settings icon
share icon
Swali

Mbinguni inafanana namna gani?

Jibu


Mbinguni ni mahali halisi ilivyoelezwa katika Biblia. neno "mbinguni" linapatikana mara 276 katika Agano Jipya peke yake. Bibilia inarejelea mbinguni tatu. Mtume Paulo alikuwa "amechukuliwa juu katika mbingu ya tatu," lakini alikatazwa kufunua kile alichokiona huko (2 Wakorintho 12:1-9).

Kama mbingu ya tatu ipo, ni lazima pawepo na mbingu zingine mbili. Ya kwanza mara nyingi inajulikana katika Agano la Kale kama "wingu" au "anga." Hii ni mbinguni ambayo ina mawingu, eneo ambalo ndege huruka kupitia. Mbingu ya pili ni bain aya nyota / anga, ambayo ni makaazi ya nyota, sayari, na vitu vingine vya angani Mwanzo 1:14-18).

Mbingu ya tatu, eneo ambalo halijawekwa wazi, ni makao ya Mungu. Yesu aliahidi kuandaa nafasi kwa ajili ya Wakristo wa kweli mbinguni (Yohana 14:2). Mbinguni pia ndio hatima ya watu wa Mungu katika Agano la Kale ambao walikufa wakiamini ahadi ya Mungu ya mkombozi (Waefeso 4:8). Kila mtu amwaminiye Kristo hawatapotea bali watapata uzima wa milele (Yohana 3:16).

Mtume Yohana aliwezeshwa kuuona na kutoa taarifa juu ya mji wa mbinguni (Ufunuo 21:10-27). Yohana alishuhudia kwamba mbinguni (nchi mpya) ina "utukufu wa Mungu" (Ufunuo 21:11), uwepo wa Mungu. Kwa sababu mbinguni hana usiku na Bwana mwenyewe ndiye mwanga, jua na mwezi hazihitajiki tena (Ufunuo 22:5).

Mji huo umejazwa na uzuri wa mawe ya thamani na kioo wazi cha almasi. Mbinguni ina milango kumi na miwili (Ufunuo 21:12) na misingi kumi na miwili (Ufunuo 21:14). Paradiso ya bustani ya Edeni imerejeshwa: mto wa maji ya maisha unatiririka kwa uhuru na mti wa uzima unapatikana kwa mara nyingine tena, ukizaa matunda ya kila mwezi na majani ambayo "huponya mataifa" (Ufunuo 22:1-2). Hata hivyo Yohana mtu mfasaha alikuwa katika maelezo yake ya mbinguni, hali halisi ya mbinguni ni zaidi ya uwezo wa mwanadamu aliye na mwisho kuelezea (1 Wakorintho 2:9).

Mbinguni ni mahali pa "hamna tena." Hakutakuwa na machozi tena, hamna maumivu tena, na hakuna huzuni tena (Ufunuo 21:4). Hakutakuwa na utengano tena, kwa sababu ya kifo kitashindwa (Ufunuo 20:6). Jambo bora juu ya mbinguni ni uwepo wa Bwana na Mwokozi wetu (1 Yohana 3:2). Sisi tutakuwa na Mwana-kondoo wa Mungu uso kwa uso na ambaye alitupenda, na alijitoa sadaka mwenyewe ili tuweze kufurahia uwepo wake katika mbingu milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mbinguni inafanana namna gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries