settings icon
share icon
Swali

Jehanamu inaonekanaje? Jehanamu ina joto kiasi gani?

Jibu


Hatuwezi kujua hasa jehanamu inaonekanaje au itakuwa na joto kiasi gani. Lakini Maandiko hayatumii lugha ya maelezo juu ya kuzimu, na hiyo inatupa wazo la jinsi kuzimu kutakavyokuwa. Bila shaka patakuwa mahali pa mateso, ambapo Biblia hufananisha mara nyingi kuwa moto. Kwa madhumuni ya nakali hii, maneno kuzimu na ziwa la moto yanatumika kwa mkabala.

Wafasiri wengine wanachukulia maelezo ya Biblia ya kuzimu kuwa ya mfano, kwa sababu baadhi ya maelezo ni vigumu kupatana. Kwa mfano, kufananisha kuzimu na moto (Mathayo 25:41) na giza la nje (Mathayo 8:12) inaonekana kuwa ya kitendawili. Bila shaka, Mungu wa yasiyowezekana anaweza kufanya lolote ikiwa ni pamoja na kuunda moto totoro. Kwa hivyo, maelezo yanaweza kuwa halisi. Hata ikiwa lugha inayoeleza kuzimu ni ya mfano, mahali penyewe ni halisi-na bila shaka hali halisi itakuwa mbaya zaidi kuliko ishara.

Ufafanuzi wa kimaandiko wa kuzimu unakusudiwa kusisitiza mateso na masumbuko yatakayowapata wale wanaotumwa huko. “Moto” huo unaweza kuwa picha ya ghadhabu ya Mungu ambayo watu wasioamini hupitia jehanamu, ilihali “giza la nje” linaweza kuonyesha kutengwa na upendo, rehema na neema ya Mungu. Iwe lugha iliyo wazi na ya mfano au halisi, tunaweza kuwa na uhakika kwamba kuzimu ni mahali pabaya na pa kuogopesha. Huenda kipengele cha kutisha zaidi cha kuzimu ni muda wake. Mateso ya milele. Haina mwisho. Kwetu sisi, hapa na sasa, dhana ya kuzimu inapaswa kutupeleka kwenye msalaba wa Kristo. Ni kwa toba tu na imani katika Kristo tunaweza kuokolewa kutoka kwa ghadhabu inayokuja.

Hapa kuna baadhi ya vifungu vinavyoelezea kuzimu:

Mathayo 25:41, “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.”

Mathayo 8:12, “Lakini warithi wa Ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwako kilio na kusaga meno.”

2 Wathesalonike 1:6-9, “Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake.”

Ufunuo 20: 10, 15, “Naye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo usiku na mchana, milele na milele… Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.

Warumi 2:8, “Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.”

Mathayo 25:30, “Nanyi mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje, kwenye giza, mahali ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.”

Kuzimu, ingawa hatujui jinsi itakavyokuwa hasa, kutakuwa mahali pa mateso na masumbuko yasiyo na mwisho ambapo hapatakuwa na njia ya kuepuka. Kwa hiyo, sasa ni siku ya wokovu. Sasa ni siku ya wote kutubu na kuiamini injili. Sasa ndioyo siku sisi kutangaza habari njema kwamba Kristo amekuja kuwaokoa wenye dhambi wanaomtumaini kwa ajili ya msamaha. Wale wanaomtazama Kristo sasa wataokolewa kutoka kwa ghadhabu inayokuja (1 Wathesalonike 1:9-10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Jehanamu inaonekanaje? Jehanamu ina joto kiasi gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries