settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya Kila kitu kina Uungu?

Jibu


Kila kitu kina Uungu ni mtazamo kwamba Mungu ni kila kitu na kila mtu na kwamba kila mtu na kila kitu ni Mungu. Kila kitu ni chaghj Uungu ni sawa na ushirikina (imani katika miungu wengi), lakini inaenda zaidi ya ushirikina na kufundisha kwamba kila kitu ni Mungu. Mti ni Mungu, mwamba ni Mungu, mnyama ni Mungu, anga ni Mungu, jua ni Mungu, wewe ni Mungu, nk Kila kitu kina Uungu ni dhana iliyo nyuma ya ibada na dini za uongo (kwa mfano, Uhindu na Ubuddha kwa kiasi, mbalimbali umoja wa muungano wa dini, na "mama asili" waja).

Je Biblia inafundisha kuhusu ikiwa kila kitu kina Uungu? La!, haifunzi. Chenye watu wengi hushindwa kutofautisha ni kama Kila kitu kina Uungu ni mafundisho ya Mungu kuwa kila mahali. Zaburi 139:7-8 inasema, "Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kam ningepand mbinguni, Wewe uko; ningefanya kuzimu kitakdna changu, Wewe uko." Mungu yuu kila mahali maana yake ni sasa na Yeye kuwa kila mahali. Hakuna nafasi katika ulimwengu ambapo Mungu hayuko. Hii sio sawia na Kila kitu kina Uungu. Mungu ako kila mahali, lakini si kila kitu. Naam, Mungu yupo "sasa" ndani ya mti na ndani ya mtu, lakini hiyo haimfanyi mti huo au mtu huyo Mungu. Kila kitu kina Uungu kwa vyovyte vile sio imani ya Biblia.

Hoja ya wazi ya kibibilia dhidi ya Kila kitu kina Uungu ni amri sisizohesabika dhidi ya ibada ya sanamu. Biblia inakataza ibada ya sanamu, malaika, vyombo mbinguni, vitu katika asili, nk Kama Kila kitu kina Uungu ni kweli, haitakuwa makosa kuabudu vyombo kama hivyo, kwa sababu chombo hicho kitakuwa ni Mungu. Kama Kila kitu kina Uungu ni kweli, kuabudu mwamba au wanyama ingekuwa na uhalali tu kama vile kuabudu Mungu asiyeonekana na ustawi wa kiroho. Biblia hii wazi na thabiti kwa kuukana ibada ya sanamu ni hoja adilifu ya hitimisho dhidi ya Kila kitu kina Uungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya Kila kitu kina Uungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries