settings icon
share icon
Swali

Je! Mwanzo 2:18 inamaanisha nini kuhusiana na uhusiano wa kati ya mke na mume?

Jibu


Mwanzo 2:18 inasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” Hii inamaanisha nini?

Inapendeza kuona kwamba sehemu pekee ya uumbaji wa Mungu inayotangazwa kuwa “si vyema” inahusu hali ya upweke ya Adamu. Mungu alisema kuwa si vyema mtu awe peke yake (Mwanzo 2:18). Mwanadamu, kwa asili, ni kiumbe wa kijamii; Mungu alituumba na hitaji la uhusiano. Na, bila shaka, mtu pekee yake hawezi kueneza kizazi. Adamu peke yake alikuwa hajakamilika. Ndiyo sababu Mungu aliumba Hawa kuwa “msaidizi” anayefaa: ili kumkamilisha Adamu, kuandaa jamii kwa ajili yake, na kumwezesha kuzaa watoto. Hawa ndiye hasa Adamu alihitaji —msaidizi aliyemfaa.

Je, hii ina maana kwamba kila mwanamume lazima awe na mke, msaidizi wa kumkamilisha? Hapana. Kwa hakika, mtume Paulo alisema kwamba useja ni jambo jema kwa mtumishi wa Mungu (1 Wakorintho 7:7-9). Je, hii inamaanisha kuwa mwanamke lazima awe mke na mkamilishaji wa mwanaume? La. Sio kila mwanamke anataka kuolewa au kuongozwa kwenye ndoa. Hata hivyo, kifungu cha Mwanzo kinaweka kiwango kwa watu wengi katika mazingira mengi. Mke ndiye msaidizi anayefaa kwa mumewe.

Kwa hiyo inamaanisha nini hasa kuwa msaidizi anayefaa? Jambo kuu ni neno anayefaa. Mke anayefaa anapatana na mume wake katika mambo mengi—kimwili, kiakili, kihisia-moyo, na kiroho. Hii haimaanishi kwamba mwanamume na mwanamke ni sawa katika kila kitu, kwamba wanalingana kwa maelewano. Wanakamilishana. Kitufe cha B kwenye piano si sawa na G, lakini kwa pamoja hufanya sauti ya usawa. Vile vile, msaidizi anayefaa kwa mume ni mke aliye tofauti naye, lakini anayemfaa vizuri, anayemkamilisha kwa kila njia na anayeleta maelewano, sio mafarakano, kwenye uhusiano.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mwanzo 2:18 inamaanisha nini kuhusiana na uhusiano wa kati ya mke na mume?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries