settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu kuavya mimba?

Jibu


Bibilia kamwe haijalizungumzia swala la kuavya mimba moja kwa moja. Ingawa, kuna mafundisho mengi katika maandiko ambayo yanaifanya kuwa wazi kuwa mtazamo wa Mungu kuhusu uavyaji wa mimba ni upi. Yeremia 1:5 yatuambia Mungu anatujua kabla atuumbe tumboni mwa mama zetu. Zaburi 139: 13-16 yasungumzia jukumu la Mungu katika uumbaji wetu na kutengezwa kwetu katika tumboni mwa mama zetu. Kutoka 21: 22-25 yaelezea hukumu hiyo hiyo- kifo kwa yoyote anayesababisha kifo cha mtoto aliye tumboni sawa na mtu mwuaji. Hii yaonyesha wazi wazi kuwa Mungu anaihesabu mimba kama mwanadamu ambaye ni mtu mzima. Kwa Mkristo uavyaji mimba si jambo la haki ya mwanamke kuchagua. Ni jambo la uhai na kifo cha mwanadamu ambaye ameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27; 9:6).

Kwa pingamizi la kwanza ambalo lainuka kinyume na kitendo cha Mkristo kuavya mimba ni “Itakuaje kwa kesi ya ubakaji/ kujamiana kwa maharimu?” vile itakavyo kuwa vipaya sana kuwa mja mzito kwa mjibu wa ubakaji/kujamiana kwa maharimu, ndivyo uuwaji wa mtoto jibu litakuwa. Makosa mawili hayawezi kuifanya iwe zuri. Mtoto ambaye ametokea kwa ajili ya kubakwa/kujamiana kwa maharimu atapeana kwa uasili kwa familia ambayo kwa muda mrefu hawajaweza kupata mtoto, au mtoto atalelewa na mama yake. Pia, hakika mtoto huyo hana hatia, na asiadhibiwe kwa tendo la uovu la babaye.

Pingamizi la pili ambalo lainuka na mzimamo wa Kikristo kuhusu uavyaji mimba ni “itakuaje ikiwa maisha ya mama yako hatarini?” kwa kweli hili ni swali gumu kulijibu kwa hoja ya uavyaji mimba. Kwanza, tukumbuke kwamba katika hali hii sababu ambayo imemfanya aavye ni thuliuthi kumi ya asili mia moja ya uavyaji mimba ambao wafanywa ulimwenguni hii leo. Zaidi ya hayo wanawake wamekuwa na uavyaji mimba kuwa hali inayofaa kuliko wamama ambao wanavya mimba ili waokoe maisha yao. Pili, hebu tukumbuke Mungu ni Mungu wa miujiza. Anaweza yaweka/yaokoa maisha ya mama na mtoto mbali na juhudi zote za matibabu kuwa kunyume. Hatimaye, ingawa hili swali linaweza amuliwa kati ya mume na mke na Mungu. Wanandoa wowote ambao wanakumbana nah ii hali ngumu sana lazima wamuombe mungu hemima (Yakobo 1:5), ili wabaini ni nini lini Mungu angeliwataka wafanye.

Zaidi ya asili mia 95 ya uavyaji mimba ambao wafanywa hii leo wahuzisha wanawake ambao hawataki kuwa na mtoto. Chini ya asili mia 5 ya uavyaji mimba ni kwa sababu ya ubakaji, kujamiana kwa maharimu, au afya ya mama kuwa hatarini. Hata katika asili mia 5 hii ya hail ambayo ni ngumu kutokea, uavyaji mimba usiwe jambo la kwanza. Maisha ya mwanadamu katika tumbo ni ya dhamani kwa juhudi zote mtoto awezeshwe kuzaliwa.

Kwa wale ambao wameshiriki uavyaji mimba, kumbuka dhambi ya uavyaji mimba si kubwa ambayo haitasamehewa kuliko dhambi zingine. Kupitia kwa imani katika Kristo, dhambi zote zinaweza samehewa (Yohana 3:16; Warumi 8:1; Wakolosai 1:14). Mwanamke ambaye amewai avya mimba, mwanamume ambaye amewai unga mkono uavyaji mimba, au daktari yeyote ambaye amazaidia kuavya mimba wakati mmoja- wote wanaeza kusamehewa kwa imani katika Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu kuavya mimba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries