settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu ngono katika ndoa/ngono ya ndoa?

Jibu


Ngono iliundwa kuwa uzoefu wa kipekee wa kuwaunganisha mume na mke pamoja katika kile ambacho Biblia inakiita “mwili mmoja” umoja (Mathayo 19:6). Kwa kuwa Mungu alianzisha ngono, anapata kuweka vigezo vya matumizi yake, na Anaweka vigezo hivyo wazi kabisa katika Maandiko Matakatifu (Waebrania 13:4; 1 Wakorintho 6:18). Ngono iliundwa kwa ajili ya ndoa. Ngono yoyote nje ya mipaka hiyo ni dhambi. Na licha ya kile ambacho utamaduni wa sasa unatutaka tuamini, ngono ya ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke, si wanaume wawili au wanawake wawili. Baolojia rahisi huifanya iwe wazi kwamba miili ya wanaume na wanawake iliundwa ili kuingiana pamoja kwa njia ambayo fiziolojia ya jinsia moja haiwezi. Mungu anajua anachofanya. Kwa hiyo, acheni tuchunguze kile ambacho Biblia inasema kuhusu ngono katika ndoa.

Kwanza kabisa, ngono katika ndoa inapaswa kuwa utimilifu wa ahadi ya maisha, iliyotolewa na watu wawili. Katika nyakati za kale na katika tamaduni mbalimbali, sherehe za arusi mara nyingi zinazojumuishwa ni “sherehe ya kulala,” ambapo bibi na bwana wanarudi kwenye chumba cha kulala ili kukamilisha ndoa yao. Wangerudi kwenye karamu baadaye, na sherehe pamoja na marafiki na familia ingeendelea. Ndoa haikuzingatiwa kuwa kamili hadi bibi na bwana arusi walionana kimwili. Ingawa hili linaweza kuonekana kuwa gumu kidogo kulingana na viwango vytu vya kisasa, lakini linaonyesha thamani ambayo tamaduni nyingi huweka juu ya ubikira na ngono katika ndoa.

Kwa sababu msukumo wa ngono una nguvu sana, Biblia inahimiza ndoa ili kuepuka uasherati (1 Wakorintho 7:1-2). Ngono ya ndoa inapaswa kuwa ya pande zote na ya mara kwa mara ili mume na mke wasishawishike kufanya uzinzi (1 Wakorintho 7:5). Biblia inatoa maagizo ya kina kuhusu ndoa, kujamiiana, na talaka katika 1 Wakorintho 7. Miili ya mume na mke ni ya kila mmoja. Mstari wa 4 unasema, “Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.” Kumpa huku kwa mwili yule tuliyejitolea kunapaswa kuondoa uwezekano wowote wa mahusiano nje ya ndoa. Tunapoelewa kwamba miili yetu si yetu wenyewe, kwamba imeahidiwa kwa mwenzi, tunaweza kufunga mlango kwa mawazo yoyote ya kumkopesha mtu mwingine.

Ndoa iliundwa na Mungu kama picha ya uhusiano wa agano anaotaka nasi (2 Wakorintho 11:2). Mungu anaweka umuhimu mkubwa juu ya kujamiiana kwa mwanadamu kwa sababu ngono ya ndoa ndio uhusiano wa karibu sana ambao wanadmau wawili wanaweza kuwa nao. Pia ni picha ya ukaribu ambayo Mungu alituumba ili tufurahie pamoja Naye. Katika ngono ya ndoa, kuna utaoji wa mwili, na katika uhusiano wetu wa kiroho na Mungu, tunapaswa kutoa miili yetu kama dhabihu iliyo hai (Warumi 12:1-2). Tendo la ngono ni utimilifu wa agano lililofanywa kati ya mwanamume na mwanamke. Maagano kila mara yalitimizwa kwa kumwaga damu (Kutoka 24:8), na kwa kawaida, damu humwagika wakati ubikira unapopotea. Mungu alipofanya agano lake nasi, damu ya Kristo ilimwagika (Waebrania 13:20). Ngono ya ndoa ni zaidi ya njia ya uzazi na njia salama ya misukumo yetu ya ngono. Ni takatifu kwa Mungu kwa sababu inaashiria ukaribu wa roho safi anayotaka kushiriki nasi. Kufanya ngono kama shughuli ya kawaida ni kuondoa maana yake halisi.

Ngono ya ndoa ndiyo njia pekee ya kuonyesha ngono iliyokubaliwa na Muumba wetu. Inapaswa kuonwa kuwa zawadi takatifu na kufurahiwa na mume na mke. Tunapaswa kulinda mioyo na macho yetu dhidi ya vishawishi vyovyote vya nje vinavyojaribu kuchafua au kuiba urafiki wa kingono. Ponografia, ngon nje ya dnoa, talaka, na uasherati zote hutupotezea urembo na thamni ambayo Mungu alianzisha katika tendo la ngono. Hatuwezi kupata usoefu wa kujamiiana wote ambo Mungu alikusudia isipokuwa tuhifadhi shughuli zote za ngono kwa ajili ya ndoa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu ngono katika ndoa/ngono ya ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries