settings icon
share icon
Swali

Kipawa cha kuongea na ndimi ni nini?

Jibu


Mara ya kwanza kuongea kwa ndimi kulitendeka katika siku ya pentekote katika matendo ya mitume 2:1-4. mitume wakatoka nje kutangaza injili kwa makutano huku wakiongea kwa ndimi zao wenyewe, ‘tunawasikia wakitangaza maajabu ya Mungu kwa lugha zetu wenyewe!” (matendo ya mitume 2:11). Neno la kigiriki llililotafsiriwa “ndimi” lina maana sawa na “ lugha.” Kwa hivyo kuongea na ndimi ni kuhudumu na lugha usiyoijua kwa mtu aijuaye. Katika wakorintho wa kwanza mlango wa 12-14, mahali Paulo anapozungumzia vipawa vya miujiza anasema kuwa, “ sasa ndugu zangu, nikija kwenu nikiongea kwa lugha ngeni itawafaidisha ninyi vipi, Isipokuwa nikiwaletea neno la ufunuo aumaarifa au unabii au neno la mafundisho?” (wakorintho wa kwanza14:6). Kulengana na Mtume Paulo na ndimi zilizozungumziwa katika matendo ya mitume kusema kwa lugha ngeni ni faida kwa mwenye kusikia ujumbe wa Mungu katika lugha yake binafsi lakini haina maana kwa mwingine awaye yule isipokuwa itafsiriwe.

Mtu mwenye kipawa cha kutafsiri lugha (wakorintho wa kwanza12:30) aweza kufahamu kinachozungumziwa katika lugha ngeni hata akiwa lugha yenyewe haifahamu. Na kwa njia hii mtu huyu anaweza kuitafsiri hotuba hiyo ili kila mmoja akafahamu yasemwayo katika lugha hiyo ngeni. “ kwa sababu hii basi kila anenaye kwa lugha aombe iliaweze kuyatafsiri ayasemayo” wakorintho wa kwanza 14:13). Paulo amalizia hivi juu ya lugha zisizotafsiriwa, “ lakini katika kanisa ingefaa zaidi niongee maneno matano tu ya kufundisha kuliko maneno elfu kumi katika lugha ngeni” (wakorintho wa kwanza 14:19).

Je, kipawa cha ndimi ni cha wakati wa sasa? Wakorintho wa kwanza 13:8 inataja kukoma kwa kipawa cha ndimi ijapokuwa inaonyesha kinachofuata baadaye ni kile kisichokoma katika wakorintho wa kwanza 13:10. wegine hutumia Isaya 28:11 na Yoeli 2:28-29 kama ushahidi wakuwa kuzungumza kwa lugha ngeni ni ishara ya hukumu ya Mungu ijayo. Wakorintho wa kwanza yazungumzia ndimi kama, “ishara kwa wasioamini.” Maandiko hayatuelezei kama wakati kuzungumza kwa lugha ngeni kumekoma.

Pia kama kipawa hiki kingekua hai kwa wakati huu kanisani kingefanyika sawa na maandiko. Ingekuwa ni lugha inayoeleweka (wakorintho wa kwanza 14:10). Ingekuwa ni kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe wa Mungu kwa Mtu wa lugha nyingine( matendo ya mitume 2::6-12). Ingekuwa ikilengana na amri Mungu aliyotoa kupitia Mtume Paulo, “ mtu yeyote akizungumza kwa ndimi - wawili au hata watatu – lazima wazungumze mmoja baada ya mwingine na mmoja mlazima atafsiri. Kama hakuna wa kutafsiri, mnanaji anyamaze kanisani na ajizungumzie tu peke yake na Mungu” ( wakorintho wa kwanza 14:27-28). Ingekuwa ikitii pia wakorintho wa kwanza 14:33, “ kwa kuwa Mungu si mwanzilishi wa machafuko, bali amani kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.”

Mungu anaweza kumpa mtu kipawa cha kuongea kwa ndimi ili kumwezesha kuwasiliana na mtu wa lugha nyingine. Roho mtakatifu ndiye mwamuzi katika mambo ya vipawa hivi. ( wakorintho wa kwanza 12:11). Fikiria kungekuwa na wamishonari wangapi wazuri kama hawangehitajika kusomea lugha za watu bali wangekuwa na kipwa hiki! Ndimi hazipatikani siku hizi kama ilivyofanyika katika agano jipya. Wengi wa waaminio wanaosema wanazungumza kwa ndimi hawafanyi sawa na maandiko. Kwa sababu hizi tunaweza kusema kipawa cha ndimi kimekoma ama ni nadra katika kanisa la sasa.

Wale waaminio kipawa cha ndimi kama “ lugha ya maombi” kwa ajili ya kukamilishwa kwao hupata maoni haya kutoka wakorintho wa kwanza 14:4 na 14:28, “ yule anayeongea kwa lugha hujikamilisha mwenyewe lakini anayetabiri hulikamilisha kanisa.” Katika mlango wote wa 14 Paulo asisitiza ndimi zitafsiriwe tazama 14:5-12. kile Paulo anachozungumzia katika aya ya 4 ni kwamba unapozungumza kwa ndimi bila kutafsiriwa, unajikamilisha mwenyewe huku ukijifanya wewe kuwa kiroho zaidi kuliko wengine. Ukizungumza kwa ndimi na ikitafsiriwa, unawakamilisha wote.” Hakuna mahali katika agano jipya, Biblia inapotoa maagizo watu waombe kwa ndimi. wakorintho wa kwanza 12:29-30 inaeleza waziwazi kuwa si kila mtu anaweza kuwa na kipawa cha kuzungumza kwa ndimi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kipawa cha kuongea na ndimi ni nini? Je, kipawa cha ndimi ni cha wakati wa sasa? Je, pia ni nini kuomba kwa ndimi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries