settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini viongozi wengi wa kiinjili wa kikristo wapatikana katika kashfa?

Jibu


Kwanza, ni muhimu kusema kwamba "wingi" sio Tabia sahihi. Inaweza kuonekana kwamba viongozi wengi wa kiinjili wa kikristo wanapatikana katika kashfa, lakini hii ni kutokana na kiasi kikubwa cha mawazo kashfa kama hii inapewa. Kuna maelfu ya viongozi Kikristo wa kiinjili, wachungaji, maprofesa, wamisionari, waandishi, na wainjilisti ambao hawajawahi shiriki katika kitu chochote cha "kashfa." Idadi kubwa ya viongozi wa kikristo wa kiinjili ni wanaume na wanawake ambao humpendo Mungu, ni waaminifu kwa wenzi wao na familia, na kushughulikia shughuli zao kwa uaminifu na uadilifu mkubwa. Kuanguka kwa wachache hakupaswi kutumika kushambulia tabia ya wote.

Kwa hayo kusemwa, bado kuna tatizo kwamba kashfa hutokea wakati mwingine miongoni mwa wale waliodai kuwa Wakristo wa kiinjili. Viongozi maarufu wa Kikristo wamewekwa wazi kwa ajili ya uzinzi au kushiriki katika ukahaba. Baadhi ya Wakristo wa kiinjili wamekuwa na hatia ya udanganyifu wa kodi na utumiaji mpaya wa fedha. Kwa nini haya hutokea? Kuna maelezo angalau matatu ya msingi: 1) Baadhi ya wale waliodai kuwa Wakristo wa kiinjili ni walaghai wasioamini, 2) baadhi ya viongozi wa kikristo wa kiinjili huruhusu cheo chao kusababisha kiburi, na 3) Shetani na mapepo yake hushambulia na kuwachanganya wale walio katika uongozi wa kikristo kwa sababu wanajua kwamba kashfa inayo mshirikisha kiongozi inaweza kuwa na matokeo makubwa, juu ya Wakristo na wasio Wakristo.

1) Baadhi ya "Wakristo wa kiinjili" ambao wanapatikana katika kashfa ni walaghai wenye hawajakombolewa na manabii wa uongo. Yesu alionya," Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali ... Kwa hiyo kwa matunda yao mtawatambua" (Mathayo 7:15-20). Manabii wa uongo ni wanaume na wanawake hujifanya kuwa watu wanaomcha Mungu, na kuonekana kuwa viongozi imara wa kiinjili. Hata hivyo, "matunda" (kashfa) yao hatimaye inawaonyesha hadharani kuwa kinyume cha kile wanakidai kuwa. Katika hili, wao hufuata mfano wa Shetani, "Wala si ajabu, maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi neon kubwa watumishi wa haki, ambao wmisho wao utakuwa sawasawa na kazi" (2 Wakorintho 11:14-15).

2) Biblia inaeleza wazi kwamba "kiburi hutangulia uangamivu, na roho yenye kutakabari hutnagulia maanguko" (Mithali 16:18). Yakobo 4:6 inatukumbusha kwamba "Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu." Biblia mara kwa mara inatuonya dhidi ya kiburi. Viongozi wengi wa Kikristo huanza huduma katika roho ya unyenyekevu na kumtegemea Mungu, lakini huduma inapo endelea na kukua vyema, wao hujaribiwa na kuchukua baadhi ya utukufu huu kuwa wao wenyewe. Baadhi ya viongozi wa injili ya kikristo, wakati wao hutoa huduma kwa Mungu, kwa kweli wao hujaribu kusimamia na kujenga huduma kwa nguvu zao wenyewe na hekima. Aina hii ya kiburi inaongoza kwa kuanguka. Mungu, kwa njia ya nabii Hosea, alionya, "Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau mimi" (Hosea 13:6).

3) Shetani anajua kwamba kwa kuchochea kashfa kwa kiongozi wa injili ya kikristo, anaweza kuwa na athari ya nguvu. Tu kama uasherati wavMfalme Daudi na Bathsheba na mpango wa mauaji ya Uria ulisababisha uharibifu mkubwa katika familia ya Daudi na taifa zima la Israeli, na hivyo wingi wa kanisa au huduma zimekuwa zikiharibiwa au kuangamizwa kwa maadili mabaya ya kiongozi wake. Wakristo wengi wamekuwa na imani yao kuwa hafifu kwa sababu ya kuona kiongozi ameanguka. Mashirika yasiyo ya Wakristo hutumia kushindwa kwa viongozi wa "Wakristo" kama sababu ya kukataa Ukristo. Shetani na mapepo yake wanajua hili, na kwa hiyo hulenga moja kwa moja mashambulizi yao dhidi ya wale wako katika majukumu ya uongozi. Biblia inatuonya sisi wote, "Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kam simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze"(1 Petro 5:8).

Je tunastahili kujibu vipi wakati kiongozi wa kiinjili ya kikristo anatuhumiwa au kupatikana katika kashfa? 1) usisikilize au kukubali shutuma yoyote isiyo na msingi wowote (Mithali 18:8, 17; 1 Timotheo 5:19). 2) kuchukua hatua sahihi Biblia kukemea wale ambao dhambi ( Mathayo 18:15-17, 1 Timotheo 5:20). Kama dhambi imethibitika na ni mbaya, kuondolewa kabisa kutoka kwa uongozi wa huduma unapaswa kutekelezwa (1 Timotheo 3:1-13). 3) Basi wasamehe walio dhambini (Waefeso 4:32, Wakolosai 3:13), na wakati toba imethibitika, warejeshe wao kwa ushirika (Wagalatia 6:1; 1 Petro 4:8) lakini si kwa uongozi. 4) Kuwa waaminifu katika kuomba kwa ajili ya viongozi wetu. Kujua matatizo wanayopitia na, majaribu yao ya matezo, na dhiki ambayo ni lazima waivumilie, ni lazima tuombee viongozi wetu, kumuomba Mungu awaimarishe, awalinde, na kuwatia moyo. 5) muhimu zaidi, chukua mwanguko wa kiongozi wa injili ya kikristo kama mawaidha kwa kuweka imani yako ya mwisho katika Mungu na Mungu peke yake. Mungu kamwe hashindwi, kamwe hatendi dhambi, na kamwe haneni uongo. "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake" (Isaya 6:3).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini viongozi wengi wa kiinjili wa kikristo wapatikana katika kashfa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries