settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu aliruhusu mitala / zaidi ya mke, mume mmoja katika Biblia?

Jibu


Suala la mitala ni mojawapo la kuvutia kwa kuwa watu wengi hii leo hutizama mitala kama ukosefu wa maadili huku hamna mahali Biblia inalaani. Mara ya kwanza ya mitala / kuwa na mke,mume zaidi ya mmoja katika Biblia ni ile ya Lameki katika Mwanzo 4:19 "Lameki alioa wanawake wawili" Watu wengi maarufu katika Agano la Kale walikuwa mitala. Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Sulemani, na wengine, wote walikuwa na wake wengi. Katika 2 Samweli 12:8, Mungu, akizungumza kupitia ya nabii Nathani, alisema kwamba kama wake na mahawara wa Daudi hawakuwa wa kutosha, naye angempa Daudi zaidi. Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300 (kimsingi wake wa hali ya chini), kulingana na 1 Wafalme 11:3. Tunapaswa kufanya nini na matukio haya ya mitala katika Agano la Kale? Kuna maswali matatu yanafaa kujibiwa: 1) Kwa nini Mungu aliruhusu mitala katika Agano la Kale? 2) Mungu anaionaje mitala leo hii? 3) Kwa nini alifanya ubadilisho?

1) Kwa nini Mungu aliruhusu mitala katika Agano la Kale? Biblia haisemi hasa ni kwa nini Mungu aliruhusu mitala. Tunapo kisia kimya cha Mungu, kuna mambo chache muhimu ya kuzingatia. Kwanza, kumekuwa na wanawake zaidi katika dunia kuliko wanaume. Takwimu sasa inaonyesha kwamba takriban asilimia 50.5 ya idadi ya watu duniani ni wanawake, na wanaume kuwa asilimia 49.5. Ukichukulia asilimia hiyo katika nyakati za zamani, na uongeze mara nyingi mamilioni ya watu, kutakuwa na mamia ya maelfu zaidi ya wanawake kuliko wanaume. Pili, vita katika nyakati za kale vilikuwa hasa vya kikatili, kwa kiwango cha utasa. Hii itakuwa imesababisha asilimia hata zaidi ya wanawake kwa wanaume. Tatu, kutokana na jamii ya mfumo wa udume, kwa karibu sana ni jambo lisilowezekana kwa mwanamke ambaye hajaolewa kujikimu mwenyewe. Wanawake mara nyingi hawakuwa wansomeshwa na kufunzwa zanaa. Wanawake hutegemea baba zao, ndugu zao, na waume kwa ajili ya kujikimu na ulinzi. Wanawake ambao hawajaolewa mara nyingi walilazimika kuingia katika ukahaba na utumwa. Tofauti kubwa kati ya idadi ya wanawake na wanaume ingeacha wengi, wanawake wengi katika hali mbaya.

Kwa hiyo, inaonekana kwamba Mungu aliweza kuruhusiwa mitala kulinda na kukimu wanawake ambao hawakuweza kupata mume kwa vyovyote vile. Mume angeweza kuchukua wake wengi na kutumika kama mtuzi na mlinzi wao wote. Huku ikiwa dhahiri kuwa si bora, kuishi katika kaya wake wengi ni bora zaidi kuliko kunyume: ukahaba, utumwa, au njaa. Mbali na ulinzi / utunzi, mitala iliwezesha upanuzi wa jamii kwa kasi zaidi, kutimiza amri ya Mungu ya "Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake" (Mwanzo 9:7). Wanaume wana uwezo wa kuwatia mimba wanawake wengi katika kipindi kimoja, na kusababisha ubinadamu kukua kwa kasi zaidi kuliko kama kila mume alikuwa tu anazalisha mtoto mmoja kila mwaka.

2) Mungu anaionaje mitala hii leo? Hata wakati tunaruhusu ndoa za mitala, Biblia inatoa ndoa ya mke mmoja kama mpango ambao unafana kwa karibu zaidi na ule bora wa Mungu kwa ajili ya ndoa. Biblia inasema kwamba nia ya awali ya Mungu ilikuwa kwa mtu mmoja kuolewa na mwanamke mmoja tu: "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, nao watkuwa mwili mmoja" (Mwanzo 2:24). Huku Mwanzo 2:24 ikielezea ndoa ni nini, kuliko jinsi watu wengi wanahusika, matumizi thabiti ya umoja ukumbukwe. Katika Kumbukumbu la Torati 17:14-20, yatafusiriwa kuwa Mungu kuwa wafalme walistahili kusidisha (au farasi au dhahabu). Huku hii haiwezi kutafsiriwa kama amri ya kuwa wafalme lazima awe na mke mmoja, inaweza kueleweka ikitangaza kwamba kuwa na wake wengi husababisha matatizo. Hii inaweza kuonekana wazi katika maisha ya Sulemani (1 Wafalme 11:3-4).

Katika Agano Jipya, 1 Timotheo 3:2, 12 na Tito 1:6 zinasungumzia "mume wa mke mmoja" katika orodha ya sifa za uongozi wa kiroho. Kuna baadhi ya mjadala kama vile ni nini hasa maana ya himizo hili. Kifungu kinaweza kuwa na maana ya kawaida kuwa "mume mke moja." Hata kama msemo huu unarejelea mtala au sio, kwa vyovyote vile Kwame hamna njia mtala anaweza chukuliwa "mume wa mke mmoja." Wakati sifa hizi ni mahsusi kwa ajili ya nafasi za uongozi wa kiroho, wanapaswa tumika sawia kwa Wakristo wote. Je, si Wakristo wote hawaswi kuwa "zaidi ya aibu ... kiasi, nidhamu, heshima, ukarimu, na uwezo wa kufundisha, si mlevi, wala mgomvi bali awe mpole, apendaye, si mpenda fedha" (1 Timotheo 3:2 -4)? Kama tumeitwa kuwa watakatifu (1 Petro 1:16), na kama viwango hivi ni vitakatifu kwa wazee na mashemasi, basi ni takatifu kwa wote.

Waefeso 5:22-33 inazungumzia uhusiano kati ya waume na wake. Wakati inarejelea mume (umoja), daima pia inarjelea mke (umoja). "Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe [umoja] ... Yeye ambaye ampendaye mke wake [umoja] anaupenda mwili wake mwenyewe. Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama ataungana na mke wake [umoja], nao wawili watakuwa mwili mmoja .... Kila mmoja wenu pia lazima ampende mkewe [umoja] vile anavyojipenda mwenyewe, na mke [umoja] lazima kuheshimu mumewe [umoja]." Huku kukiwa na kifungu sawia Wakolosai 3:18-19, inarejelea waume na wake kwa wingi, ni wazi kwamba Paulo anawasunguziaa Waumini wote wa Kolosai waume na wake, hasemia kwamba mume anaweza kuwa na wake wengi. Kwa ulinganisho, Waefeso 5:22-33 hasa inaelezea uhusiano wa ndoa. Kama mitala ilikuwa halali, mfano mzima wa uhusiano wa Kristo na mwili wake (kanisa) na uhusiano wa mume na mke ni totauti.

3) Ni kwa ilibadilika? Sio kuwa Mungu alikataa kile Yeye alikuwa amekiruhusu awali kama vile ilivyo Mungu anarejesha ndoa katika mpango wake wa awali. Tukirudi nyuma kwa Adamu na Hawa, ndoa za mitala haikuwa dhamira ya awali ya Mungu. Mungu anaonekana kuruhusiwa mitala ili attatue tatizo, lakini si bora. Katika jamii nyingi za kisasa, hamna kabisa haja ya mitala. Katika tamaduni nyingi hii leo, wanawake ni uwezo wa kujikimu na kujitunza na kuondoa "chanya" ya nyanja ya mitala. Zaidi ya hayo, mataifa ya kisasa yamefutilia mbali mitala. Kwa mujibu wa Warumi 13:1-7, tunapasw kutii sheria ya serikali ambayo imeundwa. Wakati pekee ambao tunaruhusiwa kuasi sharia kimaandiko ni ikiwa sheria inapingana na amri za Mungu (Matendo 5:29). Tangu ni Mungu aliruhusu mitala, na haiamrishi, sheria ya inayozuia mitala lazima izingatiwe.

Je, kuna baadhi ya matukio ambayo posho kwa ajili ya mitala bado itatumika hii leo? Labda, lakini itakuwa bahati mbaya kwamba hakutakuwa na uwezekano mwingine wa suluhizo. Kutokana na nyanja ya "mwili mmoja" ya ndoa, haja ya umoja na maelewano katika ndoa, na ukosefu wa haja yoyote halisi kwa ndoa za mitala, ni imani yetu dhabiti kwamba mitala haina heshima ya Mungu na si mfumoi wake kwa ajili ya ndoa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu aliruhusu mitala / zaidi ya mke, mume mmoja katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries