settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu alitaka dhabihu ya wanyama katika Agano la Kale?

Jibu


Mungu alihitaji dhabihu ya wanyama kwa kutoa msamaha wa dhambi kwa muda na kivuli chake hakika na kamilifu ni dhabihu ya Yesu Kristo (Mambo ya Walawi 4:35, 5:10). Sadaka ya wanyama ni mandhari muhimu hupatikana katika maandiko kwa sababu "pasipo kumwaga damu hakuna msamaha" (Waebrania 9:22). Wakati Adamu na Hawa walitenda dhambi, wanyama waliuawa na Mungu kufanya nguo kwa ajili yao (Mwanzo 3:21). Kaini na Habili walileta sadaka kwa Bwana. Kaini hakukubaliwa kwa sababu yeye alileta matunda, huku Habili ilikubalika kwa sababu ilikuwa ni "zao la kwanza la kundi lake" (Mwanzo 4:4-5). Baada ya mafuriko kumalizika, Nuhu alitoa sadaka ya wanyama kwa Mungu (Mwanzo 8:20-21).

Mungu aliamuru taifa la Israeli kufanya sadaka mbalimbali kulingana na baadhi ya utaratibu uliowekwa na Mungu. Kwanza, mnyama alikuwa asiye na doa. Pili, mtu anayetoa sadaka lazima ajitambulishe na mnyama. Tatu, mtu wa kutoa sadaka ya mnyama ni yeye alifaa kumuua mnyama wa sadaka. Wakati ilifanywa kwa imani, sadaka hyoi ilitoa msamaha wa dhambi. Sadaka nyingine iliyotolewa wakati wa Siku ya Upatanisho, yaelezewa katika Mambo ya Walawi 16, inaonyesha msamaha na kuondolewa kwa dhambi. Kuhani Mkuu alikua achukue beberu wawili, kwa sadaka ya dhambi. Mmoja wa mbuzi alikuwa sadaka ya dhambi kwa watu wa Israeli (Mambo ya Walawi 16:15), wakati mbuzi mwingine aliachiliwa katika jangwa (Mambo ya Walawi 16:20-22). Sadaka ya dhambi ni ya msamaha, wakati mbuzi nyingine zinazotolewa kuondolewa kwa dhambi.

Ni kwa nini, basi, hii leo sisi hatutia dhabihu za wanyama? Sadaka za wanyama zimeisha kwa sababu Yesu ndiye dhabihu ya mwisho na kamilifu sadaka. Yohana Mbatizaji alitambua hili alipoona Yesu akija kubatizwa na akasema, "Tazama, mwana-kondoo wa Mungu aichukuaaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29). Unaweza kujiuliza wewe mwenyewe, kwa nini wanyama? Je, wao walifanya makosa? Hiyo ni hatua- tangu wanyama hakufanya makosa, walikufa kwa niapai ya aliyetoa kafara. Yesu Kristo pia alifanya kosa bali kwa hiari alijitoa nafsi yake kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote (1 Timotheo 2:6). Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu juu yake mwenyewe na kufa kwa ajili yetu. Kama 2 Wakorintho 5:21 inasema, "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye." katika njia ya imani mambo ambayo Yesu Kristo aliyatimisha juu ya msalaba, sisi tunaweza kupokea msamaha.

Kwa kuhitimisha, sadaka za wanyama ziliamriwa na Mungu ili mtu aweze kupata msamaha wa dhambi. Mnyama aliwahi kuwa mbadala - yaani, mnyama alikufa kwa ajili ya mwenye dhambi, lakini kwa muda tu, ambayo ndio sababu ni kwa nini sadaka ilihitajika kutolewa tena na tena. Sadaka za wanyama na kusimamishwa na Yesu Kristo. Yesu Kristo ndiye alikuwa kafara kuu mbadala mara moja kwa wakati wote (Waebrania 7:27) na Yeye ndiye sasa mpatanishi kati ya Mungu na binadamu (1 Timotheo 2:5). Sadaka za wanyama ilikua kivuli cha sadaka ya Kristo kwa niaba yetu. Msingi pekee ambao dhabihu ya mnyama inaweza kutoa msamaha wa dhambi ni Kristo ambaye alijitoa kama sadaka yeye mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu, kutoa msamaha kwamba dhabihu za wanyama inaweza tu kuonyesha kivuli cha yatakayo tokea.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu alitaka dhabihu ya wanyama katika Agano la Kale?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries