settings icon
share icon
Swali

Je! Imekubalika kurudi rudia kuomba jambo moja au twastahili kuuliza mara moja?

Jibu


Katika Luka 18:1-7, Yesu anatumia mfano kueleza umuimu wa kustahimili katika maombi. Anaambiana hadhiti ya mjane ambeye alikuja kwa hakimu asiye na haki kuitisha haki kwa masaibu yaliyomkumba. Kwa sababu ya kule kushinda kudumu katika maombi, hakimu akampatia haki yake. Hoja ya Yesu hapa ni kwamba ikiwa hakimu asiye wa haki anaitoa hukumu ya haki kwa mtu anayeshinda akiitisha, je! Itakuwaje zaidi kwa Mungu wetu anayetupenda- “wateule wake” (aya ya 7) kujibu maombo yetu ambayo twashinda kumuuliza? Mfano huu haufunzi, vile umechukuliwa vipaya, kwamba ikiwa tutaliombea jambo na tuliombee tena, Mungu hulazimika kutupa. Badala, Mungu ameahidi kulipa ubaya kwa ubaya yeye mwenyewe, kuwapatia sawa na makosa yao, kuwafanyia haki, na kuwakomboa kutoka kwa masaibu. Anayafanya haya kwa sababu ya haki, utakatifu wake, na chukizo lake kwa dhambi; katika kujibu maombi, anaichunga ahadi yake na kuonyesha uweza wake.

Yesu anautoa mfano mwingine wa maombi katika Luka 11: 5-12. Ulio sawa na mfano wa hakimu asiye haki, ujumbe wa Yesu katika ufahamu huu ni kwamba ikiwa mtu atajinyima ili awapatie marafiki walio na mahitaji, Mungu atatutimizia mahitaji yetu, kwa vile hakuna hitaji ambalo ni sumbuvu kwa Mungu. Hapa tena ahadi sio kwamba atapokea chochote tutakachoendelea kuuliza. Ahadi ya Mungu kwa watoto wake ni ahadi ya kutimiza mahitaji yetu na sio haja zetu. Na anajua mahitaji yetu vizuri kutuliko. Ahadi hizo hizo zimerudiwa katika Mathayo 7:7-11 na Luka 11:13 mahali ambapo “tuzo jema” limeelezwa zaidi kuwa Roho Mtakatifu.

Kurasa zote zinatutia moyo tuombe na tuendelee kuomba. Hakuna makosa yoyote kurudia rudia kumuuliza Mungu jambo fulani. Bora tu chenye unaombea kiko katika mapenzi yake (1 Yohana 5:14-15), endelea kuuliza hadi Mungu atimize hitaji lako au akuondolee haja za moyo wako. Wakati mwingine Mungu hutulazimisha kungoja jibu kwa mombi yetu ili atufunze uvumilivu na kustahimili. Wakati mwingine tunauliza jambo ambalo haliko kwa muda wa Mungu kutupatia katika maisha yetu. Wakati mwingine tunauliza jambo lisilo mapenzi yake Mungu kwetu, na anasema “la.” Maombi sio kuweka haja zetu kwa Mungu; ni Mungu kuweka mapenzi yake katika nyoyo zetu. Endelea kuomba, endelea kubisha, na endelea kutafuta hadi Mungu atimize mahitaji yetu au akuthibitishie kwamba mahitaji yako sio mapenzi yake kwako.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Imekubalika kurudi rudia kuomba jambo moja au twastahili kuuliza mara moja?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries