settings icon
share icon

Kitabu cha Nehemia

Mwandishi: Kitabu cha Nehemia hakimtaji bayana mtunzi wake, lakini tamaduni za Wayahudi na Wakristo zinamtambua Ezra kama mwandishi. Hili lina msingi kwa ukweli kwamba vitabu vya Ezra na Nehemia kiasili vilikuwa kitabu kimoja.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Nehemia huenda kiliandikwa kati ya 445 na 420 kk

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Nehemia, mojawapo ya vitabu vya historia vya Biblia, kinaendeleza hadithi ya kurudi kwa Israeli kutoka kwa utumwa wa Babeli na kujengwa upya kwa hekalu katika Yerusalemu.

Mistari muhimu: Nehemia 1: 3, "Wakaniambia, watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.. '"

Nehemia 1:11, "Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. . "

Nehemia 6:. 15-16, "Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tama sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu. "

Muhtasari kwa kifupi: Nehemia alikuwa muiberania katika Uajemi wakati ujumbe ulimfikia kuwa Hekalu lililoko Yerusalemu linajengwa upya. Alitamaushwa huku akijua kuwa hakukuwa na ukuta wa kulinda mji. Nehemia alimwomba Mungu amutumie kuuokoa mji. Mungu alijibu maombi yake kwa kuunyenyekeza moyo wa mfalme wa Uajemi, Artaxerxes, ambaye alitoa si tu baraka zake, bali pia vifaa vitakavyotumiwa katika mradi huo. Nehemia alipewa idhini na mfalme kurudi Yerusalemu, ambapo alifanywa gavana.

Licha ya upinzani na shutuma ukuta ulijengwa na maadui kunyamazishwa. Watu kwa kutiwa moyo na Nehemia, walitoa fungu la kumi la fedha nyingi, vifaa na wafanyakazi ili kukamilisha ukuta kwa takribani siku 52, licha ya upinzani mkubwa sana. Hii nguvu ya umoja inadumu muda mfupi, hata hivyo, kwa sababu Yerusalemu inaanguka katika uasi wakati Nehemia anaondoka kwa muda. Baada ya miaka 12 alirudi na kupata kuta ziko imara lakini watu ni wadhaifu. Alianza kazi ya kuwafundisha watu maadili na hakusema maneno waziwazi. "Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao" (13:25). Yeye alikuza upya ibada ya kweli kwa njia ya maombi na kwa kuhimiza watu kwa uamsho kwa kusoma na kulishika Neno la Mungu.

Isharas: Nehemia alikuwa mtu wa maombi na aliomba akijawa na hisia kwa watu wake (Nehemia 1).Sala yake yenye raghba ya kuombea watu wa Mungu inaashiria mwombezi wetu mkuu, Yesu Kristo, ambaye aliomba kwa hamasa kwa watu wake katika sala yake kuu ya kikuhani katika Yohana 17. Nehemia na Yesu wote walikuwa na upendo dhati kwa watu wa Mungu ambao waliumwaga katika maombi kwa Mungu, wakiwaombea mbele ya kiti cha enzi.

Vitendo Tekelezi: Nehemia aliwaongoza Waisraeli katika heshima na upendo kwa neno la andiko. Nehemia, kwa sababu ya upendo wake kwa Mungu na nia yake ya kuona Mungu ameheshimiwa na kutukuzwa, uliwaongoza Waisraeli kwa imani na utiifu ambao Mungu alitamani kwao kwa muda mrefu. Kwa njia hiyo hiyo, Wakristo wanapaswa kupenda na kuheshimu sana ukweli wa maandiko, wahifadhi katika mioyo, wayatafakari mchana na usiku, na kurejea kwao kwa ajili ya kutimiziwa kila haja ya kiroho. 2 Timotheo 3:16 inatuambia "Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. "Ikiwa tunatarajia kuwa na uzoefu wa urudishaji wa kiroho wa waisraeli (Nehemia 8: 1-8), lazima tuanze na Neno la Mungu.

Kila mmoja wetu anapaswa kuwa na huruma ya kweli kwa watu wengine ambao wana madhara ya kiroho au kimwili. Kuwa na huruma, kisha, usifanye chochote kusaidia, hauna msingi wa kibibilia. Wakati mwingine tunaweza kuweka kando starehe zetu ili kuwahudumia wengine vizuri. Lazima tuamini kabisa katika sababu kabla ya kutumia wakati wetu au fedha kwake kwa moyo mzuri. Tunapomruhusu Mungu kuhudumu kupitia kwetu, hata makafiri watajua ni kazi ya Mungu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Nehemia
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries