settings icon
share icon
Swali

Je! Ni sawa kufanya mapenzi kabla ya ndoa ikiwa unajua kuwa utamuoa mtu huyo?

Jibu


Kwa mtazamo wa kibinadamu, inaonekana ni jambo la busara kufikiria kuwa ni sawa kwa wanandoa kufanya ngono ikiwa watafunga ndoa hivi karibu. Neno la Mungu lina amri iliyo wazi na ya moja kwa moja juu ya mada hii: “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote” (Waebrania 13:4). “Wazinzi” katika mstari huu ni pamoja na wale wote wanaofanya ngono nje ya ndoa. Ulimwengu unachukulia uasherati kwa njia rahisi, lakini sivyo na Mungu.

Paulo anawahimiza Wakristo wa Korintho, akisema, “Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke. Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe” (1 Wakorintho 7:1-2). Maneno yake baadaye yatawatia moyo wale wanoweza kuishi pasipo mwenzi na useja ili kumtumikia Kristo kikamilifu (1 Wakorintho 7:7-9, 25-40). Kibiblia, muktadha pekee unaofaa kwa mahusiano ya ngono ni ndoa. Wale ambao “watafunga ndoa” kwa ufafanuzi, hawajaoa na hawapaswi kuishi kana kwamba wameolewa.

Katika utamaduni wa Kiyahudi, chini ya Sheria ya Musa mahusiano ya ngono yaliwekewa vizuizi waziwazi hadi wakati wa ndoa. Ingawa uchumba ulizingatiwa kuwa makubaliano ya lazima, mahusiano ya ngono bado yalikuwa na vizuizi hadi wakati wa ndoa halisi. Mara ya kwanza mwanamume na mwanamke walipofanya ngono pamoja ilizingatiwa kuwa utimilifu wa ndoa. Matendo haya mawili—ndoa na kujamiiana—yalihusiana sana kiwango kwamba yanakaribia kufanana. Hii inaeleza kwa sehemu ni kwa nini Yesu alijibu swali la Mafarisayo kuhusu talaka kwa kusema, “Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini” (Mathayo 19:9).

Paulo anafafanua wazo hili katika 1 Wakorintho 6:12-20, katika mjadal wake wa ubwana wa Mungu juu ya miili yetu na pia roho zetu. Anasema kwamba, mwanamume anapofanya ngono na kahaba, amekuwa “mmoja naye katika mwili” (mstari 16). Ni wazi kwamba uhusiano wa kimapenzi, haijalishi muktadha, ni maalum. Kuna kiwango cha adhari ambacho mtu anapitia katika uhusiano wa kimapenzi ambao Mungu anataka uhifadhiwe ndani ya muungano wa ndoa wa kujitolea na unaoaminika. Hata kama unafikiri utamuoa huyo mtu, ni muhimu kuheshimiana kwa kusubiri hadi mtakapofunga ndoa kweli ndipo mkajamiiane.

Kuwa na mipango ya ndoa kwa wakati ujao hakumpi mtu yeyote haki ya kutotii amri za Mungu zilizo wazi katika Maandiko. Ikiwa unapanga kuolewa, pongezi. Lakini, katika kupanga kwako, mheshimu Mungu na mheshimu mwenzi wako wa baadaye. Ngono kabla ya ndoa ni jaribu kwa kila wanandoa waliochumbiwa au wanochumbiana, linalohitaji tahadhari na kujitolea kutembea katika Roho. Fikiria mipango yako ya harusi. Fikirini juu ya wema wa Mungu kwenu kama wanandoa. Lakini “msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi”

Kwa wale ambao wameshiriki ngono kabla ya ndoa, kuna matumaini na msamaha katika Kristo. Tikiungama dhambi zetu, atatusamehe na kutusafisha na “udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Njia mpya ya usafi inaweza kuanza leo, kwa kujitolea pya kuishi maisha safi kingono hadi ndoa, licha ya maisha ya zamani ya mtu. Kama Paulo alivyoandika, “Ndugu zangu, sijihesabu kuwa nimekwisha kushika. Lakini ninafanya jambo moja: Ninasahau mambo yale yaliyopita, nakaza mwendo kufikia yale yaliyo mbele. Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Kristo Yesu” (Wafilipi 3:13-14).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni sawa kufanya mapenzi kabla ya ndoa ikiwa unajua kuwa utamuoa mtu huyo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries