settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kuwa na uhakika kwamba ninaomba kulingana na mapenzi ya Mungu?

Jibu


Lengo kuu Zaidi la mwanadamu lazima liwe la kuleta utukufu kwa Mungu (1 Wakorintho 10:31), na hii ni pamoja na kuomba kulingana na mapenzi yake. Kwanza, ni lazima tuomba hekima. "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa" (Yakobo 1:5). Katika kuomba hekima, ni lazima pia tuamini bila shauku kwamba Mungu ni wa neema na yu tayari kujibu maombi yetu: "Ila na aombaye kwa Imani, pasipo shaka yoytoe" (Yakobo 1:6, tazama pia Marko 11:24). Hivyo, kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu ni pamoja na kuomba kwa ajili ya hekima (kujua mapenzi ya Mungu) na kuuliza katika imani (kuamini mapenzi ya Mungu).

Hapa kuna maelekezo saba ya kibiblia ambayo yatakuwa yakimwongoza muumini katika kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu:

1) Omba kwa ajili ya mambo ambayo Biblia inaamrisha tuombee. Tunaambiwa tuombee adui zetu (Mathayo 5:44); kwa Mungu kutuma wamishenari (Luka 10:2); kwamba tusiingie katika majaribu (Mathayo 26:41); kwa wahudumu wa neno (Wakolosai 4:3; 2 Wathesalonike 3:1); kwa mamlaka ya serikali (1 Timotheo 2:1-3); kwa msaada kutoka mateso (Yakobo 5:13); na kwa ajili ya uponyaji wa waumini wenzetu (Yakobo 5:16). Ambapo Mungu anaamrisha maombi, tunaweza kuomba kwa ujasiri kwamba tunaomba kulingana na mapenzi yake.

2) Kufuata mfano utauwa katika maandiko. Paulo aliomba kwa ajili ya wokovu wa Israeli (Warumi 10:1). Daudi aliomba kwa huruma na msamaha wakati yeye alitenda dhambi (Zaburi 51:1-2). Kanisa la kwanza liliomba kwa ujasiri lishuhudie (Matendo 4:29). Maombi haya yalfuatana na mapenzi ya Mungu, na maombi sawia hayo hii leo yanaweza kuwa mazuri. Kama Paulo pamoja na kanisa la kwanza, ni sisi lazima tuombe kila wakati kwa ajili ya wokovu wa watu wengine. Kwa wenyewe, ni lazima tuombe kama Daudi aliomba, daima tukiwa na ufahamu ya dhambi zetu na kuzileta mbele ya Mungu kabla zizuie uhusiano wetu na yeye na kupotosha maombi yetu.

3) Omba kwa motisha ya kweli. Nia ya ubinafsi haitabarikiwa na Mungu. "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu" (Yakobo 4:3). Tunapaswa pia kuomba, si kwa maneno yetu ya fahari tuweze kusikika na tuonekane na wengine "kuwa wa kiroho," lakini mara nyingi katika siri na binafsi, ili Baba yetu wa mbinguni atasikia katika siri na kutulipa hadharani (Mathayo 6: 5-6).

4 ) Ombeni na roho wa msamaha kwa wengine (Marko 11:25). Roho wa uchungu, hasira, kisasi au chuki kwa wengine huzuia mioyo yetu kuomba Mungu kwa unyenyekevu. Kama vile tu tunaambiwa kuwa tusitoe sadaka kwa Mungu wakati tuna mgogoro kati yetu na Mkristo wwingine (Mathayo 5:23-24), kwa njia hiyo Mungu hataki sadaka ya maombi yetu hadi pale sisi huridhiana na ndugu zetu na dada katika Kristo.

5) Omba kwa shukrani (Wakolosai 4:2, Wafilipi 4:6-7). Sisi daima tunaweza kupata kitu cha kushukuru, haijalishi mzigo yetu ni mizito namna gani au mahitaji. Anayeteseka Zaidi katika dunia hii ya upendo wa ukombozi, na ambaye ana pendekezo la mbinguni mbele yake, ana sababu ya kumshukuru Mungu.

6) Ombeni bila kukoma (Luka 18:1, 1 Wathesalonike 5:17). Tunapaswa kudumu katika sala na si kuacha au kuzushwa moyo kwa sababu hatujapata jibu haraka. Sehemu ya kuomba katika mapenzi ya Mungu ni kuamini kwamba , kama jibu lake ni "ndiyo" "la," au " kusubiri," sisi hukubali uamuzi wake, kunyenyekea kwa mapenzi yake, na kuendelea kuomba.

7) Mtegemee Roho wa Mungu katika maombi. Huu ni ukweli wa ajabu: "Kadhalika Roho naye hutsaidia udhaifu wetu, kwa maana hatuji kuomba jinsi itupasavyo, lakini roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye miyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu" (Warumi 8:26-27). Tuna msaada wa Roho katika kuomba. Wakati wetu wa huzuni sana au sikitiko, nyakati zile sisi huisi kuwa "siwezi kuomba," tuna faraja ya kujua kwamba Roho Mtakatifu kweli anatuombea! Tunaye Mungu wa ajabu namna gani!

Ni uthibitisho ulioje sis tunao wakati tunatafuta kutembea katika Roho na sio katika mwili! Kisha tunaweza kuwa na uhakika kwamba Roho Mtakatifu hukamilisha kazi yake katika kuwasilisha maombi yetu kwa Baba kulingana na mapenzi yake kamili na muda, na tunaweza kupumzika tukijua kwamba kwamba Yeye anafanya mambo yote pamoja kwa wema wetu (Warumi 8:28).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuomba kadri na mapenzi ya Mungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries