settings icon
share icon
Swali

Je, ni kwa nini Wakristo hujaribu kulazimisha maadili yao kwa wengine?

Jibu


Mara nyingi Wakristo hushutumiwa kwa kujaribu kulazimisha maadili yao au imani yao kwa wengine. Shtaka linalosikika mara nyingi ni kwamba Wakristo wanajaribu “kulazimisha dini yao kwetu.” Katika kujibu swala hili, ni lazima pia tushughulikie shtaka linalodokezwa kwamba Wakristo ni kikundi cha kimabavu ambacho kinataka kukandamiza haki za wengine. Bila shaka, kumekuwa na watawala jeuri ambao walidai kuwa Wakristo, lakini wafuasi wa kweli wa Kristo hawatafuti kukiuka haki za msingi za kibinadamu za mtu yeyote. Mungu yule yule aliyetoa hiari kwa muumini pia ndiye alitoa hiari kwa asiyeamini.

Mungu huongeza baraka zake za jumla kwa kila mtu (Mathayo 5:45); kwa hivyo, uhuru kwa wote ni thamani ya Kikisto. Mwanadamu ni kiumbe maalum cha Mungu (Mwanzo 1:27); kwa hivyo, utu na heshima ya kibinadamu kwa mtu binafsi ni maadili ya Kikristo.

Wengine husema kwamba ni makossa kujaribu ”kutoa sheria ya maadili.” Tunasema kwamba haiwezekani kutofanya hivyo. Kila sheria “hulazimisha” maadili ya mtu kwa mtu mwingine. Kwa mfano, sheria ambayo inakataza mauaji, inalazimisha imani kwamba kuua ni kosa na kuunga mkono kanuni ya Kikristo kwamba uhai wa mwanadamu una thamani ya asili.

Karibu kila mtu anakubali kwamba mauaji, uzinzi, wizi, uongo, ni uchoyo ni mbaya. Watu wengi wanakubali kwamba mtu kuheshimu wazazi ni bora. Hisia hizi za mema na mabaya, ambayo yameunganishwa katika mfumo wa jamii yetu, unaakisi amri sita kati ya Amri Kumi za Biblia. Wale wanaopinga “kuwekwa” kwa maadili Kiyahudi-Kikristo labda wanapaswa kufanya juhudi za kufuta sheria dhidi ya mauaji, kutoa ushahidi wa uongo, na wizi

Wakristo hawataki kulazimisha maadili yao, bali wanataka kutambua kwamba, katika kila jamii, maadili ya mtu lazima yatawale. Swali ni, ni maadili ya nani yatatawala? Hakuna kitu kama mfumo wa maadili ya katikati yasiyo egemea upande wowote. Kwa hivyo, Wakristo hujitahidi ili kuendeleza maadili yao kwa imani ya kweli kwamba, katika ulimwengu wa imani zenye kushindana, maadili ya Kikristo yanakuza ustawi wa jumla na kuhifadhi utulivu nyumbani.

Wakristo hawataki kulazimishia maadili yao, lakini wanaona umuhimu wa kuwa na mamlaka iliyo juu kutuliko. Jamii zinazojaribu kutoa kanuni za maadili yanayoegemea mantiki ya kibinadamu yanaweza kubadilishwa na yeyote aliye na kura nyingi au silaha zaidi. Iwe ni kisa cha mdhalimu wa binadamu kama vile Joseph Stalin au udhalimu wa pamoja kama vile Mapinduzi ya Ufaransa, kutengwa kwa kanuni za Kikristo husababisha uhuru mdogo mno, na sio zaidi.

Wakristo hawataki kulazimisha maadili yao, bali wanataka kuishi kwa amani katika jamii yoyote wanamoishi (Warumi 12:18; 1 Timotheo 2:2). Wakristo wana wajibu wa kutenda mema kwa watu wote (1 Wakorintho 6:10) na kuombea kila mtu (1 Timotheo 2:1). Kristo aliwafunza wafuasi wake kujiibu baraka kwa laana (Mathayo 5:44), funzo ambalo aliigiza kikamilifu (1 Petro 2:23).

Kuna baadhi ya watu wanaotamani laiti kungekuwa na jamii ya “kidunia” pekee ambapo dini imekandamizwa na maoni yote ya Kikristo yamenyamazishwa. Kwa watu kama hao, tunatoa vikumbusho vifuatavyo:
1) Wakristo wana haki ya kushiriki katika mchakato wa kisiasa kama mtu yeyote. Hii inamaanisha kwamba wanaweza kupiga kura, kufanya mikutano ya hadhara, kushawishi, kongamano na kuwa katika uongozi kama raia yeyote-huku wakiendeleza sheria zinazoakisi maadili yao wenyewe. Wakristo hawatafuti kupindua mchakato wa kisiasa; wanaishirikisha, kwa kuwa ni haki ya kila raia.
2) Wakristo katika jamii ya tamaduni nyingi wana haki ya kutoa maoni yao kama mtu yeyote. Hii inamaanisha wanaweza kutangaza, kuandika, kuongea, kuchapisha, na kuunda sanaa vile wapendavyo-wakati wote huku wakitoa maoni yao kuhusu maadili. Wakristo wakati mwingine wanatuhumiwa kuwa na udhibiti, kwa msingi kwamba wamekosoa kitabu fulani au wamepinga kutozwa ushuru kwa pesa wanazofadhili semi sinazopinga Ukristo, walakini hawachomi vitabu hivyo. Ukweli ni kwamba uhuru wa kujieleza ni thamani ya Kikristo.
3) Wakristo katika jamii huru ya kidini wana haki ya kuishi kulingana na imani yao kama mtu yeyote yule. Hii inamaanisha kuwa wanaweza kuhubiri na kufundisha injili na kuishi kulingana Biblia na dhamiri yao. Wakati Mkristo anasema, “Lazima uzaliwe mara ya pili” (Yohana 3:7),yeye hajaribu kulazimisha maadili yake; yeye anazungumza ukweli, ambao mtu yeyote yuko huru kuukubali au kuukataa.

Hakuna shaka kwamba wakati Wakristo wanaposhiriki imani yao katika Kristo, wengine huona hilo kama jaribio la kulazimisha Ukristo kwa wengine. Lakini ukweli ni kwamba kama Wakristo, tunajua kwamba tunayo dawa ya kuteseka kwa wanadamu katika maisha haya na umilele wa kuzimu katika maisha yajayo. Kutoshiriki tiba hiyo na wengine, kama tulivyoamriwa na Kristo kufanya (Mathayo 28:18-20), itakuwa sawa na kujua tiba ya saratani na ukatae kuishiriki na ulimwengu wote. Hatuwezi lazimisha imani yetu kwa mtu yeyote; kile tunaweza kufanya ni kuwapa tiba na kuomba waikubali. Ikiwa mtu ataona juhudi hizo kuwa “kulazimisha” imani yetu kwao, hili ni suala la maoni yao, na sio uakisi wa uhalisi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni kwa nini Wakristo hujaribu kulazimisha maadili yao kwa wengine?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries