settings icon
share icon
Swali

Ni namna gani na ni lini vitabu vyote vya Bibilia viliwekwa pamoja?

Jibu


Neno “kanoni” limetumika kuelezea vitabu ambavyo viliandikwa kwa pumzi ya Mungu na kwa hivyo vinastahili kuwa katika Bibilia. Ugumu wa kutambua kanoni ya Kibibilia (Vitabu vinavyostahili kuwa katika Bibilia) ni kwamba Bibilia haitupi idadi ya vitabu vinavyostahili kuwemo katika Bibilia. Kuitambua kanoni ya Bibilia ulikua mjakato wa walimu wa Kiyahudi na wachanganusi wa Bibilia na kisha baadaye wale Wakristo wa kwanza. Zaidi ya yote ni Mungu mwenyewe ndiye aliamua ni kitabu kipi kilistahili kuwa katika kanoni ya Bibilia. Kitabu cha Bibilia kilijumlishwa kwa kanoni wakati ule Mungu aliweka pumzi yake katika uandishi wa Bibilia. Ilipelekea ushawishi wa Mungu kwa mwanadamu wanaomwamini kuamini ni kitabu gani kitakua katika Bibilia.

Kulinganisha na Agano Jipya kulikua na mfutano kuhuzu kanoni ya Agano La Kale. Waumini wa Kiyahudi waliwatambua watume wa Mungu na kukubali uandishi wao kuwa na pumzi ya Mungu. Kulikuwa na mijadala ambayo hatuwezi kuikataa kuhusu kanoni (vitabu vya) Agano La Kale kufika mwaka wa 250 A.D (Baada ya Yesu kuzaliwa) kulikuwa na kubaliano la jumla juu ya kanoni ya Bibilia ya Kiyahudi. Wengi wa wachanganusi wa Bibilia ya Kiyahudi. Jambo kuu lilikua lile la vile vitabu vilivyoachwa nche na vinakubalika na dini zingine, liliacha mdahalo na majadiliano ambao ulikuwa kwa wengi wa wachanganusi wa Bibilia wa Kiyahudi.

Kwa agano Jipya, mjakato wa kuvitambua kusanyiko la vitabu ulianza katika karne ya kwanza ya kanisa la Kikristo. Mapema kidigo, baadhi ya vitabu vya Agano Jipya vilikuwa vimetambulika. Paulo aliuchukulia uandishi wa Luka kuwa la pumzi ya Mungu sawa na Agano la Kale (1 Timotheo 5:18; pia angalia Kumbuku La Torati 25:4 na Luka 10:7). Petero aliutambua uandishi wa Paulo (2 Petero 3: 15-16). Baadhi ya vitabu vya Agano Jipya vilikuwa vimekwisha sambaswa katika makanisa yote (Wakolosai 4: 16; 1 Wathesalonike 5:27). Kilementi (Clement) wa Rumi alitaja karibu vitabu nane vya Agano Jipya (A.D. 95). Ignatius wa Antiokia alivitambua vitabu saba (A.D. 115). Polycarp aliyejufunza chini ya mtume Yohana alivitambua vitabu 22 (A.D. 170-235). Vitabu vya Agano Jipya vilivyokuwa na utata ni Waebrania, Yakobo, 2 Petero, 2 Yohana, na 3 Yohana.

Kanoni ya kwanza ilikua ile ya Muratori (Muratorian) ambayo iliwekwa pamoja mwaka wa A.D 170. kanoni ya Muratori ilikuwa na vitabu vyote vya Agano Jipya, Vitabu vilivyokosa ni Waebrania, Yakobo na 3 Yohana. Mwaka wa A.D 363, kikao cha Laodikia kilisema kwamba Agano La Kale pekee (pamoja na vitabu 27 vya Agano Jipya ndivyo vingesomwa pekee katika makanisa. Kikao cha Hippo (A.D 393) na kikao cha Carthage (A.D. 397 pia vyathibitisha vitabu hivi 27 kuwa na pumzi ya Mungu.

Vikao hivi vilifuata njia zile zile za kutambua kwamba vitabu vya Agano Jipya viliandikwa kupitia Roho Mtakatifu: 1) Je! Mwandishi alikua mwanafunzi wa Yesu au alikua na uhusiano wa karibu na mitume? 2) je! Kitabu kimekubalika na makanisa yote? 3) Je! Kitabu kilikua na mafunzo ya kweli? 4) Je! Kitabu chenyewe kilikuwa na ushuhuda wa hali ya juu ya matunda ya Roho Mtakatifu? Pia, kitu cha muimu kukumbuka kwamba si kanisa ilikua na uamuzi juu ya kanoni. Hakuna kikao cha kanisa la kwanza kilifanya uamuzi juu ya kanoni. Ni Mungu tu pekee aliamua ni kitabu gani kilistahili kuwekwa kwa Bibilia. Ilikua tu jukumu la Mungu kuwawekea yale aliyoyataka wayaandike. Jitiada za watu za kukusanya vitabu vya Bibilia ziliendelea lakini Mungu kwa uweza wake, na mbali na kutojua kwetu na tutuku wetu, aliifanya kanisa la kwanza kutambua vitabu alivyokuwa na pumzi yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni namna gani na ni lini vitabu vyote vya Bibilia viliwekwa pamoja?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries