settings icon
share icon
Swali

Tunawezaje kujiwekea hazina mbinguni?

Jibu


Yesu alituambia “Lakini jiwekeeni hazina mbinguni” (Mathayo 6:20). Aliunganisha amri hii na tamaa ya mioyo yetu: “Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa” (Mathayo 6:21; soma pia 10-12).

Biblia inataja thawabu zinazomngoja muumini anaymtumikia Bwana kwa uaminifu katika ulimwngu huu (Mathayo 10:41). Thawabu “kubwa” imeahidiwa wale wanaoteswa kwa ajili ya Yesu. Taji mbalimbali zimetajwa (katika 2 Timotheo 4:8, k.m). Yesu anasema kwamba Ataleta thawabu pamoja naye atakaporudi (Ufunuo 22:12).

Tunapaswa kumthamini Bwana Yesu zaidi ya yote. Yesu anapokuwa hazina yetu, tutakabidhi rasilimali zetu-fedha zetu, wakati wetu, talanta zetu-kwa kazi Yake katika ulimwengu huu. Msukumo wetu kwa kile tunaochafanya ni muhimu (1 Wakorintho 10:31). Paulo anawatia moyo watumishi kwamba Mungu ana thawabu ya milele kwa wale wanaochochewa kumtumikia Kristo: “Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia” (Wakolosai 3:23-24).

Wakati tunaishi kwa kujitolea kwa ajili ya Yesu au kumtumikia kwa kutumikia mwili wa Kristo, tunaweka hazina mbinguni. Hata kama matendo ya utumishi yanayoonekana kuwa madogo hayaendi bila kutambuliwa na Mungu. “Kama yeyote akimpa hata kikombe cha maji baridi mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, amin, nawaambia, hataikosa thawabu yake” (Mathayo 10:42).

Wengine walio na karama zinaoonekana wazi (ongalia 1 Wakorintho 12) kama vile kufunidisha, kuimba, au kucheza ala ya muziki wanaweza kujaribiwa kutumia karama zao kwa utukufu wao wenyewe. Wale wanaotumia karama zao au vipaji vyao kiroho kutamani sifa za wanadamu badala ya kutafuta utukufu wa Mungu hupokea “malipo” yao kikamilifu hapa na sasa. Shangwe ya wanadamu ilikuwa kiwango cha thawabu kwa Mafarisayo (Mathayo 6:16). Kwa nini tunapaswa kufanyia kazi sifa za kilimwengu, hata hivyo, wakati tunaweza kuwa na mengi zaidi mbinguni?

Bwana atakuwa mwaminifu kutupa thawabu kwa ajili ya huduma tunayompa (Waebrania 6:10). Huduma zetu zinaweza kutofautiana, lakini Bwana tunayemtumikia ni yule yule. “Apandaye mbegu ana lengo sawa na yule atiaye maji na kila mmoja atalipwa kulingana na kazi yake” (1 Wakorintho 3:8).

Kijana Tajiri alipenda pesa zake kuliko Mungu katika Mathayo 19:16-30, ukweli ambao Yesu alitaja. Suala halikuwa kwamba kijana huyo alikuwa Tajiri, bali kwamba “alithamini” utajiri wake na “hakuweka hazina” kile ambacho angeweza kuwa nacho katika Kristo. Yesu alimwambia mtu huyo auze mali yake na kuwapa maskini. “nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate” (aya ya 21). Yule kijana alimwacha Yesu akiwa na huzini, kwa sababu alikuwa tajiri sana. Alichagua hazina ya ulimwengu huu na hivyo hakujjiwekea hazina mbinguni. Hakuwa tayari kumfanya Yesu kuwa hazina yake. Kijana huyo alikuwa mtu wa kidini sana, lakini Yesu alifichua moyo wake wa pupa.

Tunaonywa tusipoteze thawabu yetu kamili kwa kufuata waalimu wa uongo (2 Yohana 1:8). Hii ndiyo sababu ni muhimu sana kuwa katika Neno la Mungu kila siku (2 Timotheo 2:15). Kwa njia hiyo tunaweza kutambua mafundisho ya uongo tunapoyasikia.

Hazina zinazomngoja mtoto wa Mungu zitashinda shida yoyote, masumbuko, au mateso tunayoweza kukabiliana nayo (Warumi 8:18). Tunaweza kumtumikia Bwana kwa moyo wote, tukijua kwamba Mungu ndiye anayeweka alama, na thawabu yake itakuwa ya nema nyingi. “Simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure” (1 Wakorintho 15:58).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunawezaje kujiwekea hazina mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries