settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu angekuwa alifanya dhambi? Kama yeye hakuwa na uwezo wa kutenda dhambi, ni jinsi gani Yeye kweli angekuwa na uwezo wa kutuhurumia katika unyonge wetu (Waebrania 4:15)? Kama hakuweza kutenda dhambi, lengo la majaribu ni nini?

Jibu


Kuna pande mbili kwa swali hili la kuvutia. Ni muhimu kukumbuka kwamba hili sio swali la kama Yesu alitenda dhambi. Pande zote mbili hukubaliana, kama vile Biblia inavyosema, kwamba Yesu hakufanya dhambi (2 Wakorintho 5:21, 1 Petro 2:22). Swali ni kuwa kama Yesu alisini. Wale wa mtizamo kuwa hukuwa na uwezo wa kutenda dhambi wanaamini kuwa Yesu hakutenda dhambi. Wale wa mtizamo kuwa Yesu alikua na uwezo wa kutenda dhambi wanaamini kuwa Yesu alikua na uwezo wa kusini, lakini hakutenda dhambi. Ni mtizamo upi uko sahii? Mafunzo sahii ya maandiko ni kwamba, Yesu alikua “asiye na dhambi” Kamwe Yesu hangeweza kuwa na dhambi, vile vile hawezi kuwa na hali ya dhambi hii leo kwa sababu yeye angali na ile asili alikua nayo wakati aliishi duniani. Yeye ni Mungu-Mwanadamu na milele atabaki hivyo, baada ya uungu na ubinadamu kamili kuunganishwa pamoja kwa mtu mmoja bila utengano wowote. Kuamini kwamba Yesu angeweza kutenda dhambi ni kuamini kwamba Mungu angeweza tenda dhambi. “Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilfu wote ukae” (Wakolosai 1:19). Wakolosai 2:9 Anaongeza kuwa, “Maan katika yeye unaka utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”

Ingawa Yesu ni binadamu kamili, Hakuzaliwa na hali ya dhambi ya asili kwamba sisi huzaliwa nayo. Bila shaka alijaribiwa katika njia na namna hiyo sisi hujaribiwa, kwa kuwa majaribu yalikuwa yamewekwa mbele yake na Shetani, lakini yeye akakaa bila dhambi kwa sababu Mungu hana ile hali ya dhambi. Ni kinyume cha asili yake (Mathayo 4:1; Waebrania 2:18, 4:15; Yakobo 1:13). Dhambi kwa ufafanuzi ni hatia ya sheria. Mungu aliumba sheria, na sheria ni asili ya mapenzi ya Mungu ya kile atakacho kifanya au chenye hafanyi, kwa hiyo, dhambi ni kitu chochote ambacho Mungu hawezi fanya kwa ajili ya asili yake.

Kujaribiwa katika hali yake si ya dhambi. Mtu anaweza kukujaribu kwa kitu huna haja ya kukifanya, kama vile kufanya mauaji au kushiriki katika upotovu wa kijinsia. Pengine huna haja yoyote ya kushiriki sehemu yoyote katika hatua hizi, lakini bado ulijaribiwa kwa sababu mtu ,mwingine aliweka uwezekano wa kutenda mbele yako. Kuna ufafanuzi angalau aina mbili kwa neno “kujaribiwa”

1) Kwa kuwa na kauli ya dhambi imependekezwa kwako na mtu au kitu kisicho toka kwako mwenyewe au kwa ajili ya dhambi yako mwenyewe ya asili.

Kufikiria kweli kushiriki katika tendo la dhambi na raha iwezekanavyo na matokeo ya tendo kwa kiwango hicho ni tendo tayari ushachukua nafasi katika akili yako.

Ufafanuzi wa kwanza hauelezi tendo /wazo la dhambi; lakini ule wa pili wafafanua. Wakati unaishi katika tendo la dhambi na kufikiria jinsi unaweza kuwa na uwezo wa kulipita, umeuvuka mstari wa dhambi. Yesu alijaribiwa katika mtindo wa ufafanuzi moja ila kwa kuwa Yeye alikuwa kamwe hajaribiwi na asili ya dhambi kwa sababu haikuwepo ndani mwake. Shetani alipendekeza matendo fulani ya dhambi kwa Yesu, lakini hakuwa na hamu ndani yake ya kushiriki katika dhambi. Kwa hivyo, alijaribiwa jinsi na namna tunavyojaribiwa lakini alibaki bila dhambi.

Wale ambao ni wa mtizamo kuwa Yesu alikua na uwezo wa kutenda dhambi lakini hakutenda dhambi kuamini, kama Yesu hakuweza kufanya dhambi, Yeye hakuweza pitia majaribu sahii na kuwa na ule uzoefu, na kwa hivyo hawezi kamwe kuwa na hisia na mapambano yetu na majaribu dhidi ya dhambi. Na tukumbuke kwamba sio lazima mtu awe na uzoefu wa kitu ili akielewe. Mungu anajua kila kitu na kuhusu kila kitu. Huku Mungu akiwa hajawahi hisi hamu ya dhambi, na hajawai tenda dhambi, Mungu anajua na kuelewa dhambi ni nini. Mungu anajua na kuelewa mtu uhisi namna gani anapojaribiwa. Yesu anaweza kutambua hisia na majaribu yetu kwa sababu yeye anajua sio kwa sababu Yeye ako na “uzoefu” wa mambo yote tuliyonayo.

Yesu anajua hali huwa namna gani unapojaribiwa, lakini hajui huwa namna gani mtu akitenda dhambi. Hii haimzui yeye kutusaidia. Sisi hujaribiwa na dhambi ambazo ni za kawaida kwa mtu (1 Wakorintho 10:13). Dhambi hizi kwa ujumla zinaweza kujumlishwa chini ya aina tatu tofauti: “Tamaa ya macho, tamaa ya mwili, na kiburi cha uzima” (1 Yohana 2:16 NKJV). Chunguza majaribu na dhambi ya Hawa, vile vile na majaribu ya Yesu, na utakuta kwamba kila jaribu latokana na makundi hayo matatu. Yesu alijaribiwa katika kila njia na katika kila hali amboyo sisi tuliomo, lakini alibaki kuwa kamilifu na takatifu. Ingawa asili yetu iliyoharibiwa kuwa na hamu ya ndani ya kushiriki katika dhambi fulani, tuna uwezo kwa njia ya Kristo ya kushinda dhambi kwa sababu sisi hatumo tena watumwa wa dhambi bali watumwa wa Mungu (Warumi 6, hasa mistari ya 2 na 16-22 ).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu angekuwa alifanya dhambi? Kama yeye hakuwa na uwezo wa kutenda dhambi, ni jinsi gani Yeye kweli angekuwa na uwezo wa kutuhurumia katika unyonge wetu (Waebrania 4:15)? Kama hakuweza kutenda dhambi, lengo la majaribu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries