settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini niamini katika ufufuo wa kristo?

Jibu


Ni jambo linalofahamika vizuri sana kuwa hakika kwamba Yesu Kristo alikuwa alinyongwa hadharani katika Uyahudi, katika karne ya 1 Baada ya Yesu kuzaliwa, chini ya Pontio Pilato , kwa njia ya mateso, kwa amri ya Baraza ya Wayahudi. Maelezo ya kihistoria yasiyo ya Mkristo ya Flavius Josephus, Cornelius Tacitus, Lucian wa Samosata, Maimondes na hata Baraza la Wayahudi yanathibitisha ushahidi wa hawali wa Wakristo waelezea tukio hili muhimu ya kihistoria la kifo cha Yesu Kristo.

Kuhusu ufufuo wake, kuna mistari kadhaa ya ushahidi ambayo inatulazimisha kuuamini. Hayati waziri wa kimataifa Bwana Lionel Luckhoo (wa kitabu cha umaarufu cha matukio ya kimataifa jambo lisilo la kawaida mara 245 mfululizo wa tetezi zake za kuachilia huru watuhumiwa wa kesi za mauaji) kwa ufupi shauku Mkristo na kujiamini katika nguvu ya kesi kwa ufufuo wakati yeye aliandika, "Nimetumia zaidi ya miaka 42 kama mwanasheria wakili wa kesi katika mahakama kuu, huku nikionekana katika sehemu nyingi za dunia na bado ninaendelea katika taaluma ya uwakili. Nimekuwa na bahati ya kupata idadi ya mafanikio katika majaribio ya kuwa katika kile kikao cha Mahakama ya rufaa na mimi ninasema bila utata wowote kuwa ushahidi wa ufufuo wa Yesu Kristo ni kweli na wa kukubalika ambao hauachi na nafasi ya shaka."

Jamii ya kidunia yajibu kuhusu ushahidi huo kuwa ule hauna haja ya ahadi zao thabiti kulingana na mbinu ya mtazamo wa hoja. Kwa wale wasio na ufahaamu wa kawaida kuhusu; mbinu yay a vitu vinavyo onekana ni jitihada za binadamu kwa kueleza kila kitu katika suala la sababu za asili na sababu za asili tu. Kama madai ya tukio ya kihistoria yanahitilafiana na maelezo ya asili (kwa mfano, ufufuo wa kimiujiza), wasomi wa kidunia kwa ujumla hulichukulia swala kwa tashwishwi, mbali na ushahidi, bila kujali lazimisha nzuri litakalo kuwepo.

Kwa mtazamo wetu, kama vile utii kwa sababu ya asili bila kujali ushahidi halisi ushahidi mkubwa kinyume na sizo nzuri kwa upendeleo (na hivyo kutosha) uchunguzi wa ushahidi. Tunakubaliana na Daktari Wernher von Braun na wengine wengi ambao bado wanaamini kwamba kulazimisha falsafa maarufu ya maelekezo juu ya ushahidi unaozuia usawa. Au katika maneno ya Daktari von Braun, "Kwa kulazimishwa kuamini hitimisho moja tu ... utakiuka ule usawa wa sayansi yenyewe."

Baada ya kusema hayo, hebu sasa tuchunguza mistari kadhaa ya ushahidi ambao waungua mkono ufufuo.

Mstari wa kwanza wa Ushahidi wa ufufuo wa Kristo

Kwa kuanzia, tumeonyesha ukweli wa shuhuda za ushahidi. Watume Wakristo wa kwanza walitoa mamia ya ushahidi waliouona kwa macho, ambao baadhi yao walinakili kumbukumbu ya uzoefu wao wenyewe. Wengi wa mashahidi hawa kwa makusudi na uthabiti walivumilia mateso ya muda mrefu na kufa kuliko kukataa ushahidi wao. Ukweli huu washuhudia uaminifu wao, wakifutilia mbali uongo kwa upande wao. Kwa mujibu wa rekodi ya kihistoria (kitabu cha Matendo 4:1-17; Barua ya Pliny kwa Trajan wa kumi, 96, nakadhalika) Wakristo wengi wanaweza kukomesha mateso yao tu kwa kukana imani yao. Badala yake, inaonekana kwamba wengi wamechagua kuvumilia mateso na kutangaza ufufuo wa Kristo hadi kifo chao.

Kule kuuawa kwa ajili ya imani, sio jambo la kulazimisha. Haihalalishi imani sana kama inavyo mtibitishia muumini imani yake (kwa kuonyesha uaminifu wake katika njia inayoonekana). Kinachowafanya mashahidi wa kale wa Kikristo kuwa mashujaa ni kwamba walijua kamba kile walichokuwa wanakikiri ni kweli. Wao aidha walimwona Yesu Kristo akiwa hai na baada ya kifo chake au hawakumwona. Hii ni ajabu. Kama hayo yote ni uongo, kwa nini wengi kuuendeleza ingawa mazingira yao hayakuwa mazuri? Kwa nini wao wote huku wakijua kushikamana na uongo usio na faida katika hali ya mateso, kufungwa jela, mateso na kifo?

Mwezi wa tisa (Septemba) 11, 2001, watekaji nyara wa kujitolea muhanga wa mauaji bila shaka waliamini chenye walicho kikiri (kama inavyothibitishwa na nia yao ya kufa kwa ajili yake), lakini hawakuweza kujua kama ni kweli. Wao huweka imani yao katika mila walizozirithid kutoka kwa vizazi vingi. Kwa ulinganisho mwingine, mashujaa wa imani wa zamani wa Kikristo walikuwa kizazi cha kwanza. Aidha wao walikiona chenye walichokitangaza, au wao hawakukiona.

Miongoni mwa ushahidi tukufu uliokiriwa ni wa Mitume. Wao kwa pamoja walipitia mabadiliko yasiyo kataliwa kufuatia madai ya kuonekana kwa Kristo baada ya ufufuo. Mara tu baada ya kusulubiwa kwake, walijificha kwa sababu ya hofu ya kupoteza maisha yao. Kufuatia ufufuo huo waliingia mitaani, kwa ujasiri kutangaza ufufuo licha ya kuongezeka kwa mateso. Ni nini kinachangia mabadiliko yao makubwa na ya ghafla? Hakika hailikuwa faida ya kifedha. Mitume walitoa kila kitu walichokuwa nacho ili wahubiri ufufuo, ikiwa ni pamoja na maisha yao.

Mstari wa pili wa Ushahidi kwa ufufuo wa Kristo

Mstari wa pili wa ushahidi kuhusu kuoka kwa baadhi wasioamini, hasa Paulo na Yakobo. Paulo alikuwa mtekeleshaji wa mateso na vurugu ya kanisa la kwanza. Baada ya kile anachokieleza kuwa kukutana na Kristo aliye fufuka, Paulo alipitia ubadilisho wa haraka kutoka kutesa Kanisa na kuwa mmoja wa watetezi wake. Kama Wakristo wengi wa kwanza, Paulo alipitia mateso umaskini, mateso, kupigwa, kufungwa jela, na kunyongwa kwa ahadi yake imara kwa ufufuo wa Kristo.

Yakobo alikuwa na wasiwasi, ingawa si adui kama Paulo. Kule kukutana na Kristo kunao tuhumiwa baada ya kufufuka kulimgeusha na kuw muumini mwenye msimamo usiotingizika, na kuwa kiongozi wa kanisa la Yerusalemu. Bado tuna kile wasomi kwa ujumla hukubali kuwa mojapo wa nyaraka zake kwa kanisa la kwanza. Kama Paulo, Yakobo kwa hiari aliteswa hadi akafa kwa ajili ya ushahidi wake, ukweli ambao washuhudia uaminifu wa imani yake (angalia kitabu cha Matendo Ya Mitume na Josephus ' Mambo ya Kale ya Wayahudi XX, ix, 1).

Mstari wa Tatu na wa Nne wa Ushahidi kwa ufufuo wa Kristo

Mstari wa tatu na mstari wa nne wa ushahidi kuhusu tangazo la uadui la kaburi tupu na ukweli kwamba imani katika ufufuo alichukua mizizi katika Yerusalemu. Yesu alinyongwa hadharani na kuzikwa katika Yerusalemu. Ingekuwa jambo lisilowezekana kwa imani katika ufufuo wake kuchukua mzizi katika Yerusalemu wakati mwili wake ulikuwa bado katika kaburi ambapo Baraza kuu lingeweza kuufukua, na kuuweka mahali unaweza kuonekana na umma, na hivyo kufunua uongo. Badala yake, baraza kuu waliwatuhumia wafuasi wa Yesu kuwa waliuiba mwili wake, hii inaonekana ni jitihada katika kueleza kupotea kwa mwil wake (na kwa hivyo na kuacha kaburi tupu). Je, sisi tunaelezaje ukweli wa kaburi tupu? Hapa kuna maelezo matatu ya kawaida:

Kwanza, wanafunzi waliuiba mwili. Kama hii ndio kesi, wangejua ufufuo ulikuwa wa uongo. Basi wao hawangekuwa tayari kuteseka na kufa kwa ajili yake. (Angalia mstari wa kwanza wa ushahidi unao onyesha ukweli kuhusu mashahidi wa moja kwa moja.) Wote wanaodai mashahidi waliona matukio kwa macho yao, wangejua kwamba hawakumwona Kristo na hivyo wamstarina uongo. Kwa pamoja wengi wa wanaoshirikiana, hakika mtu angekiri kwamba, ikiwa si kwa kukomesha mateso yake mwenyewe basi angalau kukomesha mateso ya marafiki zake na familia. Kizazi cha kwanza cha Wakristo walifanyiwa ukatili, hasa kufuatia ule moto katika mji wa Roma katika miaka ya 64 Kabla Yesu azaliwe (moto ambayo Niro aliamrisha ali apanue makzi yake kwa ajili ya upanuzi wa nyumba yake, lakini yeye mwenye akawalaumiwa Wakristo wa Roma katika jitihada ya kujiondolea lawama yeye mwenyewe). Cornelius Tacitus kama mwanahistoria ya Kirumi alielezea katika kumbukumbu yake ya Roma (iliyochapishwa tu na kizazi baada ya moto):

"Niro akakazia Wakristo hatia na kuachilia mateso zaidi juu kile kikundi kilichochukiwa kuwa katili, kwa jina walilojulikana kwalo sana na watu ni Wakristo. Kristo, asili ya jina lao, walipata adhabu kubwa mno wakati wa utawala wa Tiberio kwa mikono ya mmoja wa maliwali, Pontio, mkatili mbaya zaidi, kwa muda alikoma kidogo, tena kukatokea maovu katika Uyahudi pekee, chanzo cha kwanza na ubaya, bali hata katika Roma, ambapo mambo yote maovu na ya aibu kutoka kila sehemu ya dunia yalipata kituo na kuwa maarufu. Vile vile, kukamatwa kwa mara ya kwanzakulifanyika kwa wote ambao walikiri, na kisha, juu ya habari zao, umati mkubwa wa watu ulipatikana na hatia, si eti ni kwa ajili ya uhalifu wa kuuchoma mji, kama chuki dhidi ya mwanadamu. Kejeli ya kila aina iltunikwa kwa vifo vyao. Kufunikwa kwa ngozi za wanyama, waliliwa na mbwa na kuuwawa, au walisulubiwa msalabani, au kuangamizwa kwa moto na kuteketezwa, ili watumike kama mwanga wa usiku, wakati mwanga wa mchana uliisha. "(Kumbukumbu, XV, 44)

Niro aliwateketeza Wakristo wakikwa hai ili watumike kama mwanga wa bustani. Hakika mtu angeweza kukiri ukweli chini ya tishio la maumivu kama hilo. Ukweli ni kwamba, ingawa, hatuna rekodi ya Mkristo yeyote wa awali aliyekaana imani ili akomeshe mateso yake. Badala yake, tuna kumbukumbu nyingi za baada ya ufufuo zamamia ya mashahidi walio ona kwa macho yao wakiwa tayari kuteseka na kufa kwa ajili yake.

Kama wanafunzi hakuiba mwili wa Yesu, ni namna gani tunawelezea kaburi tupu? Baadhi ya watu wamependekeza kwamba Kristo alijidai amekufa na baadaye alitoroka kutoka kaburini. Hili ni jambo la kusikitisha. Kwa mujibu wa shuhuda za ushahidi, Kristo alipigwa, aliteswa, na kukwaruzwa, na kupigwa. Alipata uharibifu wa ndani, akapoteza damu, kukosa hewa, na kuchomwa mkuki kwa moyo wake. Hakuna sababu nzuri ya kuamini kwamba Yesu Kristo (au mtu mwingine yeyote kwa sababu ya jambo hili) kuwa Yesu anaweza kuishi kwa tatizo kama hilo la bandia kwa kifo chake, kukaa kaburini kwa siku tatu mchana na usiku bila matibabu, chakula wala maji, kuondoa jiwe kubwa ambalo lilifunika kaburi yake, kuepuka bila kujulikana ( bila kuacha nyuma ya uchaguzi tone la damu ), kushawishi mamia ya mashahidi kwamba alifufuka kutoka wafu, na katika afya njema, na kisha kutoweka bila kuwaeleza. Dhana kama hiyo ni ya kukanganya.

Mstari wa tano wa Ushahidi kwa ufufuo wa Kristo

Hatimaye, mstari wa tano wa ushahidi maalumu wa wale walioshuhudia. Katika hadidhi simulizi zote kuu za ufufuo wanawake wemetunukiwa sifa kama mashahidi wa kwanza na wa msingi. Hii itakuwa uvumbuzi usio wa kawaida jinsi katika tamaduni za kale za Wayahudi na Warumi wanawake walidunishwa sana. Ushuhuda wao ulichukuliwa kuwa si wa maana na kutupiliwa mbali. Kutokana na ukweli huu, kuna uwezekano mkubwa kwamba wahusika wowote wa uongo katika karne ya 1 katika Yudea bila kuchagua wanawake kuwa mashahidi wao wa msingi. Wanafunzi wake wote wa kiume ambao walidai kumwona Yesu akiwa amefufuka, kama wote walikuwa wanadanganya na ufufuo ulikuwa wa kashfa, ni kwa nini wao waliupokea ushuhuda potovu usioweza kuaminika ambao wangeweza kupata?

Daktari William Lane Craig anaeleza, "Wakati unaelewa jukumu la wanawake katika jamii ya karne ya kwanza katika jamii ya Wayahudi, kilicho cha ajabu ni kwamba hii hadithi ya kaburi tupu lazima iwahusishe wanawake kuwa wa kwanza wenye walioigundua kaburi tupu. Wanawake waliwekwa kitika kiwango cha chini sana cha ngazi ya kijamii katika karne ya kwanza ya Wapalestina. Kuna medhali za kirabi ambayo inasema, 'Heri maneno ya Sheria yachomwe kwa moto badala ya kutolewa kwa wanawake ' na ' heri ni mtu yule ambaye watoto wake ni wa kiume, lakini ole wake mtu ambaye watoto wake ni kike.' Ushahidi wa wanawake alichukuliwa kuwa sio wa maan kiwango kwamba hawakuruhusiwa kutumika kama mashahidi wa kisheria katika mahakama ya Sheria ya Wayahudi. Katika mwanga wa hili, ni ajabu kwamba mashahidi wakuu wa kaburi tupu ni hawa wanawake ... kumbukumbu yoyote ile ya baadaye bila shaka ingehuzisha wanafunzi wa kiume kama ndio wa kugundua kaburi - Petro au Yohana, kwa mfano. Ukweli kwamba wanawake ndio mashahidi wa kwanza wa kaburi tupu kwa uwezekano mwingi inaelezwa kwa ukweli kwamba – kama huo au sio - kuwa wao ndio waligundua kaburi tupu! Hii inaonyesha kwamba waandishi wa Injili kumbukumbu kwa uaminifu walinakili kile kilichotokea, hata kama ilikuwa aibu. Hii yazungumza kinyume na historia ya mila hii badala ya hadhi yake ya hadithi." (Daktari William Lane Craig , alinukuliwa na Lee Strobel , Uchunguzi kihusu Kristo, Grand Rapids. Zondervan, 1998, p 293)

Kwa Ufupi

Mistari hii ya ushahidi: usafi unaodhihirishwa na mashahidi wa moja kwa moja (na katika kesi ya Mitume, kulazimisha, mabadiliko yasiyo elezeka), badiliko la ukweli liwezalo thibitishwa la maadui wakuu - na la wenye shaka liliwabadilisha mashujaa wa imani, ukweli wa kaburi tupu, kataa la adui kwa kaburi tupu, ukweli kwamba haya yote yalifanyika katika Yerusalemu, mahali ambapo imani katika ufufuo alianza na ilinawili, ushahidi wa wanawake, umuhimu wa ushahidi kama huo uliotolewa katikia mazingira ya kihistoria; yote haya kwa nguvu yanashuhudia historia ya ufufuo. Tunawahimiza wasomaji wetu kufikiri kwa umakini shuhuda hizi. Je, wao wanapendekeza nini wewe? Baada ya sisi wenyewe kuyatafakari, sisi kwa uthabiti tunathibitisha tamko la msomi Lionel:

"Ushahidi kwa ajili ya ufufuo wa Yesu Kristo ni wa kufutia mno na walazimisha kukubalika kwa ushahidi ambao kwamwe hauaji kabisa hakuna nafasi ya shaka."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini niamini katika ufufuo wa kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries