settings icon
share icon
Swali

Je! Wanandoa ambao wameachana wanaweza kuolewa tena?

Jibu


Yesu alipokuja katika ulimwengu huu, “alizaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sharia” (Wagalatia 4:4-5). Mkristo anapaswa “Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa” (Wagalatia 5:1). Maandiko yanaweka wazi kabisa kwamba sisi tulio ndani ya Kristo hatuko chini ya Sheria ya Agano la Kale. Badala yake, “tunaenenda katika Roho” (Wagalatia 5:16) na kufuata “sharia ya Kristo” (Wagalatia 6:2).

Sheria ya kumbukumbu la Torari 24:4 ilikuwa sehemu ya kanuni za Mungu juu ya talaka, desturi ambayo Yeye alivumilia, lakini hakuipuuza, kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya Waisraeli (Mathayo 19:8). Musa alihitaji hati ya kisheria, iliyoandikwa ya talaka (Kumbukumbu 24:1) na akawazuia “kupindua” talaka. Kanuni zote mbili zilihesabiwa ili kusisitiza uzito na mwisho wa talaka. Kimsingi, Mungu alikuwa akisema, “Talaka ni jambo zito sana; usichukue hatua hii kirahisi.”

Leo hii, wenzi wa ndoa wangefanya vyema kufuata neno la Yesu na kuacha kikamilifu kile ambacho Mungu ameunganisha (Mathayo 19:6). Wanandoa waliotalakiana, ingawa hawafungwi kufuata maelezo ya Sheria ya Agano la Kale, bado lazima wazingatie athari zote za kuoa tena. Ikiwa uhusiano na mwenzi wa zamani utasonga mbele, ushauri wa kichungaji unapendekezwa ili kuhakikisha kuwa mambo yaliyosababisha talaka hapo awali yamekabiliwa na kuzuluhishwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wanandoa ambao wameachana wanaweza kuolewa tena?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries