settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu ngono ya mdomo?

Jibu


Ngono ya mdomo, inayojlikana pia ka “cunnilingus” inapofanywa kwa wanawake na “fellatio” inapofanywa kwa wanaume haijatajwa katika Biblia. Kuna maswali mawili ya msingi yanaoyoulizwa kuhusiana na ngono ya mdomo: (1) “Je, ngono ya mdomo ni dhambi ikifanywa kabla ya ndoa?” na (2) Je, ngono ya mdomo ni dhambi ikifanywa ndani ya ndoa?” Ingawa Biblia haiangazii swali lolote moja kwa moja, kwa hakika kuna kanuni za kibiblia zinazotumika.

Je! ngono ya mdomo ni dhambi ikiwa imefanywa kabla au nje ya ndoa?
Swali hili linazidi kuwa la kawaida miongoni mwa vijana wanapoambiwa kwamba “ngono ya mdomo si ngono haswa,” na jini ngono ya mdomo inavyokuzwa kuwa salama zaidi (hakuna hatari ya kupata mimba, hatari ndogo ya magonjwa ya zinaa*) badala ya kujamiiana. Biblia inasema nini? Waefeso 5:3 inatangaza, “Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu.” Ufafanuzi wa kibiblia wa “uasherati” ni “aina yoyote ya kujamiiana nje ya ndoa” (1 Wakorintho 7:2). Kulingana na Biblia, ngono inapaswa kutengwa kwa ajili ya ndoa (Waebrania 13:4). Kwa hiyo, naam, ngono ya mdomo ni dhambi ikiwa inafanywa kabla au nje ya ndoa.

Je! ngono ya mdomo ni dhambi ikifanywa ndani ya ndoa?
Wengi wa wanandoa Wakristo wamekuwa na swali hili. Kinachofanya iwe vigumu ni ukweli kwamba Biblia haisemi popote ni nini inaruhusiwa au kukataliwa kuhusu ngono kati ya mume na mke, isipokuwa, bila shaka, ngono yoyote inayohusisha mtu mwingine (kubadilishana, ngono ya watu watatu, n.k.) au inayohusisha kumtamani mtu mwingine (ponografia). Kando na vikwazo hivi viwili, kanuni ya “makubaliano ya pande zote mbili” ingeonekana kutumika (1 Wakorintho 7:5). Ingawa maandiko haya yanahusu hasa kujiepusha na ngono/ya mara kwa mara, “makubaliano ya pamoja” ni dhana nzuri kutumika ulimwenguni kote kuhusiana na ngono ndani ya ndoa. Chochote kinachofanyika kinapaswa kukubalika kikamilifu kati ya mume na mke wake. Hakuna mume au mke anayepaswa kulazimishwa au kushawishiwa kufanya jambo ambalo hafurahishwi nalo kabisa. Ikiwa ngono ya mdomo inafanywa ndani ya mipaka ya ndoa na kwa roho ya kuridhiana, hakuna kifungu cha kibiblia kinachoitangaza kuwa ni dhambi.

Kwa muhtasari, ngono ya mdomo kabla ya ndoa ni dhambi kabisa. Ni uasherati. Kwa vyovyote vile si njia mbadala inayokubalika kibiblia badala ya kujamiiana kwa watu ambao hawajafunga ndoa. Ndani ya mipaka ya ndoa, kujamiiana kwa mdomo sio dhambi ili mradi kuna maridhiano.

Ingawa kuna usalama katika kujamiiana kwa mdomo kuambatana na magonjwa ya zinaa, ambako yi salama. Klamidia, kisonono, malengelenge, Ukimwi, na magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kuambukizwa kupitia ngono ya mdomo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu ngono ya mdomo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries