settings icon
share icon
Swali

Nitajuaje kama kitu fulani ni dhambi?

Jibu


Kuna mambo mawili yanayohusika na swali hili, mambo ambayo Bibilia hasa yayataja na kuyanena kuwa dhambi na yale ambayo Bibilia haiyataji moja kwa moja. Uratiba wa kibibilia wa dhambi tofauti tofauti ni pamoja na Methali 6:16-19, Wagalatia 5:19-21, na 1 Wakorintho 6:9-10. Hakutakuwa na shaka yoyote kuwa kurasa hizi zawazilisha kazi zote kuwa za dhambi, vitu ambavyo Mungu haviithinishi ni; Uwaji, uzinzi, uongo, wizi na kadhalika- hakuna shaka yoyote kuwa Bibilia yawazilisha mambo hayo kama dhambi. Mambo magumu zaidi ni kutambua ni jambo lipi ovu katika zile sehemu ambazo Bibilia haizitaji moja kwa moja. Bibili haifuniki baadhi ya masomo mengine, tuko na misimamo ya kijumla katika neno lake kutuongoza.

Kwanza, wakati hakuna nukuu ya maandiko, ni vizuri kuuliza sio kama kitu fulani ni makosa, lakini, kama ni kizuri. Bibilia husema, kwa mfano, hivi “yafaa tutumie kila nafasi tupatayo” (Wakolosai 4:5). Siku zetu ulimwenguni ni fupi na za dhamana ukilinganisha na milele hatupaswi kuharibu wakati na vitu vya uchoyo, ila tutumie “kile pekee kina manufaa katika kujenga wengine kwa mahitaji yao”(Waefeso 4:29).

Jaribio zuri ni lile linaloamua ikiwa tunaweza kwa kweli, kwa fikira safi, kumuuliza Mungu atubariki na kutumia kazi hiyo kwa lengo lake zuri. “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” (1 Wakorintho 10:31). Ikiwa hakuna nafasi ya shaka kama kwamba inamfurahisha Mungu, ni vizuri kuachana nayo. “Kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi” (Warumi 14:23). Tunastahili kukumbuka kwamba miili yetu, hata nafsi zetu, zote zimekombolewa na zote ni za Mungu. “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye dhani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:19-20). Ukweli mkuu lazima uwe na dira kuu ya yote tufanyayo na kwenye tunaenda.

Kwa kuongezea, lazima tutathmini matendo yetu kuhusiana na Mungu, na pia kuhusiana na madhara yake katika jamii zetu, kwa marafiki zetu, na watu wengine kwa ujumla. Hata kama kitu fulani hasa kisituchukize kibinafsi, kinaweza kuleta madhara mabaya kwa mtu mwingine hiyo ni dhambi. “Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa…..Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe” (Warumi 14:21; 15:1).

Mwisho, kumbuka kwamba Yesu Kristo ni Bwana na mwokozi wetu na hakuna kitu kingine kinaweza ruhusiwa kuchukua nafasi juu ya upatano wetu na mapenzi yake. Hamna mazoea au makusudio yanaweza ruhusiwa kuwa na mwongozo usiyostahili katika maisha yetu; ni Kristo pekee ako na hayo mamlaka. “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote” (1 Wakorintho 6:12). “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye” (Wakolosai 3:17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nitajuaje kama kitu fulani ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries