settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu?

Jibu


Wakati hatuwezi kuwa na hakika kabisa kwa nini Yuda alimsaliti Yesu, baadhi ya mambo fulani ni halisi. Kwanza, ingawa Yuda alichaguliwa kuwa mmoja wa wale kumi na wawili (Yohana 6:64),ushahidi wote wa maandiko matakatifu unaashiria kwamba kamwe hakuamini kuwa Yesu ni Mungu. Yeye pengine hata hakushawizika kwamba Yesu alikuwa Masihi (kama Yuda alivyoelewa). Tofauti na wanafunzi wengine waliomwita Yesu "Bwana," Yuda kamwe hakutumia jina hili kwa Yesu na badala yake alimwita "Mwalimu," ambalo lilimtambua Yesu kama tu mwalimu. Wakati wanafunzi wengine mara kwa mara walifanya fani kubwa ya imani na uaminifu (Yohana 6:68; 11:16), Yuda kamwe hakufanya hivyo na alionekana kuwa kimya. Ukosefu huu wa imani katika Yesu ni msingi kwa masuala mengine yote yaliyoorodheshwa hapa chini. Ukweli sawa na huu unatangamana nasi. Kama tutashindwa kutambua Yesu kama Mungu mwenyewe, na kwa hiyo tu wa pekee ambaye anaweza kutoa msamaha kwa ajili ya dhambi zetu-na wokovu wa milele ambao huja na hilo- tutakuwa chini ya matatizo mengine mbalimbali ambayo yanatokana na mtazamo mbaya wa Mungu.

Pili, Yuda si tu alikosa imani katika Kristo, lakini pia alikuwa na uhusiano kidogo wa kibinafsi na Yesu au aliukosa. Wakati muhtasari wa injili unaorodhesha kumi na wawili, wameorodheshwa kwa mpangilio sawa na uwiano wao(Mathayo 10: 2-4; Marko 3: 16-19; Luka 6: 14-16). Mpangilio wa jumla umeaminika kuonyesha utangamano wa karibu wa uhusiano wao kibinafsi na Yesu.Licha ya tofauti, Petro na ndugu zake Yakobo na Yohana daima walioorodheshwa kwanza, ambayo ni sawa na mahusiano yao na Yesu. Yuda daima alitajwa mwisho, ambayo inaweza kuonyesha ukosefu wake wa uhusiano binafsi wa karibu na Kristo. Kwa kuongezea, kumbukumbu ya pekee ya mazungumzo kati ya Yesu na Yuda inahusisha Yuda kukemewa na Yesu baada ya usemi wake kwa Mariamu uliochochewa na tama yake(Yohana 12: 1-8), Yuda kukataliwa na usaliti wake (Mathayo 26:25), na usaliti wenyewe (Luka 22:48).

Tatu, Yuda alitawaliwa na tamaa kwa kiwango cha kusaliti uaminifu sit u wa Yesu, bali pia wanafunzi wenzake, kama tunavyoona katika Yohana 12: 5-6.Pengine Yuda angetamani kumfuata Yesu kwa sababu tu yeye aliona umati mkubwa uliomfuata na akaamini angeweza kufaika kutoka kwa makusanyo yaliyochukuliwa kwa ajili ya kikundi. Ukweli kwamba Yuda alikuwa msimamizi wa mfuko wa pesa kwa ajili ya kundi ingeonyesha haja yake katika fedha (John 13:29).

Kwa kuongezea, Yuda, kama watu wengi kwa wakati mmoja, aliamini Masihi alikuwa anaenda kuupindua utawala wa Roma na kuchukua nafasi ya utawala wa nguvu katika taifa la Israeli. Yuda angeweza kumfuata Yesu akiwa na matumaini ya kunufaika kutokana na muungano pamoja naye kama atakayekuwa mtawala mpya wa kisiasa. Bila shaka yeye alitarajia kuwa miongoni mwa tabaka la watawala baada ya mapinduzi. Kwa wakati wa usaliti Yuda, Yesu alikuwa ameweka wazi kwamba Alipanga kufa, si kuanza uasi dhidi ya Roma. Basi, Yuda anaweza kuwa alidhani-tu kama Mafarisayo walifanya-kwamba tangu hangepindua Warumi, Hapaswi kuwa Masihi wao walikuwa wanatarajia.

Kuna mistari michache ya Agano la Kale inayoashiria kwa usaliti, baadhi halisi zaidi kuliko mingine. Hapa ni mbili:

"Hata rafiki yangu wa karibu, ambaye nimemtegemea, yeye ambaye alishirikiana mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu" (Zaburi 41: 9, tazama utimilifu katika Mathayo 26:14, 48-49). Pia, "Nikawaambia,mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo,msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu. Kisha Bwana akaniambia,mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu hao.Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha ,nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya Bwana "(Zekaria 11: 12-13; angalia Mathayo 27: 3-5 kwa ajili ya kutimiza unabii wa Zekaria). Huu unabii wa Agano la Kale unaonyesha kuwa usaliti wa Yuda ulikuwa unajulikana kwa Mungu na kwamba ulikuwa umepangiwa kwa mamlaka yake kama njia ambayo Yesu atauwawa.

Lakini kama usaliti wa Yuda ulikuwa unajulikana kwa Mungu, je, Yuda alikuwa na uamuzi, na yeye anawajibika kwa upande wake katika usaliti? Ni vigumu kwa wengi kupatanisha dhana ya "mapenzi ya bure" (kama watu wengi wanaielewa ) kwa maarifa ya Mungu ya matukio ya baadaye, na hii ni kwa kiasi kikubwa kutokana na uzoefu wetu mdogo wa kwenda kwa wakati katika mtindo nyoofu. Kama tunaona Mungu kama amepitwa na wakati, tangu Aliumba kila kitu kabla ya "wakati" alianza, basi tunaweza kuelewa kwamba Mungu anaona kila wakati kama uliopo.Tuna uzoefu wa muda katika hali ya unyoofu-tunaona wakati kama mstari ulionyooka, na tunapita kutoka hatua moja hadi nyingine hatua kwa hatua, tukikumbuka zamani ambayo tumekwishapitia tayari, lakini hatuwezi kuona siku za baadaye tunazokaribia. Hata hivyo, Mungu, kuwa Muumba wa milele wa ujenzi wa muda, si "katika wakati" au kwenye kalenda ya matukio, lakini nje ya hiyo.Inaweza kusaidia kufikiri juu ya muda (kulingana na Mungu) kama mzunguko na Mungu akiwa katikati na hivyo sawa karibu na pointi zote.

Katika hali yoyote, Yuda alikuwa na uwezo kamili wa kufanya uamuzi- angalau hadi kufikia hatua ambapo "Shetani akamwingia" (Yohana 13:27)-na maarifa ya Mungu (Yohana 13:10, 18, 21) hakuna njia ambayo kwayo inapita kiwango cha kawaida kwa uwezo wa Yuda kufanya uamuzi . Badala yake,chenye Yuda angehagua hatimaye, Mungu aliona kama kwamba ilikuwa maono ya sasa, na Yesu aliweka wazi kwamba Yuda alikuwa na wajibu wa uamuzi wake na atawajibika kwa ajili yake. "Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti-moja anayekula pamoja nami" (Marko 14:18). Ona kwamba Yesu anasifia ushirika wa Yuda kama usaliti. Na kuhusu uwajibikaji kwa usaliti huu Yesu alisema, "Ole wake mtu yule ambaye atakayenisaliti! Ingekuwa bora kwa ajili yake kama yeye hangalizaliwa "(Marko 14:21). Shetani, pia, alikuwa na sehemu katika hili, kama tunavyoona katika Yohana 13: 26-27, na yeye, pia, atawajibika kwa matendo yake. Mungu kwa hekima yake alikuwa na uwezo, kama siku zote, kwa kuendesha hata uasi wa Shetani kwa faida ya mwanadamu. Shetani alisaidia katika kumtuma Yesu juu ya msalaba, na juu ya msalaba dhambi na mauti zilishindwa, na sasa utoaji wa Mungu wa wokovu unapatikana kwa njia huru kwa wale wote ambao wanampokea Yesu Kristo kama Mwokozi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries