settings icon
share icon
Swali

Ni siku gani ya sabato, Jumamosi au Jumapili? Wakristo wastahili kuitunza hii siku?

Jibu


Kila mara husemwa kuwa “Mungu ndiye alianzisha sabato katika shamba la Edeni” kwa sababu ya uhusiano kati ya Sabato na uumbaji katika Kutoka 20:11. ingawa starehe ya Mungu siku ya Sabato (Mwanzo 2:3) iliangazia sheria ya Sabato iliyokua inakuja, hakuna maelezo yoyote ya Bibilia juu ya Sabato kwa watoto wa Israeli kabla watoke Misri. Hakuna maandiko katika Bibilia au dondoo lolote linaloonyesha kuwa Adamu na Musa waliitunza Sabato.

Neno la Mungu laiweka wazi kuwa kuitunza Sabato ilikua ishara maalumu kati ya Mungu na Waisraeli: “Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli watishika sabato, kuiangalia sana hiyo sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika” (Kutoka 31: 16-16).

Katika Kumbukumbu La Torati 5, Musa anazirudia amri kumi kwa kizazi kingine cha Israeli. Hapa baada ya kuamrisha jinsi ya kuitunza sabato katika aya ya 12-14, Musa anatoa sababu ya sabato ambayo sabato ilipewa kwa taifa la Israeli: “Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na akuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA Mungu wako, alikuamuru uishike sabato” (Kumbukumbu La Torati 5:15).

Lengo la Mungu kupeana sabato kwa Waisraeli haikuwa kukumbuka uumbaji, bali waukumbuke utumwa wa Wamisri na kule kuokolewa na Bwana. Kumbuka yanayohitajika kwa kuitunza sabato: mtu aliyewekwa chini ya hiyo sheria hangeweza kutoka kwa boma yake (Kutoka 16:29), hangewakisha moto (Kutoka 35:3), angeruhusu mtu yeyote kufanya kazi (Kumbukumbu La Torati 5:14). Mtu mwenye angivunja shreria ya sabato angeuwawa (Kutoka 31:15; Hesabu 15:32-35).

Uchunganusi wa ukurasa wa Agano Jipya watuonyesha mambo mane muimu: 1) Popote Kristo alionekena baada ya kufufuka kwake na siku zimetajwa, kila wakati ni siku ya kwanza ya Juma (Mathayo 28:1,9, 10; Mariko 16:9; Luka 24:1,13,15; Yohana 20:19, 26). 2) Wakati pekee sabato imetajwa kutoka kwa kitabu cha Matendo ya Mitume hadi ufunuo ni kwa sababu ya lengo la uinjilisti kwa Wayahudi kwenye Masinagogi (Matendo Ya Mitume 13-18). Paulo aliandika, “Nilikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi” (1 Wakorintho 9:20). Paulo hakuenda kaitka Masinagogi kuwa na ushirika na kuwajenga waumini, bali alienda ili awathibitishie injili na kuwaokoa walikuwa wamepotea. 3) Mara moja Paulo anasema, “tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa” (Matendo Ya Mitume 18:6), sabato tena haitajwi kamwe. Na 4) Badala ya kupendekeza kuwa waitunze siku ya sabato, sehemu nyingine ya Agano Jipya iliyobaki yasema kinyume ( ikijumulisha sehemu ya tatu ilioachwa nche hapo juu, inapatika katika Wakolosai 2:16).

Kwa kuingalia hoja ya nne kwa makini, tutafumbua kwamba, hakuna jukumu lolote la kuitunza sabato kwa waumini wa Agano Jipya. Pia tutaonyesha kuwa dhana ya Jumapili “Sabato ya Wakristo” si ya kibibilia. Vile imejadiliwa hapo juu, hakuna wakati sabato imetajwa baada ya Paulo kuanza kuangazia Mataifa, “Basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Wakolosai 2:16-17). Sabato ya Kiyahudi ilifutiliwa msalabani hamali ambapo Kristo “Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki” (Wakolosai 2:14).

Wazo hili limerudiwa zaidi ya mara moja katika Agano Jipya: “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwinginie aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku huiadhimisha kwa Bwana” (Warumi 14:5-6a). “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika siku, na miezi, na nyaktati, na miaka” (Wagalatia 4:9-10).

Bali wengine wanadai kuwa agizo la Constantino katika mwaka wa 321 A.D (Baada ya Yesu kuzaliwa) ilibadilisha sabato kutoka Jumamosi hadi Jumapili. Ni siku gani kanisa la kwanza lilikutana kwa ibada? Bibilia haitaji mkusanyiko wowote wa sabato (Jumamosi) kwa waumini kwa minajili ya ushirika au ibada. Ingawa, kuna kurasa wazi zinazoitaja siku ya kwanza ya juma. Kwa mfano Matendo Ya Mitume 20:7 ambayo yasema, “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokutana ili kumega mkate.” Katika 1 Wakorintho 16:2 Paulo anawasihi Wakristo wa Korintho, “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadri ya kufanikiwa kwake.” Jinsi Paulo anayataja haya matoleo kuwa “huduma” katika 2 Wakorintho 9:12, haya matoleo lazima yamehuzishwa na ibada ya siku ya Jumapili ya Wakristo. Kiistoria siku ya Jumapili, bali si Jumamosi ilikuwa siku iliyokubalika kwa Wakristo katika kanisa na matukio yao yaweza kufuatwa hadi wakati wa kanisa la kwanza.

Sabato ilipeanwa kwa Waisraeli, si kanisa. Sabato bado ingali siku ya Jumamosi si Jumapili na haijawai badilishwa. Bali sabato ni sehemu ya sheria ya Agano La Kale na Wakristo wako huru kutoka kwa mkono wa sheria (Wagalatia 4:1-26; Warumi 6:14). Wakristo hawitakiwi kuitunza sabato hata kama iko siku ya Jumamosi au Jumapili. Siku ya kwanza ya juma, siku ya Bwana (Ufunuo 1:10) za sherekea kiumbe kipya Kristo aliyefufuka akiwa kiongozi wetu. Hatujaamrishwa kiufuata sheria ya Musa ya sabato ya kustarehe, bali tuko huru kumfuata Kristo aliyefufuka. Mtume Paulo alisema kwamba kila mkristo amue mweneyewe kama ataifuata sabato, “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe” (Warumi 14:5). Twastahili kumwabudu Mungu kila siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni siku gani ya sabato, Jumamosi au Jumapili? Wakristo wastahili kuitunza hii siku?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries