settings icon
share icon
Swali

Maangamizo ni jambo la kibibilia?

Jibu


Maangamizo ni imani kuwa wenye dhambi hatakuwa na matezo ya milele jahannamuu, lakini badala yake “wataangamia” baada ya kifo. Kwa wengi, maangamizo ni imani ya mfuto kwa sababu ya kule kutisha kwa dhana kwa watu kuwa milele yote watakuwa jahannamuu. Huku kukiwa na baadhi ya kurasa ambazo zaonekana kujadilia maangamizo, kwa kuingalia kwa undani kuhusu ni nini Bibilia inasema juu ya mwisho wa wenye dhambi, yafunua hoja kuwa adhabu katika jahannamuu ni ya milele. Imani katika maangamizo yatokana na kule kuelewa vibaya kati ya mojawapo ya hizi kanuni: 1) mshahara wa dhambi, 2) Haki ya Mungu, 3) hali ya jahannamuu.

Kuambatana na hali ya jahannamuu, anayeshikilia mafunzo ya maangamizo anaielewa vipaya maana ya ziwa la moto. Kawaida, ikiwa mwanadamu atatupwa katika tanuru la moto, basi huyo mtu papo hapo ataangamia. Hata hivyo tanuru la moto ni jambo linaloonekana na ni ulimwengu wa kiroho. Sio tu mwili wa mwanadamu kutupwa katika tanuru la moto; ni mwili wa mwanadamu, nafsi na roho. Hali ya roho haiwezi teketea kwa moto unaonekana. Inaonekana kwamba wenye hawajaokoka watafufuliwa kwa miili iliyotayarishwa milele vile waliokoka watafufuliwa (Ufunuo 20:13; Matendo Ya Mitume 24:15). Hii mili imetayarishiwa majaliwa ya milele.

Milele ni sehemu nyingine ambayo wanaoshikilia kanuni ya maangamizo wanakosa kuielewa. Wanashikilia kanuni ya maangamizo hajakosea kwamba neno la Kiyunani aionion, ambalo limefasiriwa na kumaanisha “milele,” kwa maelezo halimaanishi “milele.” Hasa la maanisha “kizazi” au “eon” kipindi maalumu cha wakati. Hata hivyo, ni wazi kuwa katika agano jipya,eon wakati mwingine inatumiwa kutaja muda wa milele.Ufunuo 20:10 yazunguzia kuhusu shetani, kinyama, na nabii mwongo akitupwa katika ziwa la moto na kuteswa “usiku na mchana milele na milele.” Ni wazi kulewa haya matatu hayakomeshwi kwa kutupwa katika ziwa la moto. Kwa nini jaala la asiye okoka kuwa tofauti ( Ufunuo 20:14-15)? Ushahidi wa Kuthibitisha dawama wa jahannamu ni mathayo 25:46, “wakati huo wao (wasiokoka) wataenda mbali kwa adhabu la milele, lakini watakatifu kwa uzima wa milele.” Katika aya hii, jina hilo hilo la kiyunani linatumiwa kutaja kuhusu majaliwa ya wenye dhambi na watakatifu.Kama wenye dhambi pekee wanateswa kwa kipindi basi hata watakatifu watapata uzoefu huko mbinguni kwa kipindi tu.Kama waumini watakuwa humo mbinguni milele, wasioamini watakuwa jahannamuu milele.

Katalio lingine la kila mara juu ya uwepo wa jahannamu ya milele na wanaoshikilia dhana ya maangamizo ni kwamba haitakuwa haki kwa Mungu kuwaadhibu wale ambao hawakuoka katika jahannamu kwa muda usio na mwisho kwa ajili ya dhambi zao. Itakuwaje haki kwa Mungu kumchukua mtu ambaye aliishi maisha ya dhambi, miaka 70 na kumwaadhibu milele yote? Jibu ni dhambi zetu zinabeba hukumu ya milele kwa sababu ni dhambi ambayo imetendwa kinyume na Mungu wa milele. Wakati mfalme Daudi alifanya dhambi ya uzinzi na uuwaji alianza, “Nimekutenda dhambi wewe peke yako, na kufanya maouvu mbele za macho yako……” (Zaburi 51:4). Daudi alikuwa amemtenda dhambi Bathiseba na Uria; Daudi anawezaje kusema kuwa amemtendea Mungu dhambi? Daudi alielewa kuwa dhambi zote si kinyume na Mungu. Mungu ni Mungu wa milele na asiye na mwisho. Kwa sababu hiii, dhambi zote kinyume naye zastahili hukumu ya milele. Sio mambo na urefu wa muda tufanyao dhambi, lakini tabia ya Mungu ambaye twamtendea dhambi.

Njia kuu ya kipinafsi ya imani kuwa kuna uangamizo ni dhana kwamba hatuwezi kuwa na furaha huko mbinguni ikiwa tulijua kwamba baadhi ya wapendwa wetu wanateseka katika mauti ya milele. Hata hivyo, tutakapofika mbinguni, hatutakuwa na kitu cho chote cha kulalamikia au kuhusunishwa. Ufunuo 21:4 yatuambia, “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” Ikiwa baadhi ya wenzi wetu hawako mbinguni, tutakubaliana asili mia 100 kuwa hastahili kuwa pale na kuwa wamehukumiwa kwa kataaa lao wenyewe kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wao (Yohana 3: 16; 14:6). Ni vigumu kuyaelewa haya, lakini hatutahusunishwa kwa kukuso kuwepo kwao. Tazamio letu liziwe ni namna gani tutasherekea mbinguni bila wendani wetu pale, lakini iwe ni namna gani tutaweza kuwaelekeza wendani wetu kwa imani iliyo katika Kristo ili waweze kuwa pale.

Jahannamu ndio sababu ya kimsingi ni kwa nini Mungu alimtuma Yesu Kristo kulipa deni ya dhambi zetu. Kifo cha Yesu hakikuwa na mwisho, kulipia dhambi zetu sizizo na mwiso ili tuwe tunailipia jahannamu milele (2 Wakorintho 5:21). Wakati tunaiweka imani yetu kwake, tumeokolewa, tumesamehewa, kutakasika, na kuhaidiwa mji wa mile huko mbinguni. Lakini kama tutakikataa kipaji ch Mungu cha uzima wa milele, tutakumbana na madhara yake mile kwa sababu ya uamuzi wetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maangamizo ni jambo la kibibilia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries