settings icon
share icon
Swali

Wakristo wanastahili kutii sheria ya nchi?

Jibu


Warumi 13:1-7 yasema, “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; asahiliye heshima, heshima.”

Ufahamu huu unaifanya kamili wazi kuwa tunastahili kutii serikali ambayo Mungu ameiweka juu yetu. Mungu aliiumba serikali ili iweke mpangalio, adhabu ya maovu, na kuendeleza haki (Mwanzo 9:6; 1 Wakorintho 14:33; Warumi 12:8). Tunastahili kutii serikali kwa kila jambo- kulipa ushuru, kutii amri na sheria, na kuonyesha heshima. Ikiwa hatutafanya hivyo, twaonyesha kutokuwa na heshima/madharau kwa Mungu, kwa sababu ni yeye Mwenyewe ameiweka serikali juu yetu. Wakati mtume Paulo aliandika Warumi, alikuwa chini ya serikali ya Rumi wakati wa mfalme Niro, ingawa alikuwa mfalme mwovu kati ya wafalme wote wa Rumi. Paulo bado aliitambua serikali ya Kirumi kuwa na mamlak juu yake. Tunawezaje kufanya chini ya hiyo?

Swali lingine ni “Kunao wakati tunastahili kukaidi sheria ya nchi kimakusudi?” Jibu kwa swali hilo linaweza patikana katika Matendo Ya Mitume 5:27-29, “Walipowaleta, wakawaweka katika baraza, kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu Yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” Hii iko wazi kuwa bora tu sheria ya nchi haitilafiani na sheria ya Mungu, wote tumefungwa kuitii sheria ya nchi. Pindi tu sheria ya nchi inahitilafiana na amri ya Mungu, tunastahili kuikataa sheria ya nchi na kutii sheria ya Mungu. Ingawa hata kwa hali hiyo tunastahili kuikubali mamlaka ya serikali juu yetu. Hii imedhihirishwa kwa hoja kuwa Petro na Yohana hawakuwapinga kwa kuwateswa, bali walifurahi kuwa waliteseka kwa kumtii Mungu (Matendo Ya Mitume 5:40-42).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wakristo wanastahili kutii sheria ya nchi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries