settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu ni wa kiume au kike?

Jibu


Katika kuchunguza maandiko, mambo mawili huwa wazi. Kwanza, Mungu ni Roho na hana hamiliki tabia ya binadamu au upungufu. Pili, ushahidi wote uliomo katika maandiko unakubaliana kuwa Mungu alijidhihirisha kwa mwanadamu katika umbo la kiume. Kwa kuanzia, asili ya kweli ya Mungu inahitaji kueleweka. Mungu ni Mtu, na ni wazi, kwa sababu Mungu ameonyesha sifa zote za utu: Mungu ana akili, mapenzi, na hisia. Mungu huwasiliana na Yeye ana mahusiano, na vitendo viake kibinafsi ni ushahidi katika maandiko.

Kama vile Yohana 4:24 inasema, “Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na katika kweli”. Jinsi Mungu ni wa kiroho, yeye hamiliki sifa za kimwili za binadamu. Hata hivyo, lugha wakati mwingine ya mfano hutumika katika maandiko ikimpa Mungu tabia ya binadamu ili iwe rahisi kumwelewa Mungu. Kazi hii ya tabia ya binadamu kuelezea Mungu inaitwa “kimajazi" kimajazi njia tu ya Mungu (kuwa kiroho) huwasilisha ukweli kuhusu asili yake kwa binadamu, viumbe wa kimwili. Kwa sababu ubinadamu wa mwili, tumepungukiwa katika kuelewa yale mambo ambayo ni zaidi ya ulimwengu wa mwili. Kwa hivyo, kimajazi katika maandiko inatusaidia kuelewa Mungu ni nani.

Baadhi ya ugumu huja katika kuchunguza ukweli kwamba binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Mwanzo 1:26-27 inasema, “Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, na watawale samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya nchi yote, na juu ya viumbe wote wanaotembea ardhini. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”

Wote wawili mwanamume na mwanamke wameumbwa kwa mfano wa Mungu, kwa kuwa wao ni zaidi ya ubunifu mwingine wote, wao kuwa kama Mungu, watakua na akili, mapenzi, hisia, na uwezo wa maadili. Wanyama hawana uwezo wa maadili na hawana sehemu yoyote isiyo haribika kama binadamu. Mfano wa Mungu ni sehemu ya kiroho ambayo ni binadamu peke yake anayo. Mungu aliumba binadamu ili awe na uhusiano pamoja naye. Binadamu ndiye kiumbe pkee iliyoumbwa kwa ajili hiyo.

Alisema, mwanamume na mwanamke ndio wameumbwa tu baada ya mfano wa Mungu, hao sio “nakala” ndogondogo ya Mungu. Ukweli kwamba kuna wanaume na wanawake hauhitaji Mungu kuwa na sifa za kiume na kike. Kumbuka, kuwa katika mfano wa Mungu hauna uhusiano wowote wa sifa za kimwili.

Tunajua kwamba Mungu ni kiumbe wa kiroho na hamili wamiliki wala sifa ya kimwili. Hii haizui Mungu, hata hivyo, jinsi Mungu anaweza kuchagua kudhihirisha mwenyewe kwa binadamu. Bibilia ina kila ufunuo wa Mungu ambao Mungu alimpa binadamu juu yake mwenyewe, na hivyo hilo ndilo lengo na chanzo cha habari juu ya Mungu. Kwa kuangalia kile maandiko hutuambia, kuna uchunguzi kadhaa wa ushahidi kuhusu namna ambayo Mungu alijidhihirisha kwa binadamu.

Biblia ina takriban 170 marejeo ya Mungu kama “Baba.” Kwa umuhimu, mtu hawezi kuwa baba isipokuwa yeye ni wa kiume. Kama Mungu aliamua kujidhirihisha wazi kwa mwanadamu katika umbo la kike, kisha neno “mama” lingeonekana katika maeneo hayo, si “baba” Katika Agano la Kale na Jipya, majina ya kiume yametumiwa tena na tena katika kumbukumbu ya Mungu.

Yesu Kristo alimtaja Mungu kama Baba mara kadhaa na katika kesi nyingine limetumika kwa kiume katika kumbukumbu ya Mungu. Ni katika Injili peke yake, Kristo anatumia neno “Baba” akimaanisha moja kwa moja Mungu karibu mara 160. Kauli ya Kristo katika Yohana 10:30: “Mimi na Baba yangu tu kitu kimoja.” Ni wazi kwamba, Yesu Kristo alikuja katika hali ya binadamu na kufa juu ya msalaba kama malipo ya dhambi ya dunia. Kama Mungu Baba, Yesu alidhhirishwa wazi kwa binadamu katika umbo la kiume. Bibilia imenakili sehemu mbalimbali matukio mengine ambapo Kristo inatumia majina ya kiume na nomino katika kumrejelea ya Mungu.

Nyaraka za Agano Jipya (kutoka Matendo hadi Ufunuo) pia zina mistari karibu 900 ambapo neno Mungu-nomino katika Kigiriki- limetumika katika kumrejelea Mungu moja kwa moja. Kwa ajili ya kumbukumbu isitoshe Mungu katika maandiko, ni wazi mfano thabiti ya kuwa anajulikana kwa, majina ya kiume, na majina, ya nomino. Ingawa Mungu si kama mwanaume, Yeye alichagua aina jinsia ya kiume ili kujidhihirisha kwa binadamu. Kadhalika, Yesu Kristo, ambaye daima anajulikana kwa majina ya kiume, majina, ya nomino, alichukua umbo la kiume wakati alitembea juu ya nchi. Manabii wa Agano la Kale na mitume wa Agano Jipya warejelea Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo kwa majina ya kiume na vyeo. Mungu alichagua kuwa wazi katika umbo hili ili iwe rahisi zaidi kwa mtu kufahamu yeye ni nani. Wakati Mungu hufanya posho ili kutusaidia kumwelewa, ni muhimu tusijaribu “;kumlazimisha Mungu kuingia ndani ya sanduku” ili kuzungumza, kwa kumwekea upunguvu ambao si sahihi na asili yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu ni wa kiume au kike?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries