezea "vile viumbe hai vinne" (Ezekieli 1:5) kama viumbe sawa na makerubi (Ezekiel 10). Kila mmoja alikuwa na nyuso nne -ule wa mtu, simba, ng'ombe, na tai (Ezekieli 1:10; pia 10:14) - na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. Katika muonekano wao, makerubi "walikuwa na sura ya mwanadamu" (Ezekiel 1:5). Makerubi hawa walitumia mbili ya mbawa zao kwa kuruka na zingine mbili kwa ajili ya kufunika miili yao (Ezekieli 1:6, 11, 23). Chini ya mabawa yao makerubi walionekana kuwa na umbo, au mfano wa mkono wa mwanadamu (Ezekieli 1:8; 10:7-8, 21).

Picha ya Ufunuo 4:6-9 pia inaonekana kuelezea makerubi. Makerubi hutumikia kwa kusudi la kutukuza utakatifu na nguvu za Mungu. Hii ni mojapo ya majukumu yao kuu katika Biblia. Mbali na kuimba sifa za Mungu, wao pia hutumika kama kumbukumbu inayoonekana ya enzi na utukufu wa Mungu na uwepo wake kukaa na watu wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Makerubi ni akina nani? Makerubi ni malaika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries