settings icon
share icon
Swali

Yesu kristo ni nani?

Jibu


Yesu kristo ni nani? Watu wachache sana huuliza kama Yesu kristo alikuweko. Inakubalika kikamilifu kuwa Yesu alikuwa ni mtu aliyetembea juu ya ardhi huko Israeli karibu miaka 2000 iliyopita. Mjadala huzuka wakati wa utambuzi kamili wa Yesu kristo unapojadiliwa. Karibu kila dini kubwa humtaja Yesu kama nabii, mwalimu mwema au mcha mungu. Tatizo ni kuwa Biblia inatuambia ya kuwa Yesu alikuwa zaidi ya nabii, mwalimu mwema au mcha mungu.

C.S. Lewis, katika kitabu chake kiitwacho ukristo wa kijinsia tu aeleza yafuatayo: “nipo hapa kuzuia yeyote asemaye upumbavu kama wengine wao juu ya Yesu kristo. Wao husema, “Niko tayari kumkubali Yesu kama mwalimu wa uadilifu tu lakini sikubali madai yake ya kuwa ni Mungu”. Hili jambo moja lapo ambalo tusiliseme. Mtu aliyekuwa mwanadamu wa kawaida na kuweza kusema yale Yesu alisema bila shaka angekuwa mwendawazimu ama ibilisi wa kuzimu. Lazima ufanye uamuzi kamili. Uamue kama Yesu alikuwa mwana wa Mungu au mwendawazimu. Unaweza kumtusi, kumtemea mate na hata kumdharau. Hakutuachia nafasi ya kumuamulia Yeye kuwa ni nani.

Je, Yesu alisema yeye ni nani? Je, biblia inatuambia alikuwa nani? Kwanza tutazame maneno ya Yesu kutoka Yohana 10:30, “Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa juu juu, hapa hakuna taswira ya kuwa yeye pia ni Mungu. Lakini ukitazama majibizano ya wayahudi dhidi ya maneno yake, “Hatukupigi mawe kwa sababu nyinginezo ila kwa hili, kukufuru. Wewe ni mwanadamu tu lakini unajifanya sawa na Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa usemi wake Yesu ulimaanisha kuwa yeye ni Mungu. Katika andiko lifuatalo Yesu hakuwasahihisha kwa kusema, “si kuleta madai ya kuwa ni Mungu.” Ina maana ya kuwa Yesu alikuwa akisema kuwa yeye ni Mungu kwa msemo huwo, “Mimi na Baba yangu ni mmoja.” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwengine. Yesu alisema, “Amini, Amini nawaambia, kabla Abraham kuweko Nilikuwako.” Hali iliyowasukuma wayahudi kushika mawe iliwampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Yesu kutangaza kitambulisho chake kama, “Mimi ndimi” ambalo ni jina lilitumika sana kumaanisha Mungu katika Agano la kale ni ishara kuwa ni Mungu (Kutoka 3:14). Kwa nini wayahudi walitaka kumpiga mawe kama hakuwa amesema kitu ambacho kwao ni kufuru, madai ya Yesu kuwa ni Mungu?

Yohana 1:1 yasema, “na Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 yasema, “ na neno akafanyika mwili”. Hii ina maana ya kuwa Yesu ni Mungu katika mwili. Tomaso, mwanafunzi wa Yesu alisema, “Bwana wangu na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi. Mtume Paulo amtaja kama, “… Mungu wetu mkuu na mwokozi Yesu kristo” (Tito 2:13). Mtume petro asema, “Mungu wetu na mwokozi Yesu kristo” (Petro wa pili 1:1). Mungu Baba ni shahidi wa kuthibitika kwa Yesu Kristo, “Na kwa ajili ya mwana asema, “Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.” Unabii wa Agano la kale wamtaja Yesu kama Mungu, “Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa. Kwetu mtoto tumepawa na ufalme utakuwa mabegani mwake. Na ataitwa Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa amani.”

Kwa hivyo, kama C.S. Lewis alivyosema, kumtaja yesu kama mwalimu mwema tu si sawa. Yesu alikiri waziwazi kuwa yeye ni Mungu. Kama si Mungu basi ni muongo na si nabii, mwalimu mwema wala mcha mungu. Wanavyuoni wa sasa, husema, “Yesu yule wa kihistoria” hakusema mengi ya yale biblia inyomtaja nayo. Sisi ni wakina nani hata tupinge neno la Mungu kuhusu kile Yesu alisema ama kufanya? Mwanachuoni huyo wa miaka zaidi ya elfu mbili baada ya Yesu atakuwa na mtazamo gani wa kweli kushinda wale walioishi na kumtumikia Yesu kristo huku wakifundishwa pia (Yohana 14:26)?

Ni kwa nini, swali juu ya Yesu ni nani, ni muhimu? Kuna tatizo gani kama Yesu kweli ni Mungu au la? Swala muhimu linalompasa Yesu kuwa Mungu ni kwamba, kama si Mungu, kufa kwake hakungetosha kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu tu ndiye angeweza kufidia adhabu hiyo (Warumi 5:8; Wakorintho wa pili 5:21). Ilimlazimu Yesu kuwa Mungu ili alipe deni zetu. Yesu ilimbidi awe mwanadamu ili afe. Wokovu wapatikana tu kwa imani juu ya Yesu kristo! Uungu wa Yesu ndio unao sababisha yeye kuwa Njia ya pekee ya wokovu. Uungu wa Yesu ndio uliomfanya kukiri, “Mimi ndimi njia kweli na uzima. Hakuna ajaye kwa Baba ila kupitia Mimi” (Yohana 14:6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu kristo ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries