settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anawatuma watu kuzimu?

Jibu


Biblia inasema kwamba Mungu aliumba kuzimu kwa ajili ya Shetani na malaika waovu waliomwasi, lakini kuna watu kuzimu pia (Mathayo 25:41). Malaika na wanadamu wote wako kuzimu kwa sababu hiyo moja, dhambi (Warumi 6:23).

Kwa sababu Mungu ni mwenye haki kabisa na mkamilifu kimaadili (Zaburi 18:30), Yeye hutenda yaliyo sawa daima-hakuna “giza” ndani yake Mungu, wala hakuna hata chembe ndogo ya kutokamilika (1 Yohana 1:5). Mungu Mwenyewe ndiye kipimo cha kile kilicho sawa, kizuri na cha maadili. Mungu asingalikuwa kiwango cha ukamilifu wa maadili, viumbe vilivyombwa havingekuwa na chochote cha kujipima. Kwa maneno mengine, ikiwa Mungu ni mwadilifu kabisa, basi chochote kinachopungukiwa na ukamilifu uliosemwa ni dhambi, na kila mwanadamu ambaye amewahi kuishi tangu anguko la Adamu kutoka kwa neema amefanya dhambi (Warumi 3:23). Kwa sababu Adamu alifanya dhambi, wanadamu wote sasa wana asili ya dhambi (Warumi 5:12). Lakini watu hawaendi motoni kwa sababu ya dhambi ya Adamu; wanaenda kuzimu kwa sababu ya dhambi zao wenyewe, ambazo wanazichagua kwa hiari (Yakobo 1:13-16).

Kwa kuwa Mungu ni wa milele, habadiliki, na hana kikomo, na dhambo zote kimsingi ni dhidi ya Mungu. Mungu ameamuru adhabu ya haki kwa dhambi lazima pia iwe ya milele (Mathayo 25:46). Kuna kipengele kingine cha kuzingatia ambacho ni kwamba Mungu pia aliumba watu ili waishi milele. Kwa hiyo mtu anapomkosea mtu mwingine, mtu aliyekosewa pia amedhulimiwa milele.

Kwa hiyo, Mungu, ameona kwamba wote wanaotenda dhambi wataenda motoni kwa sababu wameshindwa kufikia kiwango chaeke cha haki; wamevunja Sheria yake ya ukamilifu wa kimaadili. Ikiwa Mungu hakuwapeleka watu kuzimu kwa kuvunja sheria zake, inaweza kusemwa kwamba Mungu si mwenye haki (Zaburi 7:11). Mfano mzuri ni mahakama ya sheria yenye hakimu na mvunja sheria. Hakimu mwadilifu atamtia katika hatia mtu ambaye amepatikana na hatia. Ikiwa hakimu huyo hangefuata haki kwa kosa hilo, hangekuwa hakimu mwadilifu (Kumbukumbu 32:4).

Hata hivyo, habari njema ni kwamba Mungu pia ni mwenye rehema. Katika rehema zake nyingi, alitengeneza njia kwa wenye dhambi kuepuka adhabu ya kuzimu kwa kuamini kazi ya upatanisho ya Mwanawe Yesu Kristo (Warumi 5:9). Kwa Wakristo, adhabu ya dhambi imeondolewa na kuwekwa juu ya Kristo msalabani (1 Petro 2: 24). Kwa sababu ya dhabihu ya Kristo, Mungu bado ni mwenye haki-dhambi inaadhibiwa-lakini pia ana huruma kwa wote wanaoamini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anawatuma watu kuzimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries