settings icon
share icon
Swali

Ni nini kurudi kwa Yesu mara ya pili?

Jibu


Kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili ni tumaini la wakristo kwamba Mungu ndiye anatawala juu ya vitu vyote, na ni mwaminifu kwa ahadi zake na unabii wa neno lake. Katika kukuja kwake mara ya kwanza, Yesu Kristo akaja ulimwenguni kama mototo katika zizi la ng’ombe katika Bethlehemu, vile ilikuwa imetabiliwa. Yesu alitimiza unabii mwingi wa Masia wakati wa kuzaliwa kwake, maisha yake, huduma yake na kifo chake na kufufuka kwake. Ingawa kuna baadhi ya unabii kuhusu Masia ambao Yesu hajatimiza. Kukuja mara ya pili kwa Kristo kutakuwa kurudi kwa Kristo kutakuwa kwa kutimiza unabii ule umepaki. Kukuja kwake mara ya kwanza, Yesu alikuwa mtumishi aliyetezeka. Katika kurudi mara ya pili, Yesu atakuwa mfalme mkuu. Katika kufika kwake mara ya kwanza, Yesu alifika kwa njia ya unyenyekivu. Katika kurudi kwake mara ya pili, Yesu atafika na jeshi kuu la mbinguni wakiwa upande wake.

Manabii wa Agano La Kale hawakuweka tofauti kabisa kati ya kukuja huko kuwili. Hii inaweza kuonekana katika Isaya 7:14; 9:6-9; Zekaria 14:4. Kwa minajili ya unabii unaonekana kuzungumzia watu wawili, wachanganusi wengi wa Kiyahudi wanaamini kwamba wote Masia wawili watatezeka na Masia washindi. Chenye walikosa kuelewa ni kwamba kuna Masia mmoja na atatimiza majukumu yote. Yesu anatimiza jukumu la mtumishi anayetezeka (Isaya 53) katika kukuja kwake mara ya kwanza. Yesu atatimiza jukumu la kuwaokoa Wasraeli na mfalme katika kukuja kwake mara ya pili. Zekaria 12:10 na Ufunuo Wa Yohana 1:7 zaelezea kukuja kwake mara ya pili, wanaangalia nyuma vile Yesu alichomwa mkuki. Israeli na dunia yote, wataomboleza kwa kutomkubali Masia wakati alikuja mara ya kwanza.

Baada ya Yesu kupaa mbinguni, malaika waliwatangazia mitume, “wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka wenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni” (Matendo Ya Mitume 1:11). Zekaria 14:4 inautambua, kurudi mara ya pili ni kama Mlima wa Misaituni. Mathayo 24:30, yasema, “Ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu.” Tito 2:13 yanena kurudi mara ya pili kama “mafunuo ya utukufu.”

Kurudi mara ya pili kumezungumziwa kwa ukubwa katika Ufunuo Wa Yohana 19:11-16 “Kisha nikaziona mbingu, na tazama, farasi mweupe, naye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini kurudi kwa Yesu mara ya pili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries