settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kifo cha huruma?

Jibu


Kifo cha huruma linaweza kuwa suala gumu sana. Kuna pande mbili ambazo kwamba ni vigumu kuweka katika mizani. Upande mmoja, hatutaki kuchukua maisha ya mtu kwa mikono yetu wenyewe na kuyakomesha mapema. Kwa upande mwingine, ni katika hatua gani sisi tunapaswa kuruhusu mtu kufa na bila kuchukua hatua yoyote zaidi ya kuyaokoa maisha yake?

Ukweli mkuu ambao unatoa kauli kwamba Mungu anapinga kifo cha huruma ni ukuu wake. Tunajua kwamba kifo cha kimwili ni lazima (Zaburi 89:48; Waebrania 9:27). Hata hivyo, Mungu peke yake ndiye mwenyezi nguvu wa wakati na jinsi kifo cha mtu hutokea. Ayubu anathibitisha katika Ayubu 30:23, "Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, niifikilie nyumba waliyoandikiwa weny uhai." Mhubiri 8:8a inasema, " Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho, wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa" Mungu ndiye ana uamuzi wa mwisho juu ya kifo (tazama pia 1 Wakorintho 15:26, 54-56, Waebrania 2:9, 14-15; Ufunuo 21:4). Kifo cha huruma ni njia ya mtu ya kujaribu kunyakua mamlaka hayo kutoka kwa Mungu.

Kifo ni tukio asili. Wakati mwingine Mungu anamruhusu mtu kuteseka kwa muda mrefu kabla ya kifo kutokea; mara nyingine, mateso ya mtu hukatishwa. Hakuna mtu anayefurahia mateso, lakini hiyo haifanyi kuwa haki kuamua kwamba mtu yuko tayari kufa. Mara nyingi makusudi ya Mungu hujitambulisha kwa njia ya mateso ya mtu. "Siku ya kufanikiwa ufurahi, na siku ya mabay ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili..." (Mhubiri 7:14). Warumi 5:3 inatufundisha kwamba mateso huleta uvumilivu. Mungu huwajali wale wote ambao wanaita kifo ili kukomesha mateso yao. Mungu anatoa lengo kwa maisha hata hatima yake. Ni Mungu tu anajua lilo bora, na muda wake, hata katika suala la kifo cha mtu, li kamilifu.

Wakati huo huo, Biblia haiamrishi kufanya kila kitu tunachoweza kumweka mtu hai. Kama mtu ameweka hai ni kifaa/ mashine, siyo kinyume cha maadili ukizima mashine na kuruhusu mtu kufa. Kama mtu amekuwa katika hali ya kuendelea na ugunjwa kwa muda mrefu, haitakuwa kwa kosa Mungu kuondoa kifaa chochote kilichoko / mashine ambayo inamweka mtu hai. Je Mungu an haja ya kumweka mtu hai, ako na uwezo kikamilifu wa kufanya hivyo bila ya msaada wa vifaa vya kulishia chakula / au mashine.

Kufanya uamuzi kama huu ni vigumu sana na chungu. Kamwe si rahisi kumweleza daktari kukiondoa kifaa kinacho mpa msaada mpendwa. Sisi kamwe tusitafute kamaliza mapema maisha kwa njia isiyo faa, lakini wakati huo huo, wala sisi kwendea njia za ajabu ili kuhifadhi maisha ya watu. Ushauri bora kwa mtu yeyote anayekabiliwa na uamuzi huu ni kuomba kwa Mungu kwa hekima (Yakobo 1:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kifo cha huruma?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries