settings icon
share icon
Swali

Fasili ya dhambi ndio gani?

Jibu


Dhambi imeelezewa katika maandiko kuwa kuasi sheria za Mungu (1 Yohana 3:4) na kuasi kinyume cha Mungu (Kumbukumbu La Torati 9:7; Yoshua 1:18). Dhambi ilianzishwa na Ibilisi, pengine malaika aliyekuwa mzuri sana na mwenye nguvu kati ya malaika wote. Sio kulingana na mkudhata wa cheo chake, alitamani sana kuwa kuwa na mamlaka kuliko Mungu, na hapo ndipo alianguka, ukawa ndio mwanzo wa dhambi (Isaya 14:12-15). Akapatiwa jina tena na kuitwa Shetani, akaleta dhambi kwa uzao wa mwanadamu katika bustani mwa Edeni, mahali ampapo aliwajaribu Adamu na Hawa kwa ulaghai ule uel, “mtakuwa kama Mungu.” Mwanzo 3 inaelezea kuasi kwa Adamu na Hawa kunyume na Mungu na sheria zake. Tangu wakati huo, dhambi imekuwa ikipitishwa kwa vizazi vyote vya mwanadamu, na sisi kama uzao wa Adamu tumerithi dhambi kutoka kwake. Warumi 5:12 yatuambia kwamba kupitia Adamu dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa hivyo kifo kilipitishwa kwa watu wote kwa sababu “Mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23)

Kupitia kwa Adamu urithi wa dhambi uliingia katika kizazi cha mwanadamu, na mwanadamu akawa mwenye dhambi kihali. Wakati Adamu alisini, utu wake wa ndani ulibadilishwa kwa dhambi ya kuasi, na kumleta katika kifo cha kiroho na upotovu ambao utapitishwa kwa wale ambao walikuja nyuma yake. Sisi ni wenye dhambi, sio kwa sababu tunatenda dhambi, bali tunasini kwa sababu sisi ni wenye dhambi. Na huu upotovu uliopitishwa unaitwa, dhambi iliorithiwa. Vile tunavyo rithi tabia zinazoonekana kwa nche kutoka kwa wazazi wetu, vilevile tulirithi hali yetu ya dhambi kutoka kwa Adamu. Mfalme Daudi alisikitikia hali hii ya mwanadamu kuanguka katika Zaburi 51:5: “Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Maana yangu alinuchukua mimba hatiani.”

Aina nyingine ya dhambi inaitwa dhambi ya kuambukizwa. Inatumika katika mahali pa fedha na sheria, neno la Kiyunani ambalo limefasirwa “singizia” lamaanisha “ kuchukua kitu kinachomhusu mtu mwingine, na kukiazima kwa mwingine.” Kabla ya sheria ya Musa kupeanwa, dhambi haikusingiziwa kwa mwanadamu, ingawa wanadamu walikuwa wenye dhambi kwa sababu ya ile dhambi ya kurithi. Baada ya sheria kupeanwa, dhambi iliyotendwa ambayo ilikuwa kinyume na sheria waliwajibika (Warumi 5:13). Hata kabla ya sheria kutumika, adhabu ya dhambi (kifo) iliendelea kutawala (Warumi 5:14). Wanadamu wote, toka Adamu, hadi Musa wote waliwekewa kifo sio kwa sababu ya matendo yao ya dhambi kinyume na sheria ya Musa (ambayo hakuwa nayo), bali kwa sababu ya ule urithi wa hali ya dhambi. Baada ya Musa, wanadamu walitawaliwa na kifo kwa sababu ya ile dhambi ya urithi kutoka kwa Adamu na ile dhambi ya kuasi sheria ya Mungu.

Mungu alitumia ule msimamo wa kusingizia ili anufaishe mwanadamu wakati aliipachika dhambi ya wakristo kwa Yesu Kristo, ambaye alilipa adhabu ya dhambi-kufa msalabani. Kuipachika dhambi yetu kwa Yesu, Mungu alimchukuliwa kuwa mwenye dhambi, ingawa hakuwa mwenye dhambi, na akamfanya afe kwa ajili ya dhambi za dunia yote (1 Yohan 2:2). Ni muimu kuelewa dhambi ilipachikwa kwake, lakini hakuirithi kutoka kwa Adamu. Alibeba hukumu ya dhambi, lakini hakuwa mwenye dhambi. Utakatifu wake na ukamilifu wake haukuguzwa na dhambi. Alifanywa kana kwamba alikuwa na makosa yote ambayo yalifanywa na uzao wa mwanadamu, ingawa hakuwa amefanya hata moja. Kwa ubadilisho, Mungu aliupachika utakatatifu wa Kristo kwa Wakristo na akasadikisha makosa yetu kwa utukufu wake, jinsi alivyokwisha sakidikisha makosa yetu juu ya Kristo (2 Wakorintho 5:21).

Aina ya tatu ya dhambi ni ile dhambi ya kibinafsi, ambayo inafanywa kila siku na kila mwanadamu. Kwa sababu tumerithi hali ya dhambi kutoka kwa Adamu, tunatenda dhambi ya kibinafsi, kwa kila kitu tukionekana kutojua ambazo ni uongo kwa uuaji. Wale ambao hawajaweka imani yao kwa Yesu Kristo lazima walipe gharama ya dhambi ya kibinafsi, vilevile ile ya kurithiwa na ile ya kusingiziwa. Hata hivyo Wakristo wamekwisha vukishwa kutoka kwa ile hukumu ya milele ya dhambi-jahannamu na kufa kiroho-lakini hata sasa tuko na uwezo wa kuzuia kutenda dhambi. Sasa tunaweza chagua ikiwa tutatenda dhambi au hatutatenda dhambi ya kibinafsi kwa sababu tuko na uwezo wa kuzuia dhambi kupitia kwa Roho mtakatifu ambaye anakaa ndani yetu, anatutakaza na kututhibitishia dhambi zetu wakati tunazitenda (Warumu 8:9-11). Tunapokiri dhambi zetu za kibinafsi kwa Mungu na kumuuliza msamaha, tumerejeshwa kwa ushirika kamilifu na umoja naye. “Tukiziungama dhambi zetu. Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9).

Wote mara tatu tumehukumiwa kwa sababu ya ile dhambi ya urithi, ile dhambi ya kusingizia, na ile dhambi ya kibinafsi. Hokumu pekee ya haki ya dhambi hii ni mauti (Warumi 6:23), sio kifo cha kawaida bali ni mauti ya milele (Ufunuo Wa Yohana 20:11-15). Kwa kushukuru, dhambi ya urithi, ya kusingizia, na dhambi ya kibinafsi zote zimesulubiwa kwa msalaba wa Yesu, na sasa kwa imani katika Yesu Kristo kama mwokozi “Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Fasili ya dhambi ndio gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries