settings icon
share icon
Swali

Melkizedeki alikuwa nani?

Jibu


Melkizedeki, ambaye jina lake linamaanisha "mfalme wa haki," alikuwa mfalme wa Salemu (Yerusalemu) na kuhani mkuu zaidi wa Mungu (Mwanzo 14: 18-20; Zaburi 110: 4, Waebrania 5: 6-11, 6: 20-7: 28). Melkizedeki huonekana ghafla na kupotea katika kitabu cha Mwanzo ni ajabu kwa kiasi fulani. Melkizedeki na Ibrahimu walikutana kwanza baada ya Ibrahimu kushindwa kwa Kedorlaoma na washirika wake watatu. Melkizedeki iliwasilisha mkate na mvinyo kwa Ibrahimu na watu wake walokuwa wamechoka, kwa kuonyesha urafiki. Yeye alitawaza baraka kwa Ibrahimu kwa jina la El Elyon ("Mungu aliye juu zaidi") na kumsifu Mungu kwa kumpa Abraham ushindi katika vita (Mwanzo 14: 18-20).

Ibraham alimpokeza Melkizedeki na zaka ( fungu la kumi) ya vitu vyote alivyokuwa amesanya. Kwa kitendo hiki Ibraham alionyesha kuwa alitambua Melkizedeki kama kuhani ambaye nafasi yake ya kiroho ilikuwa juu kuliko yake.

Katika Zaburi 110, zaburi ya kimasihi iliyoandikwa na Daudi (Mathayo 22:43), Melkizedeki ametolewa kama aina nyingine ya Kristo. Mada hii imerudiwa katika kitabu cha Waebrania, ambapo Melkizedeki na Kristo wote wamechukuliwa kuwa wafalme wa haki na amani.Kwa kudondoa Melkizedeki na ukuhani wake wa kipekee kama aina, mwandishi anaonyesha kwamba ukuhani mpya wa Kristo ni bora kuliko mpangilio wa zamani wa Walawi na ukuhani wa Haruni (Waebrania 7: 1-10).

Baadhi hupendekeza kwamba Melkizedeki alikuwa amepata mwili ulionekana kama Yesu Kristo, au Kristofani . Hii ni nadharia inayowezekana, ikikumbukwa kwamba Ibrahimu alikuwa amepata ziara kama hizo hapo awali. Chukulia Mwanzo 17 ambapo Ibrahimu alimwona na kuongea na Bwana (El Shaddai) katika umbo la mtu.

Waebrania 6:20 inasema, "alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki." Tamko kwa mfano kwa kawaida laweza kuonyesha urithi wa kuhani wanaoshikilia ofisi. Hakuna waliotajwa kamwe, hata hivyo, katika kipindi cha muda mrefu kutoka Melkizedeki hadi kwa Kristo, kioja kinachoweza kusuruhishwa kwa kuchukulia kwamba Melkizedeki na Kristo kweli ni mtu mmoja. Hivyo "mfano wa" umekabidhiwa ndani yake na kwake pekee milele.

Waebrania 7: 3 inasema kuwa ”hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu; huyo adumu kuhani milele.”Swali ni iwapo mwandishi wa waebrania anamaanisha hii halisi au kitamathali.

Kama maelezo katika Waebrania ni halisi, basi ni vigumu kweli kuona jinsi itakavyotekelezwa kamili kwa mtu yeyote ila Bwana Yesu Kristo. Hakuna mfalme wa duniani "atakayebakia kuwa kuhani milele, "na hakuna binadamu wa kawaida“ ambaye hana baba wala mama.” Kama Mwanzo 14 inaelezea kuhusu imani ya kumufahamu Mungu, basi Mungu Mwana alikuja kumpa Ibrahimu baraka zake (Mwanzo 14: 17-19),akionekana kama Mfalme wa Haki (Ufunuo 19: 11,16), Mfalme wa Amani (Isaya 9: 6), na mpatanishi kati ya Mungu na binadamu (1 Timotheo 2: 5).

Kama maelezo ya Melkizedeki ni mfano, basi maelezo ya kutokuwa na nasaba/kisasi, hakuna mwanzo au mwisho, na huduma isiyo na mwisho ni tu kauli inayotia mkazo asili ya kiajabu ya mtu ambaye alikutana na Ibrahimu. Katika kesi hii, kimya katika maelezo ya Mwanzo kuhusu maelezo haya yana kusudi yanahudumu bora kwa kuunganisha Melkizedeki na Kristo.

Je, Melkizedeki na Yesu ni mtu mmoja? Kesi inaweza kufanywa kwa njia yoyote. Kwa uchache sana, Melkizedeki ni aina ya Kristo, anayeonyesha huduma ya Bwana kabla yake. Lakini pia inawezekana kwamba Ibrahimu, baada ya vita vyake vya kuchosha, alikutana na kumpa heshima Bwana Yesu mwenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Melkizedeki alikuwa nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries