settings icon
share icon
Swali

Je! uhalali wa ndoa ni upi katika ulimwengu wa leo?

Jibu


“Ikiwa utaolewa, utajuta katika miaka mitano ya ndoa.” “Usifanye hivyo; mwanamume unayemuoa hatakuwa mwanaume yule yule unayemzika kwa sababu wanabadilika kadri muda unavyopita.” Maneno kama hayo ni ya kuhuzunisha na yanaenea katika ulimwengu wenye jazba uliojaa watu wanaotilia shaka ndoa, na vijana wengi wanasikitishwa na ukafiri huo. Huenda wengine hata wakaepuka kufuatia ndoa. Lakini kauli zilizo hapo juu ni usharui mbaya. Ndoa ni halali hii leo kama ilivyokuwa hapo mbeleni (Waebrania 13:4).

Nukuu za kejeli zilizo hapo juu zinashangaza katika ubinafsi wao wa asili. Ushauri wanaojumuisha ungefaa ikiwa tu ndoa ilikusudiwa kutosheleza tamaa za kibinafsi za mtu. Lakini hilo sio kusudi la ndoa.

Nadhiri ya ndoa si ahadi ya maisha yote ya kupendwa au kupokea upendo. Ndoa ni kiapo cha kutoa upendo. Ni ahadi ya kutoa upendo kwa maisha. Ni dhamira ya kuishi kwa faida ya mwingine, kusimama nyuma ya mwingine. Kutoa na kutoa na kutoa na kutoa, kisha kutoa zaidi-hata maisha yenyewe.

Kimsingi, wanadamu hawakuanzisha ndoa. Mungu ndiye alianzisha. Mungu alipowaumba wanadamu mwanamume na mwanamke na kuwaleta pamoja wenzi wa kwanza katika ndoa, Alikuwa na kusudi akilini. Kusidi la msingi zaidi lilikuwa kwamba ndoa ingezalisha watu wengi zaidi wanaobeba jina la Mungu, kuakisi sura Yake, na kuitiisha dunia (Mwanzo 1:26-28 na 2:22-24).

Zaidi ya hayo, ili kuakisi vizuri na kikamilifu sura ya Mungu, wanadamu lazima wawe na wanaume na wanawake (Mwanzo 1:27). Mwanaume peke yake sio mkamilifu; wala mwanamke. Kuakisi tabia ya Mungu katika mwanadamu kunahitaji jinsia zote—mwanamume na mwanamke kuunganishwa katika ndoa. Ndoa inapita furaha ya kimapenzi; inapita raha ya kujamiiana. Ahadi ya ndoa inahusu kuakisi kikamilifu tabia ya Mungu, umoja na ushirika. Hii inaeleza ni kwa nini mtume Paulo anafafanua ndoa ya Kikristo kwa maneno ya hali ya juu ya kiroho kama inavyopatikana katika Waefeso 5:22-33.

Msingi wa ndoa nzuri haupatakani katika kugundua mfano mzuri au shujaa wa ajabu. Wala hupatikana katika kutambua chaguo la Mungu lililotayarishwa la mwenzi wa maisha anayefaa zaidi—yule anayepatana zaidi na makusidi na matamanio ya Mungu—ndipo ndoa yenye kuridhisha zaidi hujengwa. Kwa hakika mapenzi yana nafasi yake na yatafurahiwa katika ndoa ya kimungu, lakini kama tunda tu la uhusiano wa ndani zaidi na wenye nguvu zaidi.

Naam, fungate itaisha, naam, wote mume na mke watathibitika kuwa tofauti kwa kadri kutoka kwa yale waliyoonyeshana walipokuwa wakichumbiana. Naam, mapema au baadaye wenzi wote wawili watakatishwa tamaa katika tabia fulani ya mwingine. Na, naam, majaribu yatakuja, kupima nguvu ya nadhiri zao. Lakini hakuna lolote kati ya hayo linalobadili ukweli kwamba Mungu alikuwa na wazo zuri alipoanzisha ndoa.

Kipengele kimoja ambacho wakosoaji wa ndoa huwa wanakosa ni imani. Ndoa na familia ni taasisi za Mungu kwa wanadamu. Ikiwa Mkristo kweli anatembea na Mungu, akimtakia Mungu yaliyo mema zaidi kwa mwenzi wake, akitaka kweli kuendeleza mpango wa Mungu kwa ajili yake mwenyewe, kwa ajili ya mwenzi wake wa ndoa, na kwa ajili ya ulimwengu, basi hataliacha wazo la ndoa. Sio juu ya kile tunachopata nje ya ndoa. Sio wakubwa wa ulimwengu huu wanaopata utimilifu, lakini watoaji, wale ambao kwa neema ya Mungu huiga kutao kwa kujitolea kwa Kristo, na hivyo kukua katika sura yake (Warumi 8:28-30; Waefeso 4:20-24). Ndoa nzuri itagharimu kila kitu tulicho nacho. Na, katika utoaji huo, tutapata maana ya juu zaidi ya maisha katika Kristo.

Hakuna lolote kati ya haya linalomaanisha kwamba kila muumini lazima aoe. Mungu anajua kwamba ni afadhali wengine wasifunge ndoa na kwamba hali fulani hufanya ndoa isitamanike. Tazama 1 Wakorintho 7. Kwa wale wanaofunga ndoa, ni muhimu kuwa na ufahamu wa kile ambacho Mungu anakusudia ndoa iwe. Hatupaswi kuruhusu uzoefu wa kusikitisha na uzembe wa wengine kutuzuia kumwamini Mungu kutupa kwa kweli ndoa zinazomwinua Yeye. Ndoa ya kiungu inaweza kutimiza makusudi Yake na kutoa nafasi kwa mume na mke kwa jina la Yesu Kristo.kubarikiana katika maisha

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! uhalali wa ndoa ni upi katika ulimwengu wa leo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries