settings icon
share icon
Swali

Je! Itikio la Mkristo linapaswa kuwa gani kwa ukosefu wa ngono katika ndoa (ndoa isiyo na ngono)?

Jibu


Kujamiiana ni sehemu ya mpango wa kawaida wa Mungu kwa ndoa, mume na mke wana wajibu wa kukidhi mahitaji ya kila mmoja wao katika eneo hili (1 Wakorintho 7:2-4). Iwapo hakuna hali ya kimwili au kiafya ambayo inaweza kuzuia tendo la ngono, ukosefu wa ngono katika ndoa unapaswa kuwepo kwa makubaliano kwa ajili ya mambo ya kiroho kwa muda mfupi (1 Wakorintho 7:5).

Ndoa isiyo na ngono ni haja ya kushughulikia. Tena ukionda matatizo ya kimwili, kuna uwezekano kuwa chanzo kinaweza kuwa chaa kiroho. Utaratibu wa kwanza wa kuanza kushughulikia ni kuomba kwa ajili ya hekima, rehema, na neema ya kukusaidia wakati wa hitaji (Yakobo 1:5; Waebrania 4:16). Wakati wote ni vizuri kupanga nyumba yako mwenyewe kabla ya kutafuta kumrekebisha mtu mwingine; kwa hiyo ikiwa mwenzi anahisi amekosewa katika eneo hili, anapaswa kumwomba Bwana afunue chochote anachoweza kufanya ili kuchangia kwa tatizo hilo (Zaburi 139:23). Mungu atajibu sala kama hiyo mradi tu tuko tayari kusikiliza.

Iwapo mwenzi aliyenyimwa ngono atagundua kwamba amechangia sababu ya ukosefu wa ngono katika ndoa, dahmbi hiyo inapaswa kuungamwa kwa Mungu na kwa mwenzi na hatua zichukuliwe kurekebisha tabia hiyo (Mithali 28:13). Ikiwa hii imefanywa na uhusiano wa kimapenzi bado umezuiliwa, mwenzi aliyekosewa anapaswa kuendelea kuomba kila siku kwa neema ya kupenda bila masharti na kumwamini Mungu kutenda muujiza kwa wakati wake. Hili sasa ni jaribu la imani (Yakobo 1:2-4). Wakati huo, mwenzi aliyenyimwa anapaswa kuacha wazi njia za mawasiliano na mwenzi wake na kamwe asipuuze amri za Mungu kuhusu uhusiano wa ndoa (Waefeso 5:22-33). Inachukua muda na subira kumngoja Bwana na kumtazamia Yeye katika kuinuka zaidi ya mazingira.

Ikiwa ukosefu wa ngono katika ndoa ni kwa sababu ya mke kukataa kujamiiana, mume anapaswa kuzingatia kama yeye ni mtiifu kwa amri ya Mungu ya kumpenda mke wake kama Kristo anavyolipenda kanisa (Waefeso 5:25-33) au kama anaishi naye. kwa “njia ya maelewano” (1 Petro 3:7). Hii ni muhimu hasa ikiwa ana hisia ya udhalili na kukataliwa. Mara nyingi, huenda mume asitambue sehemu yake katika matatizo ya mke wake, naye anatenda tu kwa sababu ya kufadhaika au hasira iliyozuiliwa. Mawasiliano ya uaminifu na msamaha ni njia bora za kushughulikia suala hili; kuwa mwangalifu ili kuepuka kucheza “mchezo wa lawama.” Wakorintho wa Kwanza 13 inaweza kuwa orodha—je! maelezo ya sura hiyo ya upendo yanalingana na jinsi mume anavyomtendea mke wake? Upendo wa kimungu utamzuia kuwa na uchungu dhidi ya mke wake na ukali kwake (Wakolosai 3:19).

Ikiwa ukosefu wa ngono katika ndoa ni kwa sababu ya mume kukata kuonana kimwili na mkewe, mkewe anaweza kuwa ndiye amepuuza wajibu wake mbele ya Mungu wa kumpenda, kumheshimu, na kujitiisha kw amume wake (Waefeso 5:22-24). Ikiwa anahisi kupuuzwa, udhalali, au kutawaliwa, anaweza kukataa urafiki ili kulipiza kisasi au kudhibiti tena, au anaweza kupoteza kumpendezwa kabisa. Vyovyote vile, “Angalieni sana mtu yeyote asiikose neema ya Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo” (Waebrania 12:15).

Ikiwa mwenzi anamnyima mwingine ngono bila sababu, kunaweza kuwa na shida kubwa, iliyokandamizwa inayotokana na siku za nyuma. Katika kesi hii, ushauri nasaha unaweza kusaidia kufunua shida na kushughulikiwa matumaini. Vyovyote vile, pande zote mbili zichukue muda wa mapumziko na kukaa chini kwa nia ya kuzungumza bila kuelekeza lawama. Mchungaji au mshauri wa Biblia anaweza kuwa msaada wa ajabu wakati wa mazungumzo haya. Lengo linapaswa kuwa kuelewa mtazamo wa mwenzi wa ndoa, hivyo wanandoa wanaweza kusonga pamoja katika mwelekeo sahihi na kuruhusu mabadiliko kuanza.

Uponyaji hauwezi kulazimishwa na unaweza kuchukua muda. Wakati huo, huo, msamaha ni amri ya haraka (Mathayo 6:14-15). Ikiwa pande zote mbili zinataka mema ya Mungu na ikiwa mchakato unafanywa kwa unyenyekevu na uaminifu, urafiki kmaili unawezekana tena. Wanandoa wanaoumia wanapaswa kujitolea wenyewe kwa muda katika Neno kila siku, kwa maombi, kwa utii kwa Mungu, na kwa kila mmoja wao. Kisha wanaweza kumwamini Bwana kwa uvumilivu kufanya kazi katika mioyo yao yote miwili na kuponya chochte kinachosababisha ukosefu wa ngono katika ndoa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Itikio la Mkristo linapaswa kuwa gani kwa ukosefu wa ngono katika ndoa (ndoa isiyo na ngono)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries