settings icon
share icon
Swali

Majukumu ya mume na mke ni gani katika familia?

Jibu


Ingawa wanaume na wanawake wako sawa katika uhusiano na Kristo, maandiko yanatoa majukumu maalum kwa kila mmoja katika ndoa. Mume anapaswa kuchukua uongozi katika boma (1 Wakorintho 11:3, Waefeso 5:23). Uongozi huu usiwe wa kihimla, kukandamisa, au shupavu kwa mke, lakini lazima iwe kwa mujibu wa mfano wa Kristo kuongoza kanisa. "Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neon" (Waefeso 5:25-26). Kristo alivyolipenda kanisa (watu wake) na huruma, rehema, msamaha, heshima, na kutokuwa na ubinafsi. Kwa njia hiyo waume wanapaswa kuwapenda wake zao.

Wake wanapaswa kunyenyekea kwa mamlaka ya waume zao. "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili wake. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo" (Waefeso 5:22-24). Ingawa wanawake wanapaswa kunyenyekea kwa waume zao, Biblia pia anawaambia wanaume mara kadhaa jinsi wanatakiwa kuwafanyia wake zao. Mume hapaswi kuchukua nafasi ya kiihimla, lakini wanapaswa kuonyesha heshima kwa mke wake na maoni yake. Kwa kweli, Waefeso 5:28-29 anawahimiza watu kuwapenda wake zao katika njia sawa wanavyoipenda miili yao wenyewe, kuwalisha na kuwatunza. Upendo wa mume kwa mke wake unapaswa kuwa sawa na upendo wa Kristo kwa mwili wake, kanisa.

"Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi Waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao "(Wakolosai 3:18-19). "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpamke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe" (1 Petro 3: 7). Kutokana na mistari hii tunaona kwamba upendo na heshima ni sifa ya majukumu ya waume wote na wake. Kama haya yapo katika ndoa, basi mamlaka, uongozi, upendo, na kunyenyekea hakutakuwa na tatizo kwa mpenzi yeyote.

Kuhusiana na suala la mgao wa majukumu katika boma, Biblia inawaamuru waume kukimu familia zao. Hii ina maana kuwa anafanya kazi na kupata fedha za kutosha kukimu mahitaji yote ya maisha kwa mke na watoto wake. Kwa kushindwa kufanya hivyo ina madhara maalum ya kiroho. "Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa numbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini" (1 Timotheo 5:8). Hivyo, mume ambaye hafanyi juhudi za kukimu mahitaji ya familia yake haiwezi kujiita Mkristo halisi. Hii haimaanishi kwamba mke hawezi eza katika kusaidia familia Mithali 31 inaonyesha kuwa mke mcha Mungu anaweza hakika kufanya hivyo-lakini kukimi familia si hasa wajibu wake; ni wa mume wake. Wakati mume anasaidia kutayarisha watoto na kufanya kazi za nyumbani (hivyo kutimiza wajibu wake wa kumpenda mke wake), Mithali 31 pia inaweka wazi kwamba nyumbani ni eneo kimsingi mwanamke ushawishi na wajibu. Hata kama yeye ni atalazimika kulala akiwa amechelewa na kuamka mapema, familia yake imetunzwa vyema. Haya sio maisha rahisi kwa wanawake wengi hasa katika mataifa tajiri ya Magharibi. Hata hivyo, wanawake wengi mno wamesumbuliwa na kusukumwa hadi kiwango cha talaka. Ili kuzuia matatizo hayo, wote wawili mume na mke wanapaswa kimaombi kupanga tena vipaumbele vyao na kufuata maelekezo ya Biblia juu ya majukumu yao.

Migogoro kuhusu mgao wa kazi katika ndoa hakika hutokea, lakini endapo wapenzi wote wawili ni wanyenyekevu kwa Kristo, migogoro hii itakuwa ndogo. Kama wanandoa hupata mapishano juu ya suala hili mara kwa mara na wakali, au kama mapishano yanaonekana kuwa tabia ya ndoa, tatizo ni la kiroho. Katika hali hiyo, washirika lazima wawe na juhudi wenyewe kwa maombi na kunyenyekea kwa Kristo kwanza, basi kwa mtu mwingine katika mtazamo wa upendo na heshima.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Majukumu ya mume na mke ni gani katika familia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries