settings icon
share icon
Swali

Je! Nimwambie mwenzi wangu kuhusu uraibu wangu wa ponografia?

Jibu


Mapambano dhidi ya uraibu wa ponografia kwa kawaida huwekwa kama siri, lakini kuna faida za kumwambia mwenzi wa ndoa. Uamuzi wa k ufanya hivyo unapaswa kutanguliwa na sala na maliwazo mengi (Mithali 3:5-6; Yakobo 1:5).

Biblia inasema, “Kwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana” (Yakobo 5:16). Hili linafanya kazi kanisani, na linaweza fanya kazi katika uhusiano wa ndoa. Ni vigumu kupona kabisa kutokana na uraibu huo ikiwa mtu hatafichua dhambi hiyo kwa mwenzi wake na kumjumuisha mwenzi wake katika urejesho.

Uraibu wa ngono mara nyingi hujulikana kama “ugonjwa kwa kimapenzi.” Robert Weiss, mtaalamu wa uraibu wa ngono, anafafanua ugonjwa wa mapenzi kuwa “kutoweza kupata, kuvumilia, au kuka katika uhusiano unaohusisha hatari zinazoletwa na kujulikana kikamilifu.” Mungu alituumba kama viumbe vya kijamii (Mwanzo 2:18). Kama vile Weiss anavyosema, “Sote tunahitaji mahusiano yenye afya kwa ajili ya kuendelea kuishi—ni muhimu sana. Hatufanyi vizuri peke yetu.”

Kwa hiyo, ili kuwa na kajamiiana tunahitaji kuwa na uwezo wa kujionyesha kikamilifu kwa wenzi wetu-wema, wabaya, na wasio warembo. Kuficha uraibu wa ponografia kunamaanisha kuficha sehemu muhimu y amaisha ya mtu na kuifungia kutoka kwa mwenzi wake.

Wakati wanandoa hatimaye wanajua kuhusu uraibu wa ponografia, katika hali nyingi, wanakubali tayari walijua kitu hakikuwa sawa—lakini hakuwa anajua ni nini hasa. Kuongezea, kuna wanandoa wengi wanaodhani wao wenyewe ndio tatizo; wakati mtu anajitenga kwa sababu ya aibu ya kuteleza au kujihushisha na tabia za dhambi, mwenzi wake mara nyingi huamini kuwa ni kosa lake. Kwa kweli, kutengwa ndio hasa huleta maumivu makali wakati wanandoa wanapogundua tabia. Wanadhurika kwa kuwa walikuwa wakijilaumu muda huu wote.

Kwa kuongezea, ikiwa mtu atafichua kwa hiari uraibu wa ponografia, badala ya mwenzi wake kugundua kwa njia nyingine, inapunguza kiwango cha kiwewe ambacho wanandoa hupata. Utafiti wa hivi majuzi wa Barbara Steffens, mtaalam wa kiwewe cha uhusiano, ulionyesha kwamba kipengele kimoja ambacho huzidisha kiwewe wakati mwenzi anapogundua ni kipindi ambacho dhambi ilifichwa. Kadri muda unavyopita, ndivyo maumivu yanavyoongezeka.

Faida nyingine kubwa ya kumwambia mwenzi wa ndoa ni fursa ya kushiriki naye afueni kutokana na uraibu huo. Ingawa kufichua kutakuwa chungu, kushiriki katika maumivu hayo kunaweza kuwa fursa nzuri ya kuunganisha.

Sasa, kila mara kuna hali ambapo kufichua uraibu kunaweza kuwa hatari na huenda ukahitaji kuchukua tahadhari za wakati na jinsi unavyofichua. Ikiwa mwenzi wako ana changamoto za kisaikolojia na kihisia au anakabiliana na magonjwa mengine au hali za shida, huenda asiweze kukabiliana na msizitizo wa ziada wa ungamo la uraibu wa ponografia wakati huo.

Uamuzi huu unapaswa kuwa wako, kwa sababu kuna hatari. Na inashuriwa kusonga mbele chini ya uongozi wa mshauri wa Kikristo, aliye na msingi katika Neno (Mithali 11:14). Mwishowe, thawabu za kuungama dhambi zinastahili maumivu ya kuungama.

Pornaddiction.com ina maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufichua uraibu wako wa ponografia kwa mwenzi wako.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Nimwambie mwenzi wangu kuhusu uraibu wangu wa ponografia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries