settings icon
share icon
Swali

Ukristo wa kiroho ni nini?

Jibu


Wakati sisi tunazaliwa mara ya pili, sisi hupokea Roho Mtakatifu ambaye hututia mhuri kwa siku ya ukombozi (Waefeso 1:13; 4:30). Yesu aliahidi kwamba Roho Mtakatifu atatuongoza kwakeli "kweli yote" ( Yohana 16:13). Sehemu ya ukweli huo huchukua mambo ya Mungu na kuyaweka katika matumizi kwa maisha yetu. Wakati matumizi hayo yamefanywa, muumini basi hufanya uamuzi wa kuruhusu Roho Mtakatifu kumtawala. Ukristo wa kweli kiroho msingi wake unategemea kiwango ambacho muumini ameookoka anaruhusu Roho Mtakatifu kumwongoza na kudhibiti maisha yake.

Mtume Paulo anawaambia waumini wajazwe na Roho Mtakatifu. "Tena msilew kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho"( Waefeso 5:18). Mstari katika kifungu hiki ni endelevu na kwa hiyo una maana ya "kuendelea kujazwa na Roho." Kujazwa na Roho ni kuruhusu Roho Mtakatifu kutudhibiti badala ya kujitoa kwa tamaa zetu wenyewe za kidunia. Katika kifungu hiki Paulo anafanya ulinganisho. Wakati mtu anadhibitiwa na mvinyo, yeye ni mlevi na anaonyesha sifa kama vile kukokotesha usemi, kutapatapa kwa kutembea, na maamuzi pungufu. Kama vile unavyoweza kusema wakati mtu ni mlevi kwa sababu ya sifa yeye anaonyesha, vivyo hivyo muumini aliyezaliwa mara ya pili ambayeanadhibitiwa na Roho Mtakatifu huonyesha tabia yake. Stunapata sifa hizo katika Wagalatia 5:22-23 ambapo zinaitwa "matunda ya Roho." Huku ndiko kukuwa kiroho kwa kweli kwa Kikristo, inayozalizwa na Roho ambaye anafanya kazi katika na ndani ya muumini. Tabia hii haizalishwi kwa juhudi binafsi. Muumini aliyezaliwa mara ya pili ambaye anadhibitiwa na Roho Mtakatifu ataonyesho usemi bora, kuendelea kutembea katika roho, na kufanya maamuzi kwa misingi ya neno la Mungu.

Kwa hivyo, Ukristo wa kiroho unahusisha uchaguzi tunaoufanya "kujua na kukua" katika uhusiano wetu wa kila siku na Bwana Yesu Kristo na kunyenyekea kwa huduma ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Hii ina maana kwamba, kama waumini, tunafanya uamuzi wa kuweka mawasiliano yetu na Roho kwa kukiri (1 Yohana 1:9). Wakati tunamhuzunisha yule Roho kwa dhambi ( Waefeso 4:30, 1 Yohana 1:5-8), tunajenga kizuizi kati yetu na Mungu. Wakati sisi hujiwasilisha kwa huduma ya Roho, uhusiano wetu haukatishwi (1 Wathesalonike 5:19). Ukristo wa Kiroho ni kuwa fahamu ya ushirika na Roho wa Kristo, bila kukatishwa na umwili na dhambi. Ukristo wa kiroho huanza wakati muumini aliyeokoka anafanya uamuzi thabiti na endelevu na kujisalimisha kwa huduma ya Roho Mtakatifu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ukristo wa kiroho ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries