settings icon
share icon
Swali

Ni lengo gani la kanisa?

Jibu


Matendo Ya Mitume 2:42 yaweza kuchukuliwa kama ujumbe wa lengo la kanisa: “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na kitaka kuumega mkate, na katika kusali.” Kulingana na aya hii, lengo/kazi ya kanisa yastahili kuwa 1) Kufunza funzo la kibibilia, 2) Kutoa mahali pa ushirka kwa wakristo, 3) Kushiriki mesa ya bwana/kuumega mkate, na 4) Maombi.

Kanisa yafaa kufundisha funzo la kibibilia ili tuweze kukua katika misingi ya imani yetu. Waefeso 4:14 yatwambia, “Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” Kanisa lastahili kuwa mahali pa ushirika, mahali ambapo wakristo wamejitoa kwa kupendena na kuheshimiana wao kwa wao (Warumi 12:10), kuonyana (Warumi 15:14), wafadhili na huruma wao kwa wao (Waefeso 4:32), kutiana moyo wao kwa wao (1 Wathesalonike 5:11), na muhimu sana kupenda wao kwa wao (1 Yohana 3:11).

Kanisa linastahili kuwa mahali ambapo wakristo wanashiriki mwili wa Yesu, kwa kukumbuka kifo cha Yesu na damu aliyoimwaga kwa ajili yetu (1 Wakorintho 11:23-26). Dhana ya “kuumega mkate” (Matendo Ya Mitume 2:42) pia yabeba dhana ya kuwa na chakula cha pamoja. Huu ni mfano mwingine wa kanisa kukuza ushirika. Lengo la mwisho la kanisa kulingana na Matendo Ya Mitume 2:42 ni maombi. Kanisa linastahili kuwa mahalipa kukuza maombi, kufunza juu ya maombi na kufanya zoezi la maombi. Wafilipi 4:6-7 yatupa moyo kuwa, “Msijusumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akii zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

Jukumu liningine kanisa imepewa ni ile kuitangaza injili ya wokovu kupitia Yesu Kristo (Mathayo 28:16-20; Matendo Ya Mitume 1:8) kanisa limeitwa kuwa aminifu katika kushiriki injili katika usemi na katika matendo. Kanisa inastahili kutangaza injili na pia kutayarisha washirika wake kuitangaza injili (1 Petero 3:15).

Baadhi ya malengo ya mwisho ya kanisa yametolewa katika Yakobo 1:27: “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.” Kanisa inastahili kujiuzisha na kuhudumia wale walio na maitaji, si kwa kushiriki injili pekee. Hii haimanishi kushiriki injili pekee, pia kutoa msaada kama wa (chakula, nguo and makazi) vile inavyostahili na kuitajika. Kanisa pia inastahili kuwandaa wakristo na silaha wanazozihitaji ili kuishinda dhambi na kukaa huru kutoka na mitego ya ulimwengu. Hii inafanyika kupitia kwa mafunzo ya Bibilia na ushirika wa wakristo.

Kwa hivyo, ni lengo gani la kanisa? Paulo alitoa elezo kamilifu kwa wakristo wa korintho. Kanisa ni; mikono ya Mungu, mdomo wa Mungu na miguu ya Mungu katika ulimwengu-mwili wa Kristo (1 Wakristo 12:12-27). Yatupasa tufanye mambo yale Kristo mwenyewe angeyafanya angekuwa nasi hii leo. Kanisa inastahili kuwa “Mkristo” “kama Kristo” na kufuata nyayo za Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni lengo gani la kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries