settings icon
share icon
Swali

Je, sisi wote ni watoto wa Mungu, au Wakristo tu pekee?

Jibu


Biblia ii wazi kwamba watu wote ni viumbe wa Mungu (Wakolosai 1:16), na kwamba Mungu anaipenda dunia nzima (Yohana 3:16), lakini ni wale tu ambao wamezaliwa mara ya pili ndio watoto wa Mungu (Yohana 1:12; 11:52; Warumi 8:16, 1 Yohana 3:1-10).

Katika maandiko, waliopotea kamwe hawajulikani kuwa watoto wa Mungu. Waefeso 2:3 inatuambia kwamba kabla ya sisi kuokolewa sisi tulikuwa "kiasili wana wa hasira" (Waefeso 2:1-3). Warumi 9:8 inasema kwamba "si watoto wa kawaida ambao ni watoto wa Mungu, lakini ni watoto wa ahadi ambao ni kuonekana kama uzao wa Ibrahimu." Badala ya kuzaliwa kama watoto wa Mungu, sisi tumezaliwa katika dhambi, ambayo hutenganisha sisi kutoka kwa Mungu na kutuweka sisi pamoja na Shetani kama adui wa Mungu (Yakobo 4:4, 1 Yohana 3:8). Yesu alisema, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa maana nalitoka kwa Mungu na mimi nimekuja; wal sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma" (Yohana 8:42). Kisha mistari michache baadaye Yohana 8:44, Yesu aliwaambia Mafarisayo kwamba "nanyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda." Ukweli kwamba wale ambao hawajaokoka si watoto wa Mungu pia huonekana katika 1 Yohana 3:10: "Katika hili watot w Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake."

Sisi huwa wana wa Mungu wakati tumeokolewa kwa sababu tumetwaliwa katika familia ya Mungu kwa njia ya uhusiano wetu na Yesu Kristo (Wagalatia 4:5-6, Waefeso 1:5). Hii inaweza kuonekana wazi katika mistari kama Warumi 8:14-17: "... wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto, basi tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutkuzwa pamoja naye.” Wale ambao wameokolewa ni watoto wa Mungu "kupitia imani katika Kristo Yesu" (Wagalatia 3:26) kwa sababu Mungu "kwa kuwa alitangulia kutuchukua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu sawaswa na Uradhi wa mapenzi" (Waefeso 1:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, sisi wote ni watoto wa Mungu, au Wakristo tu pekee?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries