settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu alikuwa mlaji mboga? Je, Mkristo anapaswa kuwa mla mboga?

Jibu


Yesu hakuwa mla mboga. Biblia imerekodi Yesu akila samaki (Luka 24: 42-43) na mwana-kondoo (Luka 22: 8-15). Yesu kimiujiza alilisha umati wa watu kwa samaki na mkate, jambo la ajabu kufanya kama yeye alikuwa mla mboga (Mathayo 14: 17-21). Katika maono kwa mtume Petro, Yesu alitangaza vyakula vyote kuwa safi, ikiwa ni pamoja na wanyama (Matendo 10: 10-15). Baada ya mafuriko katika wakati wa Nuhu, Mungu alitoa ruhusa ya binadamu kula nyama (Mwanzo 9: 2-3). Mungu hajawahi kubatilisha ruhusa hii.

Kwa hayo kusemwa, hakuna kitu kibaya na Mkristo kuwa mlaji wa mboga. Biblia haitushauri kula nyama. Hakuna kitu kibaya na kujizuia kula nyama. Chenye Biblia inasema ni kwamba tusilazimishe imani yetu katika kuhusu suala hili juu ya watu wengine au kuwahukumu kwa kile wanacho kila. Warumi 14: 2-3 inatuambia, "Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote, lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali."

Tena, Mungu alitoa ruhusa kwa binadamu kula nyama baada ya gharika (Mwanzo 9: 3). Katika sheria ya Agano la Kale, taifa la Israeli liliamurishwa lisile vyakula fulani (Mambo ya Walawi 11: 1-47), lakini hakukuwa na amri dhidi ya kula nyama. Yesu alitangaza vyakula vyote, ikiwa ni pamoja na kila aina ya nyama kuwa safi (Marko 7:19). Kama na kitu chochote, kila Mkristo anapaswa kuomba kwa ajili ya uongozi kwa kile Mungu angetaka yeye ale. Chochote tutakachoamua kula kimekubalika kwa Mungu kwa muda mrefu kama sisi humshukuru kwa kutoa (1 Wathesalonike 5:18). "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neon lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Wakorintho 10:31).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu alikuwa mlaji mboga? Je, Mkristo anapaswa kuwa mla mboga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries