settings icon
share icon

Kitabu cha Yuda

Mwandishi: Yuda 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha Yuda kama Yuda, ndugu wa Yakobo. Hii huenda inarejelea Yuda ndugu wa kambo wa Yesu, kama Yesu pia alikuwa na ndugu wa kambo aitwaye Yakobo (Mathayo 13:55). Yuda huenda hajitambulishi mwenyewe kama ndugu wa Yesu kwa unyenyekevu na heshima kwa ajili ya Kristo.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Yuda kinahusiana kwa karibu na kitabu cha 2 Petro. Tarehe ya uandishi kwa Yuda inategemea kama Yuda alitumika yaliyomo katika 2 Petro, au Petro alitumia yaliyomo katika Yuda wakati wa kuandika 2 Petro. Kitabu cha Yuda kiliandikwa pengine kati ya 60 na 80 BK.

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Yuda ni kitabu muhimu kwetu siku hizi kwa sababu kiliandikwa kwa nyakati za mwisho, kwa mwisho wa nyakati za kanisa. Enzi za kanisa zilianza katika siku ya Pentekoste. Yuda ndicho tu kitabu kilichotolewa kwa uasi mkubwa. Yuda anaandika kwamba matendo maovu ni ushahidi wa uasi. Yeye anatuonya tushindanie imani, kwa kuwa kuna magugu kati ya ngano. Manabii wa uongo wako kanisani na Watakatifu wako hatarini. Yuda ni kitabu kidogo lakini muhimu kinachostahili kutafitiwa, kilichoandikwa kwa Wakristo wa siku hizi.

Mistari muhimu: Yuda 3: "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."

Yuda 17-19:. "Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. "

Yuda 24-25: "Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina. "

Muhtasari kwa kifupi: Kulingana na mstari wa 3, Yuda alitamani kuandika kuhusu wokovu wetu, Hata hivyo, alibadilisha mada kushughulikia kushindania imani. Imani hii inajimuisha mwili kamilifu wa mafundisho ya Kikristo yaliyofundishwa na Kristo, na baadaye kupitishwa kwa mitume. Baada ya Yuda kuonya kuhusu walimu wa uongo (mistari 4-16) anatushauri jinsi tunaweza kufanikiwa katika vita vya kiroho (mistari 20-21). Hapa ni hekima ambayo tanaweza kufanya vizuri kuikubali na kuambatana nayo tunapoendelea katika siku hizi za nyakati za mwisho.

Mashirikisho: Kitabu cha Yuda kimejazwa na marejeleo kwa Agano la Kale, ikiwa ni pamoja na Kutoka, (mst 5.) uasi wa Shetani (mst 6.); Sodoma na Gomora (mst 7.); kifo cha Musa (mst 9.); Kaini (mst 11.); Balaamu (mst 11.); Kora (mst 11.); Henoko (mst 14,15.); na Adamu (mst. 14). Matumizi ya Yuda ya maelezo ya kihistoria yanayofahamika vizuri ya Sodoma na Gomora, Kaini, Balaamu, na Kora yaliwakumbusha Wakristo Wayahudi umuhimu wa imani ya kweli na utiifu.

Vitendo Tekelezi: Tunaishi katika wakati wa kipekee katika historia na kitabu hiki kidogo kinaweza kusaidia kutuandaa kwa ajili ya changamoto zizioonekana kuishi katika nyakati za mwisho. Wakristo wa siku hizi lazima wawe waangalifu kwa mafundisho ya uongo ambayo yanaweza kwa urahisi kutudanganya ikiwa hatuna ufahamu mzuri wa Neno. Tunahitaji kujua Injili-kwa kuilinda na kuitetea - na kukubali Ubwana wa Kristo, ambao inathibitishwa kwa mabadiliko ya maisha. Imani halisi/kweli huonyesha tabia ya kikristo. Maisha yetu katika Kristo lazima yaashirie ufahamu wa mioyo yetu halisi ambao unakaa juu ya mamlaka ya Mwenyezi Muumba na Baba ambaye anaweka imani katika matendo. Tunahitaji kuwa na uhusiano wa kibinafsi naye, basi ndipo tutakapojua sauti yake vizuri kwamba hatuwezi kufuata nyingine.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Yuda
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries