settings icon
share icon
Swali

Biblia inasem nini kuhusu wivu?

Jibu


Wakati tunatumia neno "wivu," tunalitumia kwa maana ya kuwa na wivu na mtu ambaye ana kitu hatuna. Aina hii ya wivu ni dhambi na si tabia ya Kikristo; badala yake, inaonyesha kwamba sisi bado tunadhibitiwa na tamaa zetu wenyewe (1 Wakorintho 3: 3). Wagalatia 5:26 inasema, "Tusijisifu bure, tukichokozanana kuhusudiana."

Biblia inatuambia kwamba tunapaswa kuwa na aina kamili ya upendo ambao Mungu anao kwetu. "Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu, upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya" (1 Wakorintho 13: 4-5). Tunapozidi kujizingatia wenyewe na tamaa zetu wenyewe, tutamzingatia Mungu kidogo. Wakati tunaifanya mioyo yetu kuwa ngumu kwa ukweli, hatuwezi kurejea kwa Yesu na kumruhusu kutuponya (Mathayo 13:15). Lakini wakati tunaruhusu Roho Mtakatifu kutudhibiti, Yeye huzalisha ndani yetu tunda la wokovu wetu, ambalo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole, na kujizuia (Wagalatia 5: 22- 23).

Kuwa na wivu inaonyesha kwamba haturidhiki na kile ambacho Mungu ametupa. Biblia inatuambia kuwa tutosheke na kile tunacho, kwa kuwa Mungu kamwe hawezi shindwa au kutuacha (Waebrania 13: 5). Ili kukabiliana na wivu, tunahitaji kuwa zaidi kama Yesu na sio kama sisi wenyewe. Tunaweza kupata kujua kutoka kwake njia ya kujifunza Biblia, maombi, na ushirika na waumini kukomaa. Kama sisi tunajifunza jinsi ya kuwatumikia wengine badala ya sisi wenyewe, mioyo yetu itaanza kubadilika. "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza, na ukamilifu." (Warumi 12: 2).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasem nini kuhusu wivu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries