settings icon
share icon
Swali

Maadili ya Kikristo ni gani?

Jibu


Maadili ya Kikristo muhtasari wake umetolewa na Wakolosai 3:1-6 : "Basi mkiw mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkon wa kuum wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maan mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huaja ghadhabu ya Mungu."

Huku zaidi ya orodha ya "kufanya" na ya "kutofanya ," Biblia inatupa maelekezo ya kina juu ya namna tunapaswa kuishi. Biblia ndio kila kitu tunahitaji kujua kuhusu jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo. Hata hivyo, Biblia haifuniki kila hali sisi hukumbana nayo katika maisha yetu. Ni jinsi gani ni ya kutosha kwa ajili ya mitanziko yote ya kimaadili sisi hukumbana nayo? Hapo ndipo maadili ya Kikristo yanakujia.

Sayansi yafafanua maadili kuwa "seti ya kanuni za maadili, utafiti wa maadili." Kwa hiyo, maadili ya Kikristo itakuwa kanuni inayotokana na imani ya Kikristo ambayo sisi hutenda. Wakati neno la Mungu linaweza kosa angazia kila hali sisi hupitia katika maisha yetu, kanuni zake hutupatia viwango vya kujiendesha katika hali hizo ambapo hamna maelekezo ya wazi.

Kwa mfano, Biblia haisemi chochote wazi kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, lakini kulingana na kanuni sisi hujifunza kwa njia ya maandiko, tunaweza kujua kwamba ni makosa. Kwa jambo moja, Biblia inatuambia kwamba mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu na kwamba tunapaswa kumheshimu Mungu nao (1 Wakorintho 6:19-20). Kujua ni madawa gani ya kulevya hufanyia miili yetu- madhara hayo husababisha viungo mbalimbali - tunajua kwamba kwa kuyatumia hayo sisi tutakuwa tunaharibu hekalu ya Roho Mtakatifu. Hakika hiyo si kumheshimu Mungu. Biblia pia inatuambia kwamba sisi tunapaswa kufuata mamlaka ambayo Mungu mwenyewe ameweka katika nafasi (Warumi 13:1). Kutokana na hali ya haramu ya madawa ya kulevya, kwa kuyatumia hayo sisi hutujiwasilishi kwa mamlaka lakini tunaasi dhidi yao. Je, hii inamaanisha kwamba dawa ya kulevya haramu yakihalarishwa yatakuwa sawa kutumiwa? Bila kukiuka kanuni ya kwanza.

Kwa kutumia kanuni tunapata katika maandiko, Wakristo wanaweza kuamua bila shaka maadili katika hali yoyote. Katika baadhi ya matukio itakuwa rahisi, kama sheria kwa ajili ya kuishi maisha ya Kikristo tunaona katika Wakolosai, sura ya 3. Katika kesi nyingine, hata hivyo, tunahitaji kufanya kuchimba kidogo. Njia bora ya kufanya hivyo ni kuomba kwa neno la Mungu. Roho Mtakatifu hukaa ndani ya kila muumini, na sehemu ya majukumu yake ni kufundisha jinsi ya kuishi: "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia,"(Yohana 14:26). "Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yankaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama matufa yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake"(1 Yohana 2:27). Hivyo, wakati tunaomba kwa maandiko, Roho atatuongoza na kutufundisha. Atawaonyesha sisi kanuni tunahitaji ili kusimama katika hali yoyote.

Huku kukiwa kwamba neno la Mungu halitoi kila hali sisi hukumbana nayo katika maisha yetu, yote ni ya kutosha kwa ajili ya kuishi maisha ya Kikristo. Kwa mambo mengi, tunaweza tu kuona ni nini Biblia inasema na kufuata mwendo sahihi kwa kuzingatia kanuni hizo. Katika maswali ya kimaadili ambapo maandiko hayatoi mwelekeo wa wazi, sisi tunapaswa kuangalia kwa kanuni ambayo inaweza kutumika katika hali hiyo. Tunapaswa kuomba juu ya neno lake, na kujifungulia sisi wenyewe kwa Roho wake. Roho atatufundisha na kutuongoza katika Biblia kupata kanuni ambazo sisi tunahitaji kusimama kwayo ili tuweze kuishi kama iwapasavyo Wakristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maadili ya Kikristo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries