settings icon
share icon
Swali

Ikiwa mwanamume ako na wake wengi, na akawa Mkristo, anapaswa kufanya nini?

Jibu


Kwa kuwa mitala haikubaliki katika jamii nyingi, hili ni swali ambalo watu wengi hulifikiria. Lakini bado kuna sehemu nyingi duniani ambapo mitala inakubaliwa. Nchi nyingi za Kiislamu zinaruhusu mitala. Kwa mwanaume kuwa na wake wengi ni jambo la kawaida katika mtaifa kadhaa ya Afrika. Hata Marekani, kuna baadhi ya jumuiya zinazoidhinisha mitala. Hata hivyo, takribani wasomi wote wa Biblia wanakubali kwamba mitala si ya Wakristo (tazama, Ni kwa nini Mungu aliruhusu mitala/kuwa wake wawili au wanaume wawili wakati mmoja katika Biblia?). Basi, mtu mwenye wake wengi anapaswa kufanya nini ikiwa amemwamini Yesu Kristo na kuwa Mkristo?

Watu wengi papo hapo hutoa jibu kama “awape ttalaka wake zake wote isipokuwa mmoja.” Ingawa hilo linaonekana kuwa suluhu la kimaadili, hali kwa kawaida si rahisi hivyo. Kwa mfano, atabaki na bibi mgani? Mke wake wa kwanza? Bibi wake wa mwisho? Bibi anayempedna zaidi? Bibi ambaye amemzalia watoto wengi? Na je, itakuaje kwa wake ambao anawataliki? Je! watajikidi namna gani? Katika tamaduni nyingi zinazoruhusu mitala, mwanamke aliyeolewa hapo awali ana nafsi ndogo sana ya kujikimu na hata uwezekano mdogo wa kupata mume mpya. Na watoto wa hawa bibi wataenda wapi? Mara nyingi hali ni hii ni ngumu sana. Hakuna suluhisho rahisi.

Hatuamini kuwa mtala ni jambo ambalo Mungu analikubali katika zama hizi. Hata hivyo, hakun amahali popote katika Biblia inatoa amri ya “usioe wake wengi.” Katika Agano Jipya, mwenye mitala hastahili uongozi wa kanisa (1 Timotheo 3:2, 12; Tito 1:6), lakini mitala yenyewe haijakatazwa. Kuoa wake wengi haikuwa nia ya awali ya Mungu (Mwanzo 2:24; Waefeso 5:22-33), lakini pia ilikuwa ni kitu alichoruhusu (angalia mifano ya Yakobo, Daudi, na Sulemani). Biblia inayokaribia sana kukataza mitala ni Kumbukumbu la Torari 17:7, ambayo inaeleweka vizuri kama amri ya Mungu dhidi ya mfalme wa Israeli kuoa wake wengi. Haiwezi kueleweka kama amri kwamba hakuna mwanamume anayeweza kuoa zaidi ya mke mmoja.

Kwa hiyo, ikiwa mwanamume ana wake wengi na akawa Mkristo, anapaswa kufanya nini? Ikiwa kuoa wake wengi ni kinyume cha sheria mahali anapoishi, anapaswa kufanya lolote linlohitajika ili kutii sheria (Warumi 13:1-17), huku akiwa bado akiyakidi mahitaji ya wake na watoto wake. Ikiwa ndoa ya wake wengi ni halali, lakini anahukumiwa kuwa ni makosa, anapaswa kuwataliki wote isipoluwa mke mmoja, lakini tena, asipuuze kuwaruzuku wote hao na watoto wao. Wao ni wajibu wake. Ikiwa ndoa ya wake wengi ni halali na hana hatia dhidi yake, anaweza kubaki ameolewa kwa kila mmoja wa wake zake, akimtendea kila mmoja kwa upendo, adhama, na heshima. Mtu anayefanya uamuzi huu atazuiliwa kutoka kwa uongozi wa kanisa, lakini haiwezi kusemwa kwamba anakiuka waziwazi amri yoyote katika Maandiko.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa mwanamume ako na wake wengi, na akawa Mkristo, anapaswa kufanya nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries