settings icon
share icon
Swali

Ni kanuni gani za kibiblia zinazopaswa kutumika kwa sherehe ya ndoa ya Kikristo?

Jibu


hutafautiana sana kutoka tamaduni hadi tamaduni. Sherehe za ndoa za Kikristo zinaweza kutofautiana katika mtindo, urefu wa sherehe, gharama, na vipengele na bado viwe vya kumheshimu Mungu. Vipengele ambavyo wanandoa huchagua kujumuisha katika sherehe si vya umuhimu mkubwa. Kilicho muhimu zaidi ni mioyo ya bi harusi na bwana harusi utayari wao wa kumweka Mungu kuwa kitovu cha maisha yao na familia. Kama viashiria vya ahadi hiyo, sherehe za ndoa za Kikristo mara nyingi hujumuisha yafuatayo:

1. Mahubiri mafupi ya kibiblia ya mchungaji anayeshikanisha ndoa

2) Kubadilishana nadhiri na pete kati ya bibi na bwana harusi

3) Maombo kwa wanandoa

4) Aina fulani ya kitendo cha ishara kinachowakilisha muungano wa watu wawili. Hii inaweza kuwa kuwasha mshumaa kwa pamoja, kuchanganya rangi mbili za mchanga katika chombo cha kumbukumbu, au njia nyingine yoyote ile ya ubunifu ambayo wanandoa wanaweza kueleza umoja wao.

Sherehe ya ndoa ya Kikristo inaweza hata kujumuisha mwaliko wa wageni kuitikia ujumbe wa wokovu.

Kanuni ya kibiblia ambayo ni muhimu ziadi katika sherehe ya ndoa ya Kikristo ni kuelewa ndoa ni nini haswa, na jinsi Mungu anavyoiona. Katika tamaduni fulani, ndoa inachukuliwa kuwa chaguo moja kati ya nyingi za kuanzisha familia, na itadumu ili mradi wanandoa watataka. Lakini kuishi pamoja bila kuoana ni dhambi kulingana na Maandiko na haipaswi kuzingatiwa kuwa chaguo kwa Wakristo (ona Waebrania 13:4). Kuelewa kusudi la ndoa kutawasaidia wanandoa kuchagua kumheshimu Mungu katika uhusiano wao na pia kutaathiri sherehe wanazobuni.

Ndoa ilikuwa wazo la Mungu, na Aliweka ufafanuzi wake na vigezo/mipaka. Katika bustani ya Edeni, Mungu aliumba mwanamke mmoja (Hawa) kwa ajili ya mwanamume mmoja (Adamu) akisema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa” (Mwanzo 2:18). Aliwaambia “zaeni mkaongezeke” (Mwanzo 1:22), amri ambayo inaweza tu kutiiwa katika muungano wa jinsia mbili tofauti. Yesu alisisitiza ukweli huu katika Agano Jipya alipowakumbusha wale waliotilia shaka kudumu kwa ndoa kwamba “tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Marko 10:6-9).

Kanuni kadhaa kuhusu ndoa ziko wazi kutoka kwa Maandiko:

1. Ndoa kama vile Mungu alivyoikusudia ni kati ya mume mmoja na mke mmoja kwa maisha yote (Mwanzo 2:18-22).
2. Ndoa ni muunganiko wa watu wawili tofauti kuwa chombo kipya, familia mpya (Mwanzo 2:23-24).
3. Ndoa inashuhudiwa na Mungu Mwenyewe anapofanya watu wawili kuwa mmoja (Malaki 2:13-15).
4. Talaka haikuwa chaguo katika mpango wa asili wa Mungu (Mathayo 19:7-10).
5. Ndoa kwa mtazamo mwingine ni uhusiano wa karibu, upendo wa Kristo na bibi arusi Wake, kanisa (Waefeso 5:31-32).

Wanandoa Wakristo wanapozingatia kanuni hizi, sherehe wanazopanga zinaweza kuwa zenye kupendeza, zenye maana, na za kumheshimu Mungu bila kugharamika sana. Ubadhirifu wa sherehe ya ndoa hauna uhusiano wowote na nguvu ya ndoa. Lakini, kanuni za kibiblia zinapotumika kwa sherehe ya ndoa ya Kikristo, kanuni hizo hufuata wanandoa katika maisha yao yote na kutoa msingi thabiti na wa kudumu maishani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kanuni gani za kibiblia zinazopaswa kutumika kwa sherehe ya ndoa ya Kikristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries