settings icon
share icon
Swali

Mtazamo wa Kikristo wa mapenzi unapaswa kuwa namna gani?

Jibu


Neno mapenzi linatumika kuelezea mitindo ya fasihi, hali, na lugha fulani, kama vile kifaransa na Kiitaliano. Lakini, kwa madhumini ya makala hii, neno mapenzi litahusu tu msisimko wa kihisia au mvuto ambao mtu fulani au hali fulani huleta kwa mwingine. Aina hiyo ya mapenzi ni mada maarufu katika tamaduni nyingi. Muziki, filamu, michezo ya kuigiza na vitabu hutumia kuvutiwa kwetu na upendo wa kimahaba na maonyesho yake yanayoonekana kutokuwa na mwisho. Katika mtazamo wa ulimwengu wa Kikristo, je, mapenzi ni mazuri au mabaya au ni kati ya hizo mbili?

Biblia imeitwa barua ya upendo ya Mungu kwa wanadamu. Ingawa ina taswira kali na maonyo kuhusu hukumu ya Mungu, Biblia pia imejaa maonyesho ya ubunifu ya upendo kati ya wanadamu na Mungu (Zaburi 42:1-2; Yeremia 31:3). Lakini upendo na mapenzi, ingawa yanaingiliana, hayafanani. Tunaweza kuwa na mahaba bila upendo wa kweli, na tunaweza kupenda bila kuhisi mapenzi. Ingawa vifungu kama vile Sefania 3:17 vinaelezea upendo wa kihisia wa Mungu kwa walio Wake, vifungu kama vile 1 Wakorintho 13:4-8 vinaeleza kwa undani sifa za upendo ambazo hazina uhusiano wowote na hisia za mahaba. Yesu alisema, “Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yohana 15:13). Kufa kifo cha uchungu msalabani kwa ajili ya wenye dhambi wasio na shukrani haikuwa mahaba kwa njia yoyote, lakini ilikuwa dhihirisho kuu la upendo (1 Yohana 4:9-10).

Wimbo Ulio Bora ni kitabu kilichojaa maonyesho ya mahaba ya upendo kati ya bibi na bwana. Kwa sababu Mungu alitia ndani kitabu hiki katika orodha ya Biblia ya Neno Lake liloongozwa na roho, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba mapenzi yanakubalika na hata kushangiliwa na Muumba wetu. Mapenzi katika muktadha wa uhusiano safi na wa kujitolea yanaweza kuimarisha uhusiano huo na kuongeza furaha ya upendo wa ndoa jinsi Mungu alivyokusudia.

Hata hivyo, mapenzi kwa ajili ya mahaba yanaweza kuharibu. Mapenzi mengi huanza na hisia yakupendeza ya “kumpenda mtu”, ambayo inaweza kutia jazba. Kitendo cha “kumpenda mtu” hutoa kemikali nyingi katika ubongo sawa na uzoefu wa matumizi ya madawa ya kulevya. Ubongo umejaa adrenalini (kichocheo mwilini), dopamine na serotonini (kemikali za kujihisi vizuri), ambazo hutufanya tutake kurudi kwenye chanzo cha hisia hiyo. Lakini, kwa sababu ya mwitikio wa ubongo wetu, mapenzi yanaweza kuwa uraibu. Kusherehekea “ponografia ya hisia” kama vile riwaya za mapenzi, filamu za mapenzi, na vipindi vya runinga vinavyohusu ngono hutuweka katika matarajio yasiyo halisi katika mahusiano yetu halisi.

Watafiti wanakadiria kwamba ubongo wa mwanadamu unaweza tu kudumisha hisia hizo kali za “mapenzi” kwa muda usiozidi miaka miwili. Kwa hakika, wanandoa wamefanya kazi ya kuimarisha upendo wao na kujitolea wakati huo ili, wakati hisia kali za kuwa “katika upendo” zinapungua, upendo wa kina huchukua nafasi yake. Hata hivyo, kwa wale “waraibu” wa mahaba, hali hii ya kupungua kwa hisia inaashiria kwamba ni wakati wa kutafuta mtu mwingine ambaye atasababisha furaha kama hiyo. Baadhi ya watu walio na “uraibu wa uhusiano” wanaweza, kwa kweli, kuwa waraibu wa hisia zinazoletwa na “kumpenda mtu.” Kwa hivyo, wanajaribu kuunda tena hisia hiyo tena na tena.

Tunapotilia maelezo hayo maanani, ni rahisi kuona kwa nini mapenzi na mahaba sio kitu kimoja. Biblia inatoa mifano kadhaa ya wenzi wa ndoa ambao walipata upendo wa kimahaba na matokeo ya mapenzi hayo. Mwanzo 29 inasimulia hadithi ya Yakobo kumpenda Raheli. Alikuwa tayari kumfanyia kazi baba mkwe kwa miaka saba ili amwoe. Mstari wa 20 unasema kwamba miaka hiyo saba ilikuwa “kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli.” Ingawa hadithi ya Yakobo iliendelea kwa udanganyifu, huzuni, na kufadhaika kwa kila mtu, mapenzi yake kwa Raheli hayashutumiwi katika Maandiko. Hata hivyo, mapenzi yalimtia Samsoni matatizoni aliporuhusu hisia zake zimtawale. Waamuzi 14 yanaelezea mwanzo wa kuanguka kwa Samsoni wakati aliruhusu mapenzi kuamuru maamuzi yake badala ya kufuata mwongozo wa Bwana.

Mapenzi yanaweza kuwa mabaya au mazuri kulingana na ikiwa tunaruhusu hisia hizo zitawale maisha yetu. Tunapofuatilia hisia zetu, tunaweza kuingia katika matatizo ya kiadili na matazi katika ndoa. Yeremia 17:9 inasema, “Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua?” Msemo maarufu “fuata moyo wako” ni ushauri mbaya. Tunapofuata tamaa za mioyo yetu, tunaongozwa kwa urahisi katika udanganyifu, dhambi, na majuto. Badala ya kutafuta mahaba, tunapaswa kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu katika mahusiano yetu. Ni jambo la hekima kufuata upendo sikuzote (1 Wakorintho 14:1). Kisha, tunapotafuta kuonyesha upendo, mtu fulani wa kipekee anapojitokeza, mapenzi ya kimungu yanaweza kuwa zawadi kutoka kwa Baba yetu wa mbinguni (Yakobo 1:17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mtazamo wa Kikristo wa mapenzi unapaswa kuwa namna gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries